Kunywa maji mengi

Kunywa maji mengi

543852_464031966990607_1905986946_n.jpg
 
Sasa mkuu unaposema anapokunywa maji na kukojoa sana ulitaka hayo maji anayokunywa yaende wapi?? Hebu saidia hapo tafadhali

Unapokuwa ni mgonjwa wa kisukari (diabetes mellitus, ile inayopanda) kunakuwa na hali kama ya ile ya osmosis. Unayatamani maji na unayanywa lakini hayakai mwilini kwa muda, yaani huchukui hata dakika 2 toka uyanywe na upate mkojo. Hiyo ndiyo maana yangu, unapokunywa maji hupaswi kuyapitisha haraka. Yanapaswa kukaa mwilini kwa muda kiasi kabla hayajapitishwa. Kwa hiyo nilichotaka kusema ni kuwa, kunywa maji inaweza kuwa sawa kama maji hayo yanabaki mwilini na kufanya kile maji yanayofanya mwilini na baadae kupitishwa kwenye kibofu. Sio kuyanywa na kuyapitisha wakati huo huo!

NB: Haya si maelezo ya kitaalam bali yanatokana uzoefu wangu kama known IDDM case for 12 years.
 
Wakuu,
Ninakunywa maji mengi kwa siku, lita 7 hadi 10. Nafahamu kwamba inashauriwa kwa siku mtu unywe maji yasiopungua lita 3. Je kuna madhara yoyote kiafya kwa kunywa maji yanayozidi kiasi hicho?

NB: Nafanya mazoezi ya viungo kwa wastani wa saa moja hadi moja na nusu kwa siku mara tano kwa wiki.
 
Je wewe mwenyewe umeona mabadiriko ya mwili? Kama ngozi kuwa nzuri, kutougua, kuwa mwepesi, kula vizuri pia inahitajika etc

yaani unajionaje utofaiti wa kabla ya kunywa hizo lita kila siku?
 
Mimaji yote hiyo lita 10 unanywea sifa? Wewe lazima utakuwa mgonjwa si bure! Bora ingekuwa chini ya lita 5 wahi kapime.
 
Duh umetisha lita 10 kwa siku si mchezo
 
Je wewe mwenyewe umeona mabadiriko ya mwili? Kama ngozi kuwa nzuri, kutougua, kuwa mwepesi, kula vizuri pia inahitajika etc

yaani unajionaje utofaiti wa kabla ya kunywa hizo lita kila siku?

Yeah! kuna mabadiliko kwa kuwa nafanya mazoezi na kupungua uzito. Tatizo ninatoka jasho jingi sana wakati wa kufanya mazoezi na nakunywa maji mengi kuliko inavyoshauriwa.
 
Japo me siyo daktari lakini kuna matatizo. Unapokunywa maji mengi kupita kiasi unaondoa madini muhimu mwilini kama chumvi nk. Tafadhali tumia kila kitu kwa kiasi.
 
nani analipa bills za maji? angalia msigombane..., kama kunywa tu lita 10, najua chooni unaenda zaidi ya mara 20 kukojoa. Kila ukiflash ni lita 9....., daah. Kwa siku jumla mamia ya lta
 
nani analipa bills za maji? angalia msigombane..., kama kunywa tu lita 10, najua chooni unaenda zaidi ya mara 20 kukojoa. Kila ukiflash ni lita 9....., daah. Kwa siku jumla mamia ya lta

hahaaaaaaaa
 
Wakuu,
Ninakunywa maji mengi kwa siku, lita 7 hadi 10. Nafahamu kwamba inashauriwa kwa siku mtu unywe maji yasiopungua lita 3. Je kuna madhara yoyote kiafya kwa kunywa maji yanayozidi kiasi hicho?

NB: Nafanya mazoezi ya viungo kwa wastani wa saa moja hadi moja na nusu kwa siku mara tano kwa wiki.

Rejeta itakuwa imepasuka...
 
nani analipa bills za maji? angalia msigombane..., kama kunywa tu lita 10, najua chooni unaenda zaidi ya mara 20 kukojoa. Kila ukiflash ni lita 9....., daah. Kwa siku jumla mamia ya lta

Hahahaa we utakuwa mchumi eeeh!
 
Japo me siyo daktari lakini kuna matatizo. Unapokunywa maji mengi kupita kiasi unaondoa madini muhimu mwilini kama chumvi nk. Tafadhali tumia kila kitu kwa kiasi.

Natoka jasho jingi sana wakati wa kufanya mazoezi kiasi cha kulowanisha nguo zote na jasho jingine kutirirka chini. Huoni inaweza kuwa sababu ya kunywa maji mengi ili ku-replace na pengine kusiwe na madhara?
 
Back
Top Bottom