Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,077
Nimekuta mchango humu JF ikiwajadili Wakurya, Wanyiha na Wazaramo kuhusu kuona wake wengi; naomba Modi mniruhusu kuufufua kwa njia ingine na kwa malengo mengine kama ifuatavyo. Mababu zetu walikuwa na uwezo ambao sisi wa leo tunaonekana hatunao.
Shizukan anasema... "tusikopi maisha ya watu wa wakati uliopita. Naamini kama ungekuwepo wakati huo wa babu yako ungekubaliana na mimi kuwa hakuwa mtu dhaifu dhaifu kama tulivyo sisi wa kizazi cha leo.
Hapo ulipo chips na mafuta ya viwandani vimeshakuharibu na mapishi ya hawa wake zetu ndio wanapika sumu jikoni, sasa hiyo nguvu ya kuhudumia mke mmoja tu ni issue tutaweza kweli wake wa4? Hilo la kwanza,
Waislam wengi wanatoka Pwani ambako uzalishaji mali si kama huko Mbeya ulikotoka. Mwanamke wa Kinyiha na wa Kizaramo wanafanana linapofika suala la kushika jembe? Hapo utaona kuwa, Babu yako kazi yake ilikuwa kupanda mbegu, wake zake wanapiga kazi na kulea kwani shambani wanajiweza. Lakini wapaka hina wa4 wanapozalishwa watoto wa3 kila mmoja na wao hawana mashamba zaidi ya kumtegemea huyo mume ambaye naye anategemea kiunga cha minazi au kugema pombe, hao watoto wanakula nini zaidi ya kushindia madafu mkuu?
Ukienda kwetu Mara, mama wa Kikurya ni ngangali na huolewa kwa sababu ya ungangari wake kwani mume anataka kuongeza nguvu ya uzalishaji mali. Sasa hata kama watoto wengi watazaliwa, mama zao ndio watunzaji tofauti wa watu wa Pwani.
Mkuu Highlander wewe unao uwezo wa kumuiga babu? (Namaanisha uwezo wa kupiga round kadhaa kwa wiki bila kumuona MziziMkavu)
Nisema hapa kuwa pana ukweli wa utofauti kutokana na afya zetu za sasa, lakini pia mila zetu zinao umuhimu katika kuamua nini cha kufanya: kuoa wake wengi au la... Mimi silichukuli hili kama suala la kidini, bali suala la kiuchumi na Afya...
\
Unaweza? na kimwana kakubali, chukua.... huwezi? waachie wenye meno.....