Kiteitei
JF-Expert Member
- Jan 14, 2009
- 1,595
- 1,540
nimekuwa nikihudhuria maonesho na matamasha mengi ambayo yanahusisha muziki wa kizazi kipya (bongo flavor), kuna hii aina ya uimbaji ambayo karibuni kila muimbaji anaitumia na sijui kama ndio fasheni yenyewe, au ni kuiga ama ni majonjo tu au ni nini,NI hivi, waimbaji asilimia kubwa, kama sio wote wanapokuwa jukwaani wakiperform mkono mmoja unakuwa umeshika microphone na wa mwingine ( mara nyingi wa kulia) unang'ang'ania kwenye suruali kwa mbele., nisaidieni huwa kuna nini huko? (mic ya pili???)mwanzo nilidhani labda wanashikilia suruali zisidondoke hasa ukizingatia na style zao za uvaaji za kata k, au labda wanajikuna kidizaini lakini nadhani sivyo! binafsi naona kama inakera na inapoteza maadili, sijui mwenzangu...