Kununua bando kwa sasa ni hasara iliyowazi

Kununua bando kwa sasa ni hasara iliyowazi


Hata mimi nililiona serikali haijali kabisa swala hili kila siku vifurushi vinapanda bei tu..
 
Kukuongezea kitu, ukitaka kutumia insta tumia web version na si application maana web version huwa haifungui medias za page nzima kama app kitu ambacho kinafanya data isiende kubwa.
Well noted!
 
Hapa mitandao ya simu tunaionea tatizo linaanzia serikalini

Ikiongeza kodi kwa makampuni lazima kampuni nazo zipandishe gharama za vifurushi ili kutopata hasara

Hii ni biashara hata kama ni wewe huwezi kuwa unatengeneza hasara tu daily
Umeongea jambo la msingi sana serikali ikipandishia izo kampuni gharama za uendeshaji maana yake iyo cost italipwa indirectly na mteja
 
Kununua bundle ni anasa na , bia zimepanda bei. Hapa unafanya opportunity Cost ufanye anasa ipi weekend ya leo

Kwanini tusianzishe mgomo kwa miezi miwili hivi wakutumia bando sio chakula hichi wadau mnaonaje bado vyanzo vya kupata habari vipo watumiaji mil 1 wanaonunua bando la elfu 30 kwa mwezi wakigoma kununua kutokuwa na loss ya bill 30
Naanza mgomo rasmi leo. Muda wa kuingia mtandaoni nitautumia kufanya meditation na kusoma vitabu
 
Nilifuta Instagram
Twita
Na app nyingine nyingi tu
Now Samsung J5 prime yangu data natumia kwenye JF na WhatsApp tu na kidogo opera min natumia Gb kwa siku 7

●Jamaa wa ikulu siwezi kukusahau kwa ulichonifanyia
 
 
Haya ni matumizi ya mtu binafsi. Kuna mtu anatamani apate hata laki 6 afanye biashara lkn kuna mtu hiyo hela ananywea bia.
Ni hela yake na ni matumizi yake
Sasa kwanini ulalamike na bei za mbs, wakati huna uwezo
 
Back
Top Bottom