Kunguni wanasababishwa na nini?

Kunguni wanasababishwa na nini?

Hakuna watu nawaonaga hawafikiri kama wanaosema kunguni wanasababishwa na uchafu...kunguni wanakaa hata kwenye vitanda vya Hilton Hotel sasa vitanda vya Hilton Hotel na chako cha geto chepi kisafi.

Sababu ya kunguni ni kuletwa na mtu aliyembebeba kutoka palipo na kunguni watazaliana mpaka watajaa...njia pekee yakuwaondosha ni sumu ya wadudu kama LAVA basi.

Kunguni anakaa sehemu chafu hao walio sehemu safi waliletwa na mtu mchafu aliyewabeba kutoka sahemu uchafu kwenye kiwanda cha kunguni.

Watu wengine ni wasafi tu huku nje huko wanakolala ni kuchafu hatari.
 
Come27, Hapo umeongea mkuu, kuna nyumba nimeishi yapata miaka mi5. Waliingia hawa wadudu walinisumbua sana. Ile nyumba haikuwa na uwezo wa kuingiza mwanga kwa namna ilivyokua imejengwa, yaani nilitumia madawa ya kila namna lakini hawakusikia dawa hadi nikahama ile nyumba yapata miezi 18 sasa.

Hii nyumba niliyohamia kwa sasa ina nafasi kubwa na madirisha mapana yanayoingiza mwanga wa jua kwa urahisi, nimeshangaa wale wadudu hawapo tena yani wamepotea mazima hakuna hata traces zao kuonyesha wanapatikana haya maeneo.

Note: kunguni sio uchafu tu hata maeneo yenye mrundikano wa vitu km nguo, Giza ambapo mwanga wa taa haufiki kiurahisi hawa wadudu ndo wanazaliana sana na wana asili ya kutosikia dawa hawafi na wanazaliana usiku na mchana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna watu nawaonaga hawafikiri kama wanaosema kunguni wanasababishwa na uchafu...kunguni wanakaa hata kwenye vitanda vya Hilton Hotel sasa vitanda vya Hilton Hotel na chako cha geto chepi kisafi.

Sababu ya kunguni ni kuletwa na mtu aliyembebeba kutoka palipo na kunguni watazaliana mpaka watajaa...njia pekee yakuwaondosha ni sumu ya wadudu kama LAVA basi.
Watu wanajiropokea tu uchafu kana kwamba huo uchafu ndio unabadilika na kua kunguni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Come27, Swali la msingi Ni wanatoka wapi?
Kunguni ni msafiri a Atoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kupitia binadamu na nguo zilizopo kwy mabegi yawasafiri.

Kunguni sehemu zenye rangi ya kijani au njano anakimbia anajua iyo rangi anaonekana kwa iyo hataama chumba au nyumba kwenda kwy nyumba iingine hawezi iishi sehemu yenye changamoto kwa sababu hawezi kuzaliana na sehemu ambayo inapitishwa usafi kwa kutumia sabuni izi za aerial, omo na kleasoft haimuui ila inamshmbua inabidi haame.

Kumbuka Kunguni hafi kwa dawa nyingi ila anaondoka kutokana na kero ya manukato. Kama ni mwanaume au mwanamke una kile kiarufu kama cha beberu Kunguni kuondoka ni shida labda ubadilishe mtindo wa maisha uwe msafi kiarufu kikisepa anakimbia

Research ya RANGE MANAGEMENT AND TSETSEFLY TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nimeishi mererani mji wenye joto la haja,ambalo ni sehemu ya mahitaji ya kunguni,baada kugundua kiumbe huyu yupo nilipiga dawa kisha nikawa mfatiliaji wa maeneo pendwa.ikafikia dogo wa chumba cha pili ambae kwake wapo kama mapambo ukutani,akiingia kwangu anaacha mbegu lkn inakua rahisi kujua kutokana na ukubwa wao.hakuna jambo lenye sababu moja tu,uchafu ni sehemu ya kustawisha wadudu waharibifu na wasumbufu.hivyo ni moja ya sababu.na inachangia sana ustawi wao.
 
Mimi Kuna mshikaji wangu kipindi nipo chuoni kaja kalala chumbani na mizigo yake akawaacha kunguni nilichofanya nilikuwa na godoro jipya la rangi ya kijani, wakawa wanajificha tuuu na nilikuwa napuliza airfresh kila jioni nawasha taaa{energy saver} usiku. Ndani ya mwezi walipotea wote maana walishindwa kuning'ata maana nilikuwa nalala nimewasha taaa nyeupe usiku mpaka asubuhi. Tatizo la kunguni kama mnaishi kwy chumba wawili na sehemu ya joto alafu mwenzako sio mtu wa kuoga na kufua nguo anazirundika ujue apo kunguni kuondoka atachukua muda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu Uchafu NAKATAA, labda uniambie tuu uchafu utaongeza kasi ya Uzalianaji n.k

Unakumbuka Skendo ya British Airline ya Mwaka 2017-2019? Kama hujui

google "BRITISH AIRLINE BED BUG"

Kuna abiria mmoja kutoka ghana alipanda na kunguni kwenye ndege kuelekewa Heathrow UK,
Kwanza walisambaa ndege nzima, kila seat, baada ya hapo kila anayepanda kwenye ile ndege akishuka anashuka nao,
Baada ya hapo wakajaa Pale airport, baada ya hapo wakajaa kwenye ndege nyingne, wakatoka hapo wakahamia Mtaani, london karibia yote na miji ya karibu ilichafuka ile, ni mwendo wa bites kwa kwenda mbele...

Kuna abiria mmoja kutoka CANADA alipanda ndege kuelekea SA kwa mapumziko, yule Mama alikula bites Zaidi ya 120, anatua cape town unajua rangi za wale wenzetu, uso km fenesi km si nanasi..
Sitanii hapa, just GOOGLE.
Screenshot_20200408-212050.jpg
Screenshot_20200408-212129.jpg

Haya niambie, Ndani ya ndege tena shirika km lile, kuna uchafu?

Wale wadudu Hawana mchezo, ukimbeba umekwisha..
Haijalishi umebeba
Wawili au Mmoja,
Jike au dume,
Alikua na mimba au hana,

Wao wanachojua ni kuzaa tuu, sijui mechanism yao ya reproduction ipoje.

Nawaelewa vzr sana, advance mpk walikua marafiki, Prepo unaenda huku umenuna, maana lazm uamke, ilikua ukiweza kulala Masaa matatu Non stop, we ni mwanaume. Na darasani nako lazma uende naye...na Mabweni na mazingira kwa ujumla yalikua masafi sana tuu, tatzo wale waliokua wanakuja na magodoro/blanket yao,

Kuanzia pale ikapgwa stop, vitu vyote unakuta shule.

Na wapo shapu kinyama, yaani Waweza uwe umembeba mmoja lkn ukahisi wapo mia,
Maana Aking'ata hapa, ndani ya sekunde ashahama venue. Mpk uje kumdaka Umejaa manundu,
Ile harufu yao nayo ni kero sanaa.

BTW nawashukuru sana ktk masomo, ile comb bila sapoti yso, ningezunguka round about/integrate zero.
 
anayesema hao wadudu wanastawi sehemu chafu.

asubiri siku kawaona ndani ya nyumba,asiue hata mmoja kisha aendelee na usafi wake wa kufua boxer na mashuka,kisha alete mrejesho.

kunguni akifika sehemu ili aishi sharti eneo hilo kuwe na msosi wa uhakika(damu ya kunyonya)anazaliana kwa wingi sana kama kuku wa nyama na uhakika wa chakula.

sasa braza,ukimuona gheto wacha dhana potofu kwamba huwenda viwango vya usafi vimeshuka,watakuandalia uchaguzi mkuu wakupe urais humo humo ndani kwako,piga dawa uwezavyo,mpaka waishe.acha mbwembwe za kufagia fagia kila saa.

aliye waleta anaweza kuwa mtu na heshima zake tu,nayeye kawabeba sehemu,ila wameishi naye mpaka muda huo sababu anayo damu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah. Sisi wengine tunawasikia tu.mara kunguni,chawa,papasi,kiroboto nk
 
Shimbuko lake ni uchafu pamoja na kutopiga pasi Nguo.Haina maana kila nyumba yenye kunguni ni wachafu,isipokua hao wadudu walisambazwa Na watu wachafu waliotoka vijijini.Inawezekana ni ndugu waliokutembelea,au ni wanafunzi walitoka nao shule,au uliwapata guest house au kwenye mabasi wakati wa kusafiri. Namna ya kuwaepuka hawa wadudu,ni kuhakikisha unapotoka safarini,Nguo ulizovaa kwenye gari au ulizolala nazo guest unazifua bila kuzichanganya na Nguo nyingine na kuzipiga pasi. Watoto wanaporudi shule wakati wa likizo,Nguo zifuliwe zipigwe pasi,kama amemaliza shule godoro asije nalo.Chumba cha wageni kijengwe nje ili iwe rahisi kukimonitor Mara kwa Mara pindi wageni wanapoondoka,usichanganye wageni na watoto wako chumba kimoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kunguni ni msafiri a Atoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kupitia binadamu na nguo zilizopo kwy mabegi yawasafiri.

Kunguni sehemu zenye rangi ya kijani au njano anakimbia anajua iyo rangi anaonekana kwa iyo hataama chumba au nyumba kwenda kwy nyumba iingine hawezi iishi sehemu yenye changamoto kwa sababu hawezi kuzaliana na sehemu ambayo inapitishwa usafi kwa kutumia sabuni izi za aerial, omo na kleasoft haimuui ila inamshmbua inabidi haame.

Kumbuka Kunguni hafi kwa dawa nyingi ila anaondoka kutokana na kero ya manukato. Kama ni mwanaume au mwanamke una kile kiarufu kama cha beberu Kunguni kuondoka ni shida labda ubadilishe mtindo wa maisha uwe msafi kiarufu kikisepa anakimbia

Research ya RANGE MANAGEMENT AND TSETSEFLY TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sabuni ya unga siyo kama haiuwi, eneo hilo haujatafiti.

Sabuni ya unga ni sumu inayomuua kunguni kwa sekunde.

Kavu ama iliyokorogwa na maji, ikimpata hapohapo anakauka na kuwa mapepe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kunguni wanaletwa nyumbani na baba su mama anaekwendaga gesti za bei rahisi. Mfano zile gesti za Mbagala selfu elfu tano, kawaida elfu tatu. Hapo hukosi kuchukua mbegu za kunguni
 
Back
Top Bottom