Dunia nzima ukisikia jina Ukechukwu, Obina directly linakupeleka kwenye asili yake. Ukisikia Patel, Sanjay, unapata asili yake. Ukisikia Yamamoto, Sadaaki Numata unapata mwanga huyo asili yake wapi. Hali kadhalika kwa Tanzania ukisikia majina kama Kamugisha, Aika, Bhoke unapata picha asili yao.
Nisiandike mengi lakini kuna nguvu katika kuikubali asili yako. Kwanza inaonesha ni jinsi gani kama jamii husika mnajiamini. Pili inapeleka ujumbe kuwa mnauimara na asili yenu na historia yenu.
Sasa tuje kizazi cha sasa, kuna wimbi kubwa sana la 'Ulimbukeni' na ushamba (ndio hivo) miongoni mwetu Watanzania hasa mtu akijua kusoma na kuandika au akiongeza na ka elimu kengine kwa juu. Kidogo utaskia mwanangu anaitwa Jayden, Brighton, Luqman, Norman, Umulkheir, Lincoln, Gianna mara Jadon, haya majina nimeyataja maksudi kwasababu yalikuja juzi juzi tu na upepo wa karate kid 2.
Basi mtanganyika hapo akafanikiwa kumpeleka english medium alafu ukakakuta kwenye watu wengi alafu kakaongea vile vingereza yani watu wanakafanya kavutio cha utalii kabisa kisa kinge. Yani bongo bana. Yani wanaona big deal yani hapo ndio mafanikio yapo kileleni kwa akili za Watanzania. Akili za kitumwa.
Kuna usemi "mkataa kwao mtumwa". Huu usemi una maana kubwa sana. Ukiangalia majina niliyoyataja hapo mwanzo , mataifa yao na yakwetu tunaojidharau asili zetu maendeleo ni tofauti kabisa. Nigeria pamoja na kuwa ni Africa, bado wanafahamika na kuheshimika sana kuanzia kwenye michezo mpaka sayansi. Hali kadhalika Japan , India pia. Ila sisi ambao utakuta mtoto anaitwa Jaden John Emmanuel ndio tupo kama tulivyo.
Wito wangu, ifike mahali tuache ulimbukeni, tujikubali kwanza ndio dunia itatukubali. Nimeamua mimi watoto wangu wote nawapa majina ya kinyumbani yenye maana nzuri ambayo ata padri wakati wa kubatiza hatutasumbuana. Yani ninataka kutengeneza identity. Kataa utumwa wewe chausiku.