Kununua gari toka Japan kwa kuangalia low milleage ni wrong.

Maelezo yako siyo kweli ukinunua gari ukakuta ina km mfano 150000 na nyingine 75000 elewa hiyo ya 150000 imetumika sana kuliko hiyo nyingine na kuzima na kuwasha gari maranyingi sana hakuathiri engine kinachoathirika ni starter ndani kuna carbon brushes starter coil na bendex hivyo ndivyo vinachoka mapema na ukibadili starter complete uwakaji unakuwa mzuri
 

Pole mkuu. Next time kuwa makini unapoagiza gari. Usisubiri uchekwe na wenzio halafu ndipo utuletee elimu ya High Mileage. Ndiyo la kwako tayari, huna namna zaidi ya kulitetea.

Yaani hapa unajaribu kutuambia bora kuoa mwanamke mzee kuliko kijana na wewe ni kijana.
 
Mr. MTUI leo umechemka, japo kunauwezekano low mileage vehicle ikawa mbovu kuliko yenye mileage nyingi kutokana na matumizi. Lakini kwa nchi kama Japan, vehicle repair history itakupa ukweli wote.

It is a high time, serikali iweke vehicle repair history kuwa mandatory wakati wa kununua gari kutoka nje ya nchi. Mtu akikuuzia gari na akakupa wrong vehicle history basi LEMON LAW inamhusu.
 
Elewa hili,starter inapokufa kwa kuwasha na kuzima hiyo gari lazima nayo iwe pia imeshachoka,huwezi kuta gari ina mileage ya 3km imekufa starter kisa imewashwa na kuzimwa mara nyingi...
mkuu kuwasha na kuzima gari mara kwa mara kunaweza sababisha gari yako kuchoka..starter huwa zinaharibika.. Vyuma vinasagika iwapo utaliondoa gari bika kusubiri stabikization
 
Nilicho ona kwa mwandishi maelezo yake yote anaongelea stater??
Nina wasiwasi amesikia story kijiweni akaziamini bila kuzifanyia utafiti.
Wakati flani nilibahatika kuongea na Specialist wa Land cruiser hardtop (Zile Gari imara sana zinazo tumika hasa kwa barabara za vumbi)
Alinifahamisha kuwa; zile gari zikifikisha kms250,000 hushauriwa zifunguliwe Engine (Over-whole) au Pengine baada ya hapo kwa mashirika yenye hela, huziuza kwani huweza kuanza matatizo ya kusumbua Engine.
Mtu angeniuliza ningemwambia KMS chache ni nzuri sana hasa gari isiwe ya zamani sana. Pamoja na kuwa kms chache au Nyingi pia hutegemea mtumiaji alikuwa akifanyia gari lake service kwa wakati
Kuna scinerio moja au mbili ambalo mtoa mada angeongelea ila sio suala la ujumla kuwa kms nyingi ni bora...hiyo sio sawa!!!!
 
Gari hutegemea service kama mtumiaji alikuwa hafanyi service kwa muda hizo kilometer hazita saidia
 
Sababi zote ulizoziandika hazina maana!very sorry.
 
Labda hoja iwe kua gari yenye KM nyingi inakua imefanyiwa ukarabati kwa vile Japan hubadilisha vipuri kulingana na mailage
 
1. Kuendeshwa mjini hakuna uhusiano na high mileage. Taxi na daladala ziko mjini zina high mileage kuliko mabasi ya mkoa.
2.Kuwasha na kuzima kunahitaji UFAHAMU kama ulivyosema na sio kuendeshwa mjini au kijijini.
3.Vilainishi kufika kila sehemu kunategemea na quality ya vialinishi na kuzingatia matakwa ya gari husika haihusiani na kuendeshwa highway au mjini
4.Ajali popote tena ajali za highway ni do or die
5.Kugongesha gari au kutomugongesha ni skills za mtu binafsi sio kuwa mjini au kijijini.

Maoni yangu:
Parts nyingi za gari zina life span mara nyingi ni km 100,000 baada ya hapo zinaanza kuchoka hivyo kuhitaji kubadilishwa. Ukinunua gari zaidi au karibia 100,000km mzigo wa kubadili unakuangukia wewe.
Unaweza kununua high mileage vehicle kama utapata genuine service history yake itakuonesha vitu vilivyobadilishwa mfano timing belt etc.

Unaweza kununua low mileage kumbe imechezewa ina miles 150,000 utaingia mkenge.
 
Kwaio gari yenye High Mileage ndo haiwezi kua na matatizo hayi uliyoyasema?
 
Scratching ni hoja dhaifu mno.

Iwe unakaa Upanga au Mlandizi, gari linalowashwa mara nyingi ndo lipo active kuliko linalowashwa mara moja kwa wiki.
 
mkuu kuwasha na kuzima gari mara kwa mara kunaweza sababisha gari yako kuchoka..starter huwa zinaharibika.. Vyuma vinasagika iwapo utaliondoa gari bika kusubiri stabikization
Starter hazijaharibika kwenye magari yetu huku mitaani ambayo yana mileage 3.000.000 km.
 
Mkuu yard yako gari hazitoki, huenda ulishauriwa hvo na wataalamu wako.

Umeongea porojo tu
 
Mileage ndogo ndio kila kitu kwangu. Na gari mpya nayo itakuwa aje?
Mpaka hapo ulipoishia, sijaona hata sababu moja yenye mashiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…