Kununua vocha kimakosa

Kununua vocha kimakosa

Tempest

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
245
Reaction score
430
Habarini wana JF

Kuna changamoto nimepata nimenunue vocha ya 300,000 bahati mbaya kupitia NBC app badala ya kutuma kama pesa ya kawaida

Kuna namna yoyote naweza kuipeleka sehemu nipate cash? hata kwa hasara fulani hivi

Ikishindikana kabisa ntakuwa najiungia tu bundle za mwezi za airtel hizi unlimited ila sina mipango mirefu hivyo kwasasa, mwenye idea nitashukuru
 
Nirushie nikupe 200k
 
Screenshot_20240616-114906~2.jpg
 
2014 nilikua nataka kununua bando la internet la 40,000 kwenye kununua muda wa maongezi m pesa nikanunua 400,000, kiufupi nilihangaika Voda hakuna msaada wowote Hio imeshaenda, jioni nikapiga vyombo nikawaunga watu wangu wa karibu bando la mwezi mmoja mmoja Kila mtu mpaka vocha ikaisha, fanya ivo utakuja kunishukuru
 
Umesikia wapi hivyo ndugu, ngoja niweke screenshots
Hapo dawa ni kujunga unlimited tu,kisha unaingia YouTube unaangalia mavideo tu. Ukilala ukiamka we unaangalia videos tu, ukiona unasinzia we unaweka video tu inatembea!!

Sasa utafanyaje wakati Airtel na NBC wamekataa kukurudishia Hela yako.

We peruzi websites za video hadi macho yavimbe nawe uwakomoe😅😅
 
Back
Top Bottom