Kununua gari toka Zanzibar

Kununua gari toka Zanzibar

Kuna post nyingi zimeongelea mambo hasi juu ya hizi gari Nissan Xtrail. Na kuna post chache zimeongelea mambo chanya juu ya hizo gari. Mawazo hasi juu ya Xtrail hayana uhalisia wowote. Ni ‘phobia’ tu kama alivyosema mdau mmoja hapo juu. Mimi naongezea ‘ignorance’ pia inachangia sana. Unaposema Xtrail ni gari ya kipato cha juu, mimi mswahili naelewa kwa maana nyingine Xtrail ni gari ya kifahari. Really!!!!!!?, Xtrail ni gari ya kifahari, hebu tuache utani. Gari za kitajiri zinaendana na muonekano, features, technology nakadhalika. Hata Nissan wenyewe wakisikia gari yao mnaiweka kwenye kundi la gari za kifahari watatushangaa sana watanzania. Xtrail haina gharama za uendeshaji kiasi mtanzania wa kipato cha kawaida aziogope, hazipo hizo gharama. Ni za kutengeneza tu. Sitaongelea sana juu ya issue ya gharama za spare na upatikanaji wake, sababu kuna post mbili tatu hapo juu zinatoa ushuhuda halisi, si wa kuambiwa kama wengi tunavyoongea. Watoa ushuhud wana ‘hands-on experience’. Yawezekana gharama zilikuwa mwanzoni na ni kwasababu za kibiashara tu. Kwamba gari zilikuwa chache, hakuna muuzaji anayeleta spare. Hata akileta zinakaa sana kwenye shelf. Hapo kipuri ukikikuta lazima bei itakuwa juu tu. Hivi sasa gari ni nyingi na uhitaji wa spare uko juu na wauzaji spare wanataka kufanya biashara. Hapo sijataka kuongelea Udarisalama mjini, mtu unapigwa jinsi ulivyoenda, Plus vishoka wanaosimama pembeni ya maduka ya spare. Yaani swala la gharama za spare ni mtambuka sana. Hasa kwa mji wenye chocho nyingi kama DSM. Inategemea umemtuma nani, fundi ama kijana wako. Ukienda mwenyewe, inategemea umeenda maeneo gani. Umekamatwa na kishoka au la, ukifika dukani pia inategemea siku hiyo umemkuta nani, mwenye duka au kijana aliyeajiriwa (kila mmoja ana bei zake hapo). Yaani ni shida. Hivyo kuja tu juu juu na kusema vipuri vya Xtrail bei iko juu, hapana.

TUBADILIKE
Kuna watu wanasema Xtrail ni plastiki. Hivi sasa kwenye ulimwengu unaojali usalama wa maisha ya watu, dunia nzima inaelekea kwenye gari za maplastiki. Labda wewe tu, utaishia kutembea kwa miguu kama hutaki kuendesha plastiki. Usalama wa maisha ya mtumiaji wa chombo cha moto ni muhimu sana. Hata kama technolojia ni convenient kiasi gani, mwisho wa siku swali…….je ni salama kiasi gani kwa mtumiaji?. Kama si salama, tia kapuni. Nitoe mfano wa jinsi muendelezo wa usalama kwenye vyombo vya moto unavyoenda. Mwanzoni vioo vya magari vilikuwa ni vihatarishi. Kwenye msukosuko kidogo vioo hupasuka na kuancha ncha kali zinazowatumbua watu na kusababisha vifo na majeruhi wasio wa lazima. Gari zikaja na vioo vya kumwagika au visivyosambaratika. Kioo vikipata crack kidogo, kinamwagika chote na kuwa chenga ndogo ndogo. Au vioo vya magari vyenye nailoni gumu katikati, hata kikivunjika hakipati nafasi ya kuacha ncha zitakazoleta madhara. Hiyo yote ni kwaajili ya usalama wakati wa misuko suko. Sasa watanzania kama kawaida…….’’hizi gari siyo kabisa, ukigusa tu kioo kinamwagika’’.
Turudi kwenye maplastiki. Nimeshashuhudia ajali, gari ilikuwa nyang’anyang’a. Hakuna cha kuokota zaidi ya frame. Lakini hakuna vifo wala majeruhi serious. Tena nakumbuka lilikuwa bus lenye abiria wengi tu. Na kuna ajali unakuta ilikuwa impact ndogo tu, hata gari yenyewe unakuta labda roof imebonyea kidogo tu. Lakini ukiuliza unaambiwa hajatoka mtu. Watu tunashangaa!!!….Mungu mkubwa. Baadhi ya nchi zenye akili nyingi wanapiga marufuku gari za mabati, au kutafuta njia fulani ya kuzipunguza barabarani kwa kupitia kodi, nk. Au ku-encourage manufacturers waachane na mabati.
Sasa nyie bakini na mabati yenu, eti kisa unaweza kwenda kulichomelea na kupiga puti. Maplastiki (kama mnavyoita) yana-absorb mpaka impact ya gari kwenye ajali, air bag inakudaka, unatoka salama na leo uko hapa Jf unaongea. Sikubali mwanafamilia wangu abanwe na bati mpaka kupelekea akakatwe mguu. Halafu niendelee kuendekeza mabati kisa naweza kwenda kupiga puti!!!!. kHapana, kwa kipato changu hichihichi familia yangu itatembea kwenye maplastiki. Wakijichanganya kwenye usafiri wa umma hiyo ni sawa. Lakini siyo nitoe milioni kumi zangu, niwaweke kwenye hatari. Pesa inatafutwa na kupatikana. Lakini siyo roho au kiungo cha mwili. Hivi sasa usalama unapigiwa upatu katika nyanja zote kabisa. Kwanza usalama wa watu walio nje na ndani ya chombo, pili usalama wa mazingira, tatu ndo usalama wa chombo chenyewe. Watanania tubadili mtazamo.

XTRAIL GARI MBOVU.
Kwanza kabisa kuna ombwe kubwa sana kwenye tasnia ya ufundi wa vyombo vya moto. Ufundi mwingi sana sana wa vyombo vya moto hapa kwetu, ni ufundi wa ‘kurithi’ kivitendo. Kijana anapelekwa akasaidie kazi karakana ya magari. Mwaka wa kwanza, wa pili, na yeye ni fundi. Wapo mafundi wachache kutoka VETA ambao nao ukiwachimba, hawakidhi haja au hali halisi ya mahitaji. Hao wa VETA tatizo si wao, ni mfumo wa elimu yetu katika nyanja zote,si ya ufundi mitambo pekee. Na hata hao mafundi mitambo wa vyuo vya juu, wenye ‘potential’ ya kwenda na hali halisi. Hawataki kazi za kuhudumia vyombo vya moto.
Kwa mtindo huo gari za aina ya Xtrail lazima ziwe ni tatizo kwenye ufundi. Kwanza gari hizo zina mfumo wa kikompyuta unaoweza kutoa taarifa za gari lote. Hapa inabidi fundi awe na kifaa maalum cha kuweza kuutumia huo mfumo na kupata taarifa za gari. Pia uwezo wa kusoma taarifa atakayoletewa, na muhimu zaidi awe na uwezo wa kusoma mchoro (ramani ya gari) ili afahamu location ya tatizo. Yaani ni moja kwa moja kwenye point. Hakuna mambo ya kukisia, kujaribu-jaribu wala kupoteza muda. Hapa sasa ndipo mafundi wetu wengi wanapowekwa benchi na gari zenye mifumo ya aina hiyo. Na habari mbaya zaidi, gari zote zinaelekea hukohuko. ‘Guess work’ ni hatari sana kwenye tasnia ya ufundi mitambo. Ni hatari hasa kwa chombo chenyewe. Mara nyingi huongeza matatizo kwenye chombo. Na kibaya Zaidi wasichokipenda wenye akili ni ‘upotevu wa muda’. Kwenye tasnia nyingine mathalani ya umeme, kukisia ni hatari mpaka kwa mkisiaji mwenyewe. Mfumo wa mitambo kutoa taarifa zake wenyewe, umekuja kufuta kabisa ‘guess work’. ‘Guess work’ ndiko uliko utaalamu wa mafundi wetu wengi kama sio wote. Kazi kwa mtindo wa kukisia kwenye magari aina ya Xtrail, itakusumbua sana. Na aghalabu sana hakuna mafanikio na upotevu wa muda. Mwisho wa siku gari za aina ya Xtrail zinaangushiwa jumba bovu. Kwa ukosefu wa vifaa na ujuzi wa baadhi ya mafundi wetu wengi
.
Mfano hai!.
Kuna rafiki yangu nafanya naye kazi na anamiliki Nissan Xtrail. Wakati anainunua alivunjwa moyo sana na wadau. Lakini kwavile na yeye ni mtaalamu wa mitambo, hakuogopa japo aliingiwa na wasiwasi. Baada ya kuinunua, akakaa nayo muda tu ikiwa vizuri. Mara siku moja isiyo na jina gari haiwaki. Huku na huku….gari imegoma. Yaani hata ku-respond labda useme battery iko down au starter, au plug, sijui nini. Gari iko kimya kama haimjui vile. Akaona enhe….ya wahenga yametimia, asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Kwanza akatumia utundu wake wote, akashindwa. Kumbuka na yeye ni msomi wa mitambo na ana uzoefu na kanuni za mitambo. Kutokana na uelewa wa jamaa yangu, hakutaka kuipelega gari kwa fundi wa ‘kurithi’. Katika hangaika yake akakutana na fundi mwenye D-Deck au scanner, ambacho ni kifaa cha kusoma taarifa za gari. Akamuita home kwake, jamaa akaja na kifaa chake kwenye mkoba. Swali la kwanza aliloulizwa na fundi, ‘’je kuna fundi yeyote alishawahi kulifungu gari lako?’’. Jamaa akajibu hapana. Na ni kweli hakuna fundi aliwahi fungua mahali, zaidi ya service za kawaida za gari. Basi, fundi akafungua gari kuchomeka kifaa ili kupata taarifa. Na wakati anafungua, akamwambia jamaa yangu kwamba ni kweli hii gari inaonekana haijaguswa. Akachomeka, akawasha kifaa na kikamuonyesha ‘Camshaft sensor’ imekufa. Akasema dah! Sasa naipata wapi hiyo ‘sensor’. Akaona ya wahenga yanazidi kutimia. Ilikuwa ni Mwanza, akaelekezwa duka flani, akafika. Bei ni laki mbili na nusu. Akaona ya wahenga yanazidi tu kutimia. Basi akaingia kwenye maelewano ya bei, na mwisho wa siku akauziwa kipuri kwa shilingi laki moja. Akampelekea fundi, fundi akafunga ile ‘sensor’. Kuwasha gari, ni mara moja tu. Akamlipa yule fundi elfu hamsini kama sijasahau. Na gari anapiga nayo masafa mpaka kesho kutwa.
Sasa kwa case hiyo, hapo mtasema nini wadau?. Kweli gari za aina ya Xtrail zina shida!!!!?. Kwenye hiyo case unapata picha ya ufundi na picha ya bei pia. Na hiyo case ni Mwanza mjini. DSM mjini nadhani hiyo spare angepata chini ya hapo, I guess (ila fundi usi-guess).
Kama unapenda Xtrail and the likes, nunua wala usiogope. Kiafya si vizuri kukandamiza nafsi pasipo sababu za msinigi. Humuhumu JF kuna wamiliki wengi tu wa hizo gari na wana taarifa chanya nyingi tu kuhusu Nissan Xtrail. Dunia hivi sasa ni kijiji. Taarifa zote zipo kiganjani mwako, labda uwe mvivu tu. Information ni power. Watu wa Xtrail mnaanzisha kijiwe chenu humu ndani, mnaonyeshana machaka ya maduka ya vipuri, chocho za mafundi wa ukweli then hii ‘phobia’ inazikwa rasmi na Xtrail zinandelea kuwa Xtrail.
 
Kuna post nyingi zimeongelea mambo hasi juu ya hizi gari Nissan Xtrail. Watu wa Xtrail mnaanzisha kijiwe chenu humu ndani, mnaonyeshana machaka ya maduka ya vipuri, chocho za mafundi wa ukweli then hii ‘phobia’ inazikwa rasmi na Xtrail zinandelea kuwa Xtrail.
Mkuu umefunga Mada au ni Mada ingine Jukwaa la Magari?
mwanzo umetaka kununua gari Zanzibar na uivushe tukupe ushauri
Gari yenyewe Nissan Xtrail
Kuna jamaa yangu yuko Zanzibar anataka kuniuzia gari. Na gari nikiangalia iko vizuri tu. Xtrail ya 2005 ananipa kwa mil 6. Ila sasa nasikia kuleta gari Bara toka Zanzibar unalipia tena ushuru. Je hiyo ni kweli?. Na kama ni kweli, kwa gari kama hiyo yaweza garimu kiasi gani mpaka naiendesha huku Tz Bara. Anayejua au aliyewahi kununua gari toka Zanzibar naomba ushauri.
Gari hiyo haina tofauti na Mitsubishi RVR
ha ya Link ta TRA hiyo hapo Country jaza Zanzibar
Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System
 
Kuna post nyingi zimeongelea mambo hasi juu ya hizi gari Nissan Xtrail. Na kuna post chache zimeongelea mambo chanya juu ya hizo gari. Mawazo hasi juu ya Xtrail hayana uhalisia wowote. Ni ‘phobia’ tu kama alivyosema mdau mmoja hapo juu. Mimi naongezea ‘ignorance’ pia inachangia sana. Unaposema Xtrail ni gari ya kipato cha juu, mimi mswahili naelewa kwa maana nyingine Xtrail ni gari ya kifahari. Really!!!!!!?, Xtrail ni gari ya kifahari, hebu tuache utani. Gari za kitajiri zinaendana na muonekano, features, technology nakadhalika. Hata Nissan wenyewe wakisikia gari yao mnaiweka kwenye kundi la gari za kifahari watatushangaa sana watanzania. Xtrail haina gharama za uendeshaji kiasi mtanzania wa kipato cha kawaida aziogope, hazipo hizo gharama. Ni za kutengeneza tu. Sitaongelea sana juu ya issue ya gharama za spare na upatikanaji wake, sababu kuna post mbili tatu hapo juu zinatoa ushuhuda halisi, si wa kuambiwa kama wengi tunavyoongea. Watoa ushuhud wana ‘hands-on experience’. Yawezekana gharama zilikuwa mwanzoni na ni kwasababu za kibiashara tu. Kwamba gari zilikuwa chache, hakuna muuzaji anayeleta spare. Hata akileta zinakaa sana kwenye shelf. Hapo kipuri ukikikuta lazima bei itakuwa juu tu. Hivi sasa gari ni nyingi na uhitaji wa spare uko juu na wauzaji spare wanataka kufanya biashara. Hapo sijataka kuongelea Udarisalama mjini, mtu unapigwa jinsi ulivyoenda, Plus vishoka wanaosimama pembeni ya maduka ya spare. Yaani swala la gharama za spare ni mtambuka sana. Hasa kwa mji wenye chocho nyingi kama DSM. Inategemea umemtuma nani, fundi ama kijana wako. Ukienda mwenyewe, inategemea umeenda maeneo gani. Umekamatwa na kishoka au la, ukifika dukani pia inategemea siku hiyo umemkuta nani, mwenye duka au kijana aliyeajiriwa (kila mmoja ana bei zake hapo). Yaani ni shida. Hivyo kuja tu juu juu na kusema vipuri vya Xtrail bei iko juu, hapana.

TUBADILIKE
Kuna watu wanasema Xtrail ni plastiki. Hivi sasa kwenye ulimwengu unaojali usalama wa maisha ya watu, dunia nzima inaelekea kwenye gari za maplastiki. Labda wewe tu, utaishia kutembea kwa miguu kama hutaki kuendesha plastiki. Usalama wa maisha ya mtumiaji wa chombo cha moto ni muhimu sana. Hata kama technolojia ni convenient kiasi gani, mwisho wa siku swali…….je ni salama kiasi gani kwa mtumiaji?. Kama si salama, tia kapuni. Nitoe mfano wa jinsi muendelezo wa usalama kwenye vyombo vya moto unavyoenda. Mwanzoni vioo vya magari vilikuwa ni vihatarishi. Kwenye msukosuko kidogo vioo hupasuka na kuancha ncha kali zinazowatumbua watu na kusababisha vifo na majeruhi wasio wa lazima. Gari zikaja na vioo vya kumwagika au visivyosambaratika. Kioo vikipata crack kidogo, kinamwagika chote na kuwa chenga ndogo ndogo. Au vioo vya magari vyenye nailoni gumu katikati, hata kikivunjika hakipati nafasi ya kuacha ncha zitakazoleta madhara. Hiyo yote ni kwaajili ya usalama wakati wa misuko suko. Sasa watanzania kama kawaida…….’’hizi gari siyo kabisa, ukigusa tu kioo kinamwagika’’.
Turudi kwenye maplastiki. Nimeshashuhudia ajali, gari ilikuwa nyang’anyang’a. Hakuna cha kuokota zaidi ya frame. Lakini hakuna vifo wala majeruhi serious. Tena nakumbuka lilikuwa bus lenye abiria wengi tu. Na kuna ajali unakuta ilikuwa impact ndogo tu, hata gari yenyewe unakuta labda roof imebonyea kidogo tu. Lakini ukiuliza unaambiwa hajatoka mtu. Watu tunashangaa!!!….Mungu mkubwa. Baadhi ya nchi zenye akili nyingi wanapiga marufuku gari za mabati, au kutafuta njia fulani ya kuzipunguza barabarani kwa kupitia kodi, nk. Au ku-encourage manufacturers waachane na mabati.
Sasa nyie bakini na mabati yenu, eti kisa unaweza kwenda kulichomelea na kupiga puti. Maplastiki (kama mnavyoita) yana-absorb mpaka impact ya gari kwenye ajali, air bag inakudaka, unatoka salama na leo uko hapa Jf unaongea. Sikubali mwanafamilia wangu abanwe na bati mpaka kupelekea akakatwe mguu. Halafu niendelee kuendekeza mabati kisa naweza kwenda kupiga puti!!!!. kHapana, kwa kipato changu hichihichi familia yangu itatembea kwenye maplastiki. Wakijichanganya kwenye usafiri wa umma hiyo ni sawa. Lakini siyo nitoe milioni kumi zangu, niwaweke kwenye hatari. Pesa inatafutwa na kupatikana. Lakini siyo roho au kiungo cha mwili. Hivi sasa usalama unapigiwa upatu katika nyanja zote kabisa. Kwanza usalama wa watu walio nje na ndani ya chombo, pili usalama wa mazingira, tatu ndo usalama wa chombo chenyewe. Watanania tubadili mtazamo.

XTRAIL GARI MBOVU.
Kwanza kabisa kuna ombwe kubwa sana kwenye tasnia ya ufundi wa vyombo vya moto. Ufundi mwingi sana sana wa vyombo vya moto hapa kwetu, ni ufundi wa ‘kurithi’ kivitendo. Kijana anapelekwa akasaidie kazi karakana ya magari. Mwaka wa kwanza, wa pili, na yeye ni fundi. Wapo mafundi wachache kutoka VETA ambao nao ukiwachimba, hawakidhi haja au hali halisi ya mahitaji. Hao wa VETA tatizo si wao, ni mfumo wa elimu yetu katika nyanja zote,si ya ufundi mitambo pekee. Na hata hao mafundi mitambo wa vyuo vya juu, wenye ‘potential’ ya kwenda na hali halisi. Hawataki kazi za kuhudumia vyombo vya moto.
Kwa mtindo huo gari za aina ya Xtrail lazima ziwe ni tatizo kwenye ufundi. Kwanza gari hizo zina mfumo wa kikompyuta unaoweza kutoa taarifa za gari lote. Hapa inabidi fundi awe na kifaa maalum cha kuweza kuutumia huo mfumo na kupata taarifa za gari. Pia uwezo wa kusoma taarifa atakayoletewa, na muhimu zaidi awe na uwezo wa kusoma mchoro (ramani ya gari) ili afahamu location ya tatizo. Yaani ni moja kwa moja kwenye point. Hakuna mambo ya kukisia, kujaribu-jaribu wala kupoteza muda. Hapa sasa ndipo mafundi wetu wengi wanapowekwa benchi na gari zenye mifumo ya aina hiyo. Na habari mbaya zaidi, gari zote zinaelekea hukohuko. ‘Guess work’ ni hatari sana kwenye tasnia ya ufundi mitambo. Ni hatari hasa kwa chombo chenyewe. Mara nyingi huongeza matatizo kwenye chombo. Na kibaya Zaidi wasichokipenda wenye akili ni ‘upotevu wa muda’. Kwenye tasnia nyingine mathalani ya umeme, kukisia ni hatari mpaka kwa mkisiaji mwenyewe. Mfumo wa mitambo kutoa taarifa zake wenyewe, umekuja kufuta kabisa ‘guess work’. ‘Guess work’ ndiko uliko utaalamu wa mafundi wetu wengi kama sio wote. Kazi kwa mtindo wa kukisia kwenye magari aina ya Xtrail, itakusumbua sana. Na aghalabu sana hakuna mafanikio na upotevu wa muda. Mwisho wa siku gari za aina ya Xtrail zinaangushiwa jumba bovu. Kwa ukosefu wa vifaa na ujuzi wa baadhi ya mafundi wetu wengi
.
Mfano hai!.
Kuna rafiki yangu nafanya naye kazi na anamiliki Nissan Xtrail. Wakati anainunua alivunjwa moyo sana na wadau. Lakini kwavile na yeye ni mtaalamu wa mitambo, hakuogopa japo aliingiwa na wasiwasi. Baada ya kuinunua, akakaa nayo muda tu ikiwa vizuri. Mara siku moja isiyo na jina gari haiwaki. Huku na huku….gari imegoma. Yaani hata ku-respond labda useme battery iko down au starter, au plug, sijui nini. Gari iko kimya kama haimjui vile. Akaona enhe….ya wahenga yametimia, asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Kwanza akatumia utundu wake wote, akashindwa. Kumbuka na yeye ni msomi wa mitambo na ana uzoefu na kanuni za mitambo. Kutokana na uelewa wa jamaa yangu, hakutaka kuipelega gari kwa fundi wa ‘kurithi’. Katika hangaika yake akakutana na fundi mwenye D-Deck au scanner, ambacho ni kifaa cha kusoma taarifa za gari. Akamuita home kwake, jamaa akaja na kifaa chake kwenye mkoba. Swali la kwanza aliloulizwa na fundi, ‘’je kuna fundi yeyote alishawahi kulifungu gari lako?’’. Jamaa akajibu hapana. Na ni kweli hakuna fundi aliwahi fungua mahali, zaidi ya service za kawaida za gari. Basi, fundi akafungua gari kuchomeka kifaa ili kupata taarifa. Na wakati anafungua, akamwambia jamaa yangu kwamba ni kweli hii gari inaonekana haijaguswa. Akachomeka, akawasha kifaa na kikamuonyesha ‘Camshaft sensor’ imekufa. Akasema dah! Sasa naipata wapi hiyo ‘sensor’. Akaona ya wahenga yanazidi kutimia. Ilikuwa ni Mwanza, akaelekezwa duka flani, akafika. Bei ni laki mbili na nusu. Akaona ya wahenga yanazidi tu kutimia. Basi akaingia kwenye maelewano ya bei, na mwisho wa siku akauziwa kipuri kwa shilingi laki moja. Akampelekea fundi, fundi akafunga ile ‘sensor’. Kuwasha gari, ni mara moja tu. Akamlipa yule fundi elfu hamsini kama sijasahau. Na gari anapiga nayo masafa mpaka kesho kutwa.
Sasa kwa case hiyo, hapo mtasema nini wadau?. Kweli gari za aina ya Xtrail zina shida!!!!?. Kwenye hiyo case unapata picha ya ufundi na picha ya bei pia. Na hiyo case ni Mwanza mjini. DSM mjini nadhani hiyo spare angepata chini ya hapo, I guess (ila fundi usi-guess).
Kama unapenda Xtrail and the likes, nunua wala usiogope. Kiafya si vizuri kukandamiza nafsi pasipo sababu za msinigi. Humuhumu JF kuna wamiliki wengi tu wa hizo gari na wana taarifa chanya nyingi tu kuhusu Nissan Xtrail. Dunia hivi sasa ni kijiji. Taarifa zote zipo kiganjani mwako, labda uwe mvivu tu. Information ni power. Watu wa Xtrail mnaanzisha kijiwe chenu humu ndani, mnaonyeshana machaka ya maduka ya vipuri, chocho za mafundi wa ukweli then hii ‘phobia’ inazikwa rasmi na Xtrail zinandelea kuwa Xtrail.

Asante sana Infopaedia kwa kuuelezea ukweli wa XTrail na ndio maana wengine sie tukitaka kununua gari kwanza tunataka kufunua boneti na mpaka tukiona carburettor ndio tunaamini kuwa ni gari na sio toy, tuseme unaenda nyumbani Kigoma ukitumia Xtrail mara umesimama pale Igunga kujaza mafuta na gari ikakataa kuwaka sijui fundi utampata wapi? sijui spare utaipata wapi?, kuna mbunge mmoja kijana wa Nzega alivamia kitu kama hicho (Sio Xtrail) kila mara gari hilo lilikuwa likichokonolewa huko porini na mafundi wa mwembeni sijui kama bado anatumia gari hiyo, maana yangu ipo pale pale kuwa kwa watu wa chini na kati kiuchumi gari hizo ni pasua kichwa na nina mfano wa rafiki yangu hakusikia ushauri wangu akanunua Honda Stream ikamfanyia kituko kama ulivyoelezea akahangaika karibu mwaka mzima kuja kufanya diagnosis kifaa ilibidi tuagize Japan kweli kilipatikana kwa dollar 580 mpaka mlangoni ...lakini yule bwana mrija wa pesa ulikuwa umekatika matokeo yake sasa hivi watu wanampa 1.8M au wengine wanamshauri abadilishe injini aweke ya Toyota corolla , mfano wako wa bodi ya plastic kwa safety issues unakubalika 100 % lakini kumbuka dukani hakuna spare ila kwa wenye uwezo kwao sio tatizo kwani dunia ni kijiji kwa wale wenye kipato kizuri.
 
Mimi nina mtu anahiyo Gari, Kuna kipindi Nilitaka kununua kama hiyo, huyo huyo mtu akaniambia nisinunue kwani siyo Gari ni matakataka

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna dhana imejengeka kwa watu wengi kuwa Extrail sio gari,kwahiyo yawezekana hata aliekwambia wewe ni mmoja wao wanaoneza hiyo dhna.Ni kama wale wanaosema Prado 90 series zinachomoka matairi,sijajua hili linatokea wapi wakati wajapan wanaendelea kuyauza...
 
Asante sana Infopaedia kwa kuuelezea ukweli wa XTrail na ndio maana wengine sie tukitaka kununua gari kwanza tunataka kufunua boneti na mpaka tukiona carburettor ndio tunaamini kuwa ni gari na sio toy, tuseme unaenda nyumbani Kigoma ukitumia Xtrail mara umesimama pale Igunga kujaza mafuta na gari ikakataa kuwaka sijui fundi utampata wapi? sijui spare utaipata wapi?, kuna mbunge mmoja kijana wa Nzega alivamia kitu kama hicho (Sio Xtrail) kila mara gari hilo lilikuwa likichokonolewa huko porini na mafundi wa mwembeni sijui kama bado anatumia gari hiyo, maana yangu ipo pale pale kuwa kwa watu wa chini na kati kiuchumi gari hizo ni pasua kichwa na nina mfano wa rafiki yangu hakusikia ushauri wangu akanunua Honda Stream ikamfanyia kituko kama ulivyoelezea akahangaika karibu mwaka mzima kuja kufanya diagnosis kifaa ilibidi tuagize Japan kweli kilipatikana kwa dollar 580 mpaka mlangoni ...lakini yule bwana mrija wa pesa ulikuwa umekatika matokeo yake sasa hivi watu wanampa 1.8M au wengine wanamshauri abadilishe injini aweke ya Toyota corolla , mfano wako wa bodi ya plastic kwa safety issues unakubalika 100 % lakini kumbuka dukani hakuna spare ila kwa wenye uwezo kwao sio tatizo kwani dunia ni kijiji kwa wale wenye kipato kizuri.

Kuna mdau na yeye alishauriwa kuhusu kununua Honda step wagon akaleta ujuaji wa story za dunia ni kijiji kimoja ntaagiza from japan,tukamwambia sawa mkuu.

Gari lilivyoanza kuloga,kila akitueleza gari yangu imezingua tunamwambia dunia ni kijiji pambana mkuu.

Ile gari alikuja kumuuzia mkenya kwa hela sawa na bure.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna dhana imejengeka kwa watu wengi kuwa Extrail sio gari,kwahiyo yawezekana hata aliekwambia wewe ni mmoja wao wanaoneza hiyo dhna.Ni kama wale wanaosema Prado 90 series zinachomoka matairi,sijajua hili linatokea wapi wakati wajapan wanaendelea kuyauza...

Kwani hayachomoki?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nilinunua gari Zanzibar na nilichofanya nilienda na Document TRA ya Zanzibar kujua kiasi ambacho kililipiwa wakati inaingia Gari hiyo Zanzibar ,baada ya hapo nakaenda TRA ya Bongo wakatipa Amount kamili na tofauti yake ilikuwa million moja tu ambayo nilipaswa kulipia, maana Zanzibar kodi yao IPO chini ukilinganisha na TZ bara.

Ikawa hivi sasa:
Ongezeko la kodi 1,000,000
Kusafirisha gari 300,000 - 350 ,000
Clearence 500,000 inategemea na Agent

Gari ikawa mkononi ila sijui kwa sasa mambo yakoje zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesahau kubadili no sh 500,000/=
 
Back
Top Bottom