MOSintel Inc
JF-Expert Member
- Mar 24, 2016
- 817
- 593
Wasalaam wana bodi,
Poleni sana na majukumu ya kulijenga Taifa.
Nchi yetu inaelekea katika uchaguzi mkuu na tayari mbiu imekwisha lia na amsha amsha za hapa na pale zimeanza.
Kuanzia tarehe 27 Agosti, 2020 hadi 28 Oktoba 2020 itakuwa kipindi cha mnyukano majukwaani kwa wagombea kutoka katika vyama vya siasa zaidi ya 10 katika nafasi ya Urais.
Katika kipindi hiki wanasiasa ambao wanaonyesha kuleta ushindani katika uchaguzi wa mwaka huu ni Mwanasheria nguli na mwanasiasa wa muda mrefu Ndugu Tundu Antipas Lissu kupitia CHADEMA na Rais anayemaliza kipindi cha utawala wake wa miaka mitano Ndugu. Dr. John Pombe Magufuli ambaye ameomba tena ridhaa kupitia chama chake cha CCM kuwa Rais kwa kipindi kingine.
Katika uchaguzi kura huwa katika makundi na wanasiasa makini katika kunyakua kura hizi za uchaguzi hurusha sera zao wakijikita katika makundi yafuatayo:
1. Vijana
2. Wakulima
3. Wafanyakazi
4. Wakina mama
5. Wafanyabiashara
Najua kampeni hazijaanza ila wagombea wengi walishaanza kutoa dodoso za nini watafanya. Wanasiasa walioingia ulingoni tumewajua.
Unadhani katika hao wawili niliowataja hapo juu ni mgombea yupi ambaye ana haiba ya kushawishi makundi hayo matano hasa ukizingatia mazingira ya KIUCHUMI(MICRO&MACRO), KISIASA na KIJAMII tuliyonayo kwa Sasa kuelekea uchaguzi?
#UCHAGUZI2020
#VISION2025
#AGENDA2063