Kuhusu Uchafu NAKATAA, labda uniambie tuu uchafu utaongeza kasi ya Uzalianaji n.k
Unakumbuka Skendo ya British Airline ya Mwaka 2017-2019? Kama hujui
google "BRITISH AIRLINE BED BUG"
Kuna abiria mmoja kutoka ghana alipanda na kunguni kwenye ndege kuelekewa Heathrow UK,
Kwanza walisambaa ndege nzima, kila seat, baada ya hapo kila anayepanda kwenye ile ndege akishuka anashuka nao,
Baada ya hapo wakajaa Pale airport, baada ya hapo wakajaa kwenye ndege nyingne, wakatoka hapo wakahamia Mtaani, london karibia yote na miji ya karibu ilichafuka ile, ni mwendo wa bites kwa kwenda mbele...
Kuna abiria mmoja kutoka CANADA alipanda ndege kuelekea SA kwa mapumziko, yule Mama alikula bites Zaidi ya 120, anatua cape town unajua rangi za wale wenzetu, uso km fenesi km si nanasi..
Sitanii hapa, just GOOGLE.
Haya niambie, Ndani ya ndege tena shirika km lile, kuna uchafu?
Wale wadudu Hawana mchezo, ukimbeba umekwisha..
Haijalishi umebeba
Wawili au Mmoja,
Jike au dume,
Alikua na mimba au hana,
Wao wanachojua ni kuzaa tuu, sijui mechanism yao ya reproduction ipoje.
Nawaelewa vzr sana, advance mpk walikua marafiki, Prepo unaenda huku umenuna, maana lazm uamke, ilikua ukiweza kulala Masaa matatu Non stop, we ni mwanaume. Na darasani nako lazma uende naye...na Mabweni na mazingira kwa ujumla yalikua masafi sana tuu, tatzo wale waliokua wanakuja na magodoro/blanket yao,
Kuanzia pale ikapgwa stop, vitu vyote unakuta shule.
Na wapo shapu kinyama, yaani Waweza uwe umembeba mmoja lkn ukahisi wapo mia,
Maana Aking'ata hapa, ndani ya sekunde ashahama venue. Mpk uje kumdaka Umejaa manundu,
Ile harufu yao nayo ni kero sanaa.
BTW nawashukuru sana ktk masomo, ile comb bila sapoti yso, ningezunguka round about/integrate zero.