Kuna wizi wa vifaa vya magari maeneo ya Goba, Mbezi na Temeke

Tyrex

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
2,373
Reaction score
5,100
Habari wana JF

Kuna wizi mpya wa vifaa vya magari naona umekithiri sana huko maeneo ya Goba, Mbezi, Temeke watu wanaibiwa sana vifaa naomba Ma RC , POLISI N.K walishugulikie hili swala wezi wanajulikana n wanaonunua hivo vifaa vya wizi wanajulikanaa.


 
Masoko yao sio kificho na serikali ikitaka kudhibiti ni rahisi tu! Ni kuweka utaratibu wa manunuzi ambao ni rahisi kufatilia hata kama ni maduka bubu. Kuna biashara hazina control kabisa na sababu pia kuwa zipo level ya local authorities!

Inabidi itungwe sheria maalum kwaajili ya udhibiti wa biashara kama hizi bila kuathiri wanaofanya kihalali.
 
Na kuna mitaa ya kkoo ukienda unavikuta vitu vyako Kama vilivyo Ila utaambiwa uvinunue....!!mjini shule
One time ndugu yangu almanusura aue watu wa kuuza vifaa vya spea za magari.

Aliibiwa kama hivi akiwa amesafiri, aliporudi akajaza risasi kwenye bastola yake akaenda kwenye hayo maduka akakuta vitu vyake, akawaomba wakamwambia avinunue, tunashukuru kwamba mambo yaliisha vizuri akachukua vitu vyake bila shida ila kijana wa dukani hatasau kilichomkuta.

Hawa jamaa wamerudi tena.
 
Nilikuwa naona huruma sana mwizi akichomwa moto,lakini kwa hali hii acha wachomwe tu mtu unapambana usiku kucha kutafuta pesa jua lako mvua yako halafu mpumbavu mmoja anakuja kuchukua kirahisi,kinachouma humiza zaidi wanajitamba utasikia mjini shule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…