Mahusiano yanayojengwa juu ya misingi ya tamaa, uzinzi na uasherati huwa hayadumu kamwe.
Tamaa za mwili zikisharidhishwa huwa zina kawaida ya kuhamia kwa mwingine. Kwa mfano :
Ukimtamani mwanamke mwenye makalio makubwa, ukimpata na kulala naye, ile hamu huwa inaisha na ukimwona mwanamke mwingine mwenye makalio makubwa zaidi ya huyu uliyenaye, tamaa yako itahamia kwake.
Vivyo hivyo na wanawake, ukianzisha mahusiano na mwanaume sababu ya pesa, siku ukikutana na mwanaume mwingine mwenye kukuhonga pesa nyingi zaidi, tamaa yako yote itahamia kwake na kumsahau huyo uliyenaye.
Hivyo ndivyo mfumo wa uzinzi na uasherati unavyoendeshwa. Msingi au nguzo kuu ya uzinzi na uasherati ni tamaa. Tamaa ya mwili kwa wanaume na tamaa ya pesa kwa wanawake.
Ndiyo maana mnaambiwa ikimbieni zinaa. Tena maandiko yanasema, tamaa ya pesa au kupenda sana pesa ndiyo shina la maovu yote.
Mwenye masikio na asikie.