Na anzia hapa. Bikra inatolewa mara moja hali kadhalika mimba inaingia mara moja.
Zinaa ni deni kaka,wewe kama ni mzinifu usitegemee kuoa mfano wako.
Hata mambo ya kuoa bikra au kuto kuoa bikra majibu yake sahihi ni ya kiroho kama baadhi ya watu wanavyoita yaani ya kidini.
Lazima watu wajue hapa duniani watu wanaishi pande mbili,mimi nasema ulimwengu mbili za kimahusiano.
Ulimwengu wa kwanza ni ule ambao si wa kidini huu kupata suluhisho la jibu hili ni ngumu sana.
Ulimwengu wa pili ni ulimwengu wa dini. Ulimwengu wa dini unatambua thamani ya mwanamke na nafasi yake. Unatambua ya kuwa maisha hayaishi katika bikra tu,wala katika kuzaa,bali wala katika kukosa uzao.
Bikra ni heshima ya mwanamke na ni thamani kubwa kwake lakini katu bikra haijawahi kuleta ubora wa mwanamke. Ubora wa mwanamke ni uchamungu wake,bali kwa kila binadamu.
Sisi binadamu tuna badilika kila kukicha leo unalala ukiwa mwema kesho una amka ukiwa muovu. Cha msingi sisi wanaume tuombe salama na tuombe wake wema,ukijaaliwa kumpata mwema na ukamtengenezea mazingira mazuri ya usimamiza lazima utafurahia maisha.
Kama hujaelewa vyema maandishi yangu,rejea kauli hizi "ZINAA NI DENI" na "USIPIGE PASI NGUO IKIWA CHAFU" na "NDEGE WAFANANAO NDIO HURUKA PAMOJA"
Sent using
Jamii Forums mobile app