Habarini mabaharia wenzangu, hasa hasa ambao hawajaoa, kama likichwa la habari linavyojieleza (kwa sauti ya jamaa aliesoma PCM akaona kila kitu anakijua), ngoja nieleze kidogo hapa, unajua ukiijua hesabu/maths vizuri sana yaani ukawa mbobezi haswa, Kuna katabia huwa kanaibuka ka kusimamia jambo unaloliamini kwa msisitizo hii inatokana na kukariri kanuni au taratibu za hesabu kwa mfano Mdogo MAGAZIJUTO.
Bhana kwasasa huku mtaani singo mama wametamalaki:
Pisi Kali nyingi ni singo mama
Wanawake wanaojua kutafuta na kuisimamia hela ni singo mama
Wanawake wenye makalio mazuri ni singo mama
Wanawake wenye sifa za u-wife material ni singo mama tayari
Wanawake wanaojua kutunza waume ni singo mama
Wanawake wenye elimu zao na biashara zao ni singo mama tayari(kwa wanaotaka kulelewa)
Wanawake maslay queen ni singo mama tayari
Wanawake waaminifu ni singo mama
HAPA HAKUNA NAMNA LAZIMA LAZIMA TUENDANE NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.hakuna cha kuona kaburi la mzazi mwenzie