Kuna wimbi kubwa sana la Ulimbukeni na ushamba kwa Watanzania hasa Mtu akijua kusoma na kuandika

Cha kushangaza anayeyatukuza majina ya kizungu ukicheki maana zake utaona ni ovyo tu, mtu anaitwa ROCK, SMITH, SOAP, CLIFF, WOOD, DINNER, CROOK N.K, sijui uwaga hawazijui tafsiri zake..
 
Niligombana Sana na mke wangu juu ya jina la kabinti kangu, nimempa jina la bibi yangu ambaye ndiye alinilea utoto wangu wote ila yeye akakomaa kuwa majina ya asili Yana laana nilitaka kumzabua na makofi Kwa dharau nikamwambia Hilo jina lake aliloshauriana na mashosti zake sitaki kulisikia mahala popote jina la Dini atatumia lile la bibi yangu alilokuwa anatumia,
 
Majina Kama Wampuka,Wandisha,Wankembeta,wanswekula,Wampumbulya nk. Yamekuwa adimu Sana huku kwetu wamejaa akina Mary,Mariam,Queen na Angel.

Ila mi naona ni sawa tu maana hata usafiri wetu wa asili Kama Punda hamtaki Tena mnataka ma V8.
 
Kwanini na wewe usingejiita Nyangema au Atuchomile Mwakachanjo
 
Usichukulie poa jina lina maana kubwa sana katika maisha,jina ndio muongozo wa maisha ya binadamu!
 
Ni kweli, ndio maana nchi zinazotumia majina yao ya asili zina maendeleo kuliko wanaotumia majina ya kukopa.
Usichukulie poa jina lina maana kubwa sana katika maisha,jina ndio muongozo wa maisha ya binadamu!
 
Kabisa. Na utakuta lina maana nzuri tu. Kisa alisound ki instagram basi halitakiwi.
 
Hawajui mazezeta. Yani wameaminishwa uzungu ni superior. Ndio slave mentality yenyewe.
Cha kushangaza anayeyatukuza majina ya kizungu ukicheki maana zake utaona ni ovyo tu, mtu anaitwa ROCK, SMITH, SOAP, CLIFF, WOOD, DINNER, CROOK N.K, sijui uwaga hawazijui tafsiri zake..
 
Kuna hili jina Chogolo sijui limekaa je. Kuna majina yalioenda shule kama Chris Wallace, Franco Da'costa, Rodger Stones, Mcmanaman Littlejohn.
Yatafutie maana yake halisi. Wenzenu hayo ni ya asili ya kwao. Ya kwenu je? Kujipendekeza tu, ndio maana mnadharaulika maana hamjikubali.
 
Yatafutie maana yake halisi. Wenzenu hayo ni ya asili ya kwao. Ya kwenu je? Kujipendekeza tu, ndio maana mnadharaulika maana hamjikubali.
Kama wewe unajikubali kwa nini usitembee uchi ama kuvaa majani na kula mizizi?
 
Mkuu,watu wanaepuka majina ya asili hasa yanayoonyesha ukabila kwa sababu nyingi.
Mfano Kuna kipindi nafasi za masomo ya juu na ajira viliangalia Sana ukanda.
Hivyo ili kuepuka ubaguzi ktk hizo nafasi inabidi mtoto aandikishwe majina ambayo hayatamtambulisha,
Mf Juma Hamid Idd,John Andrew Peter nk.
Nafikiri ukichunguza kwa makini utaelewa mengi kuhusu ukanda ukabila unavyoleta shida.
 
Umenena vema sana….ubovu wetu mkubwa ni kukumbatia tamaduni za kigeni eti ndio ujanja….na katika kila nyanja ya maisha…
 
Majina ya kiswahili sasa, sukununu, chausiku, mchambawima, si ndio hivyo ndugu zangu?
 
Fanya kitu roho inapenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…