Waliotengeza kama zilivyo hawakushindwa 'kuzinyonya' walikuwa na maana na vipimo vyao vya kiusalama.
Naamini ukitaka rim ya design hiyo unayotaka ku modify utapata special kabisa zilizotengenezwa kwa viwango.
Usitafute kufa kizembe kwa ajali kwa kutaka kuiga mambo yasiyokuwa na tija yeyote.
Nina hakika ukiulizwa sasa hivi sababu za kutaka kufanya hivyo utasema umeona kwenye movie au wenzio mtaani.
Niamini mimi hao wa kwenye movie za nje hizo zao zilitengenezwa maalum, hazikufanyiwa modification. Hao wa mitaani wengi wao ndio kama wewe wanaelekea kujidhuru kwa kuiga wasivyovijua.