Si utumwa.
Lakini, kupenda na kuuthamini utamaduni wako maana yake uwashutumu watu walioamua kuoa au kuolewa na wazungu?
Utamaduni wetu ni pamoja na kuheshimiana.
Kuheshimiana ni pamoja na kujua mipaka ya mambo ya faragha.
Mambo ya faragha ya mtu ni pamoja na uchaguzi wa nani anataka kumuoa au kuolewa naye.
Sasa mtu mmoja baki kumpangia mtu mwingine baki nani wa kuoa au kuolewa naye, au kumsema nani wa kuoa au kuolewa naye, si utamaduni wetu.
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikemea ubaguzi wa rangi. Alikemea weupe kubagua weusi Afrika ya Kusini.
Watu wakaja na dhana ya uzawa Tanzania. Akaikemea nayo. Akasema ni ukaburu tu ule ule.
Sasa kwa nini tunabagua walioamua kuoa au kuolewa na wazungu kwa hiyari zao?
Huu sio ubaguzi ule ule alioukemea Mwalimu Nyerere?
Martin Luther King alisema tusimhukumu mtu kwa rangi ya ngozi yake, bali kwa tabia zake, sasa mbona tunaingia kwenye mtego wa ubaguzi wa rangi wa kubagua watu kwa sababu ni wazungu?