Kununua gari toka Zanzibar

Mwenye gari na wenye magari, ila mleta uzi ametaka tuu kujua gharama atakazo chajiwa na TRA zina weza kuwa kiasi gani? hayo mengine kwamba x-trail ipo hivi mara vile itakuwa mwenyewe alishafanya utafiti na ndio maana anataka kununua.
 
Nilinunua gari Zanzibar na nilichofanya nilienda na Document TRA ya Zanzibar kujua kiasi ambacho kililipiwa wakati inaingia Gari hiyo Zanzibar ,baada ya hapo nakaenda TRA ya Bongo wakatipa Amount kamili na tofauti yake ilikuwa million moja tu ambayo nilipaswa kulipia, maana Zanzibar kodi yao IPO chini ukilinganisha na TZ bara.

Ikawa hivi sasa:
Ongezeko la kodi 1,000,000
Kusafirisha gari 300,000 - 350 ,000
Clearence 500,000 inategemea na Agent

Gari ikawa mkononi ila sijui kwa sasa mambo yakoje zaidi



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utalazimika kulipia 'The difference'. Yani kama gari iliingia Zbar wakalipa import Duty na VAT wewe utalazimika kulipia 25% ya Uchakavu. So hapo uandae kama M2-3.
pia kupakia gari kwenye meli ni kama laki tano. Agent fee kama laki mbili.
Mpaka hiyo gari unaiingiza bara barani itakuwa imekukamua kama M9-10.
Niliwahi kuingiza gari toka Zbar mwak 2008.
 

Ilikuwa mwaka gani mkuu?
 
Nakumbuka mwaka Jana kuna rafiki yangu alinunua gari Zanzibar kwa 7m alipolileta bara kodi ilikua 4m,
Sikumbuki aina ya gari maana Mimi najua magari ninayoyapenda i.e Spacio, Prado n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana mkuu. Nimesoma post zako na nimepata mwanga wa kutosha tu. Shukurani kwa muda wako mkuu.
 
Shukrani sana mkuu
Mkuu naona kama uko interested na hiyo issue. Kuna maelezo nimeyapata nje ya JF. Ukishanunu hiyo gari kabla hujasafirisha, hakikisha umefanya mpango wa plate number na umeipata. Safirisha gari ikiwa tayari na number za Bara, ikifika unaichukua. Lakini ikifika then isubiri process ya number, kuna majanga ya kuchomolewa vitu kwenye gari. Nimekutana na hiyo news wati nadodosa.
 
Mimi nina mtu anahiyo Gari, Kuna kipindi Nilitaka kununua kama hiyo, huyo huyo mtu akaniambia nisinunue kwani siyo Gari ni matakataka

Sent using Jamii Forums mobile app
Alikupa sababu gani? Ulimuuliza sababu? Sijaona sababu ya msingi ya kusema hivyo wakati kilasiku zinaingia, zinauzwa na watu wanatembea nazo kila siku. Pili kuhusu spare zake sidhani kama wanaosema ni expensive wapo wapo sawa, maana mie nanunua spare pale Ilala kwa bei ya kawaida tu. People have created a phobia to the unknown!!!
 
I also came across Nissan Phobia before. Kwa kuwa sikuwa na ujuzi wa magari nilikaa nazo mbali sana!
 
Watanzani wengi tunapenda vitu feki na ndiyo shida yetu. Ukiwauliza hata hawajui kuwa Toyota nazo zina spea original ambazo bei yake ipo juu pia. Hata ukifuatilia wenye Magari wengi wanachakaza Magari yao kwenye gereji za uchochoroni. Amini nawambieni gereji za watu wanaojitambua hawezi kukubari kufungi spea feki kwani itamuharibia jina lake kibiashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Thanks sana mkuu kwa info ya kiinteligensia.

Nachukua wazo lako kwa mikono yote mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…