Kununua gari toka Zanzibar

Kununua gari toka Zanzibar

Mwenye gari na wenye magari, ila mleta uzi ametaka tuu kujua gharama atakazo chajiwa na TRA zina weza kuwa kiasi gani? hayo mengine kwamba x-trail ipo hivi mara vile itakuwa mwenyewe alishafanya utafiti na ndio maana anataka kununua.
 
Kuna jamaa yangu yuko Zanzibar anataka kuniuzia gari. Na gari nikiangalia iko vizuri tu. Xtrail ya 2005 ananipa kwa mil 6. Ila sasa nasikia kuleta gari Bara toka Zanzibar unalipia tena ushuru. Je hiyo ni kweli?. Na kama ni kweli, kwa gari kama hiyo yaweza garimu kiasi gani mpaka naiendesha huku Tz Bara. Anayejua au aliyewahi kununua gari toka Zanzibar naomba ushauri.
Nilinunua gari Zanzibar na nilichofanya nilienda na Document TRA ya Zanzibar kujua kiasi ambacho kililipiwa wakati inaingia Gari hiyo Zanzibar ,baada ya hapo nakaenda TRA ya Bongo wakatipa Amount kamili na tofauti yake ilikuwa million moja tu ambayo nilipaswa kulipia, maana Zanzibar kodi yao IPO chini ukilinganisha na TZ bara.

Ikawa hivi sasa:
Ongezeko la kodi 1,000,000
Kusafirisha gari 300,000 - 350 ,000
Clearence 500,000 inategemea na Agent

Gari ikawa mkononi ila sijui kwa sasa mambo yakoje zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utalazimika kulipia 'The difference'. Yani kama gari iliingia Zbar wakalipa import Duty na VAT wewe utalazimika kulipia 25% ya Uchakavu. So hapo uandae kama M2-3.
pia kupakia gari kwenye meli ni kama laki tano. Agent fee kama laki mbili.
Mpaka hiyo gari unaiingiza bara barani itakuwa imekukamua kama M9-10.
Niliwahi kuingiza gari toka Zbar mwak 2008.
 
Nilinunua gari Zanzibar na nilichofanya nilienda na Document TRA ya Zanzibar kujua kiasi ambacho kililipiwa wakati inaingia Gari hiyo Zanzibar ,baada ya hapo nakaenda TRA ya Bongo wakatipa Amount kamili na tofauti yake ilikuwa million moja tu ambayo nilipaswa kulipia, maana Zanzibar kodi yao IPO chini ukilinganisha na TZ bara.

Ikawa hivi sasa:
Ongezeko la kodi 1,000,000
Kusafirisha gari 300,000 - 350 ,000
Clearence 500,000 inategemea na Agent

Gari ikawa mkononi ila sijui kwa sasa mambo yakoje zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app

Ilikuwa mwaka gani mkuu?
 
Nakumbuka mwaka Jana kuna rafiki yangu alinunua gari Zanzibar kwa 7m alipolileta bara kodi ilikua 4m,
Sikumbuki aina ya gari maana Mimi najua magari ninayoyapenda i.e Spacio, Prado n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikushauri tu, nenda mwenywe Zanzibar kabla ya kununua hilo Gari nauri ni 50,000 go and return kafanye Analysis ya kutosha zaidi sana cha kuangalia ni
1.Tofauti ya Ushuru wa TRA
2.Transport
3.Na clearence Agent ijapo hii ni mapatano tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana mkuu. Nimesoma post zako na nimepata mwanga wa kutosha tu. Shukurani kwa muda wako mkuu.
 
Shukrani sana mkuu
Mkuu naona kama uko interested na hiyo issue. Kuna maelezo nimeyapata nje ya JF. Ukishanunu hiyo gari kabla hujasafirisha, hakikisha umefanya mpango wa plate number na umeipata. Safirisha gari ikiwa tayari na number za Bara, ikifika unaichukua. Lakini ikifika then isubiri process ya number, kuna majanga ya kuchomolewa vitu kwenye gari. Nimekutana na hiyo news wati nadodosa.
 
Mimi nina mtu anahiyo Gari, Kuna kipindi Nilitaka kununua kama hiyo, huyo huyo mtu akaniambia nisinunue kwani siyo Gari ni matakataka

Sent using Jamii Forums mobile app
Alikupa sababu gani? Ulimuuliza sababu? Sijaona sababu ya msingi ya kusema hivyo wakati kilasiku zinaingia, zinauzwa na watu wanatembea nazo kila siku. Pili kuhusu spare zake sidhani kama wanaosema ni expensive wapo wapo sawa, maana mie nanunua spare pale Ilala kwa bei ya kawaida tu. People have created a phobia to the unknown!!!
 
Watanzani wengi tunapenda vitu feki na ndiyo shida yetu. Ukiwauliza hata hawajui kuwa Toyota nazo zina spea original ambazo bei yake ipo juu pia. Hata ukifuatilia wenye Magari wengi wanachakaza Magari yao kwenye gereji za uchochoroni. Amini nawambieni gereji za watu wanaojitambua hawezi kukubari kufungi spea feki kwani itamuharibia jina lake kibiashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naona kama uko interested na hiyo issue. Kuna maelezo nimeyapata nje ya JF. Ukishanunu hiyo gari kabla hujasafirisha, hakikisha umefanya mpango wa plate number na umeipata. Safirisha gari ikiwa tayari na number za Bara, ikifika unaichukua. Lakini ikifika then isubiri process ya number, kuna majanga ya kuchomolewa vitu kwenye gari. Nimekutana na hiyo news wati nadodosa.

Thanks sana mkuu kwa info ya kiinteligensia.

Nachukua wazo lako kwa mikono yote mkuu.
 
Back
Top Bottom