Kuoga kila siku ni afya au ni utamaduni na mazoea tu?

Kuoga kila siku inategemeana na maeneo sasa mtu yuko Makete Nyuzi joto 19 ana ubavu wa kuoga kila siku?

Saudi Arabia kuna nyuzi joto 45°C lakini bado watu hawaogi[emoji1787][emoji1787] ishu sio Africa ishu ni pesa tu...Tanzania kuna watu kibao hawaogi kila siku.
Hata Oman nyuzi joto hadi 47°C lakini nilikuwa naoga kwa mbinde [emoji23][emoji23][emoji23]. Lakini kama ukienda desert au kufanya mtoko ukirud ni lazima uoge tu, lakini ukikaa ndani haina haja ya kuoga.
 
Pia kuna sehemu inaitwa Dareda huko mbulu vijijini mkoa wa Manyara kuna baridi sana ukiamka asubuhi unakuta gear level hadi siti za gari zinavuja maji, nilikaa wiki moja na sikuthubutu kuoga kabisaa.
 
Kuoga kila siku inategemeana na maeneo sasa mtu yuko Makete Nyuzi joto 19 ana ubavu wa kuoga kila siku?

Saudi Arabia kuna nyuzi joto 45°C lakini bado watu hawaogi[emoji1787][emoji1787] ishu sio Africa ishu ni pesa tu...Tanzania kuna watu kibao hawaogi kila siku.
Niko makete naoga kila siku, we utakuwa mchafu tu
 
Pia kuna sehemu inaitwa Dareda huko mbulu vijijini mkoa wa Manyara kuna baridi sana ukiamka asubuhi unakuta gear level hadi siti za gari zinavuja maji, nilikaa wiki moja na sikuthubutu kuoga kabisaa.
Njombe je?
 
Siungi mkono hoja...

Tuogeni kila siku pale tunapoweza...
 
Lakini unaweza kuoga mara kwa mara ikiwa umetokwa jasho, uchafu kama vile vumbi, moshi, au sababu nyingine ya kukufanya uoge. Kama sababu ya kukufanya uoge kila siku ilikuwa ni ya kiafya, basi unaweza kupunguza idadi hiyo.
Yaaas, suala la kuoga lipo na uhuru mkubwa sana wa mtu binafsi na mazingira kuchagua, sawasawa tu na kukata gogo

Unaweza kuoga popote kuanzia mara mbili kwa siku hadi mara mbili kwa wiki na bado ukawa upo katika range ya kiafya.!
 
Inategemea, moja au sifuri vyovyote tu. Zaidi ni mara moja haswa.

Hint: Sent from the green city. Halafu hili n swali langu kweli? Either way nishajibu🤨
Kwa siku unaoga mara ngapi?
 
Je! Huwa unaoga kila siku? Kama jibu lako ni ndiyo, basi jua kuwa hauko peke yako.

Katika maeneo mengi duniani watu huoga kila siku, lakini nchini China chapisho la Harvard Healthy linaeleza kuwa nusu ya watu huoga mara mbili tu kwa wiki.

Lakini umewahi kujiuliza kwanini watu wengi huoga kila siku? Pengine jibu lako ni sababu za kiafya. Kwa mujibu wa Harvard, kuoga kila siku kwa watu wengi ni utamaduni au utaratibu wa kijamii zaidi kuliko suala la kiafya.

Na hii huenda ndiyo sababu suala la watu kuoga hutofautiana kutoka nchi moja na nyingine.

Mbali na suala la kiafya, baadhi ya watu wamesema huoga kila siku ili kutoa harufu mbaya mwilini, kuwasaidia kuondoa usingizi, ni sehemu ya wao kufanya mazoezi.

Lakini ni wazi pia kuwa kuoga kila siku kunaweza kuwa njia ya makampuni ya bidhaa za kusafisha mwili kuendeleza biashara zao. Linapokuja suala la afya, haijathibitishwa kuwa kuoga kila siku kuna mchango kiafya.

Tena inaelezwa kuwa kuoga kila siku kunaweza kuwa na matokeo hasi kama vile kuifanya ngozi kuwa kavu kwa kuisugua hasa kwa maji moto. Kwa kawaida, ngozi yenye afya huwa na kiasi fulani cha mafuta, uwiano mzuri wa bakteria na viumbe vingine vidogo (microorganisms). Unapooga unaondoa hivi vyote na hivyo ngozi inaweza kuwa kavu na kupauka.

Ngozi kavua na yenye mpasuko inaweza kuruhusu bakteria wenye madhara (allergens) kupenya na kusababisha athari za ngozi. Chapisho la Harvard linaeleza pia sabuni za kuogea za kuua bakteria (antibacterial) zinaua bakteria wanaotakiwa kwenye ngozi.

Hii huathiri uwiano wa viumbe hao kwenye ngozi, na huweza kupelekea uwepo wa viumbe wasio rafiki ambapo hawasikii dawa.Mfumo kinga wa ngozi unahitaji kichocheo kutoka kwa bakteria, uchafu na vitu vingine vya kwenye mazingira ili kuweza kujitengemezea kinga.

Hii ni moja ya sababu ya wataalamu wa ngozi kushauri watoto wasiogeshwe kila siku kwani kufanya hivyo kunaweza kuipunguzia ngozi uwezo wa kujitengenezea kinga yake.

Aidha, sababu nyingine ya kukufanya usioge kila siku inaweza kuwa maji unayotumia.

Maji ambayo hutumiwa kusafisha mwili yanaweza kuwa na chumvi, kemikali mbalimbali au madini (heavy metals, chlorine, fluoride) na dawa za kuuwa wadudu.

Vyote hivi vinaweza kuwa na madhara kwenye ngozi. Hata hivyo, licha ya kuwa hakuna kiwango kinachokubalika kwa wote kuhusu suala la kuoga, wataalamu wanashauri kuwa kuoga mara kadhaa kwa wiki kunafaa kwa watu wengi.

Lakini unaweza kuoga mara kwa mara ikiwa umetokwa jasho, uchafu kama vile vumbi, moshi, au sababu nyingine ya kukufanya uoge. Kama sababu ya kukufanya uoge kila siku ilikuwa ni ya kiafya, basi unaweza kupunguza idadi hiyo.
Unakuta mwanaume anakoga kila siku kila saa, sasa sijui anataka agundue nini
 
Uku makete afadhali wewe kwa siku unaoga mara moja,mimi nilishawahi kupiga hadi siku 10 sijaona maji
Makete kuna joto sana njoo hapa kawatele mbeya uona kama kukoga ni lazima
 
Haimaanishi uwe mchafu brother usipojisafisha nako mfumo wa ngozi kupumua(breathing mechanism) unaziba ziba pale kwenye vinyweleo kuhusu harufu utajua mwenyewe na yule unayemlala.
Faida za kutokuoga kila siku
1.una save maji
2.kama ili zoea kuoga ya moto unaokoa umeme
3.unaokoa pesa maana umeokoa nishat na maji
4.afya ya ngozi na hapa ndo point ya kujitanua. Iko Hivi brother kuna bacteria wa kwenye ngozi ambao ni muhimu so usipooga una balance hao bacteria na kama utaoga basi oga Kwa mtindo wa kujifuta na sponji.
5.kuimarisha nywele usipooga nywele hazinyonyoki.
6.kuimarisha kinga ya mwili
7.kama unataka kujenga body asilia usioge sana
8.harufu asilia labda ukioga target maeneo kama ya kwapa na sehemu za siri ila ukijimwagia maji mengi unaondoa bacteria hivyo na harufu asilia unaondoa.
Usiwe serious na kuoga Kwa week angalau Mara tatu inatosha.
 
Kila kitu kina faida na hasara zake ila huwa tunalinganisha ukubwa wa faida na hasara za kitu hicho ndipo tunafanya machaguzi.
 
Unasave pesa ya kununua mafuta ya kupaka unafanya mambo mengine sio unashinda kuogaoga Tu....
Hatujaja kuoga kwenye hii dunia,dunia ni njia wote tunapita sasa wewe ukikazana kuoga njiani unatushangaza..
 
Je, huwa unaoga kila siku? Kama jibu lako ni ndiyo, basi jua kuwa hauko peke yako.

Katika maeneo mengi duniani watu huoga kila siku, lakini nchini China chapisho la Harvard Healthy linaeleza kuwa nusu ya watu huoga mara mbili tu kwa wiki.

Lakini umewahi kujiuliza kwanini watu wengi huoga kila siku? Pengine jibu lako ni sababu za kiafya. Kwa mujibu wa Harvard, kuoga kila siku kwa watu wengi ni utamaduni au utaratibu wa kijamii zaidi kuliko suala la kiafya.

Na hii huenda ndiyo sababu suala la watu kuoga hutofautiana kutoka nchi moja na nyingine.

Mbali na suala la kiafya, baadhi ya watu wamesema huoga kila siku ili kutoa harufu mbaya mwilini, kuwasaidia kuondoa usingizi, ni sehemu ya wao kufanya mazoezi.

Lakini ni wazi pia kuwa kuoga kila siku kunaweza kuwa njia ya makampuni ya bidhaa za kusafisha mwili kuendeleza biashara zao. Linapokuja suala la afya, haijathibitishwa kuwa kuoga kila siku kuna mchango kiafya.

Tena inaelezwa kuwa kuoga kila siku kunaweza kuwa na matokeo hasi kama vile kuifanya ngozi kuwa kavu kwa kuisugua hasa kwa maji moto. Kwa kawaida, ngozi yenye afya huwa na kiasi fulani cha mafuta, uwiano mzuri wa bakteria na viumbe vingine vidogo (microorganisms). Unapooga unaondoa hivi vyote na hivyo ngozi inaweza kuwa kavu na kupauka.

Ngozi kavua na yenye mpasuko inaweza kuruhusu bakteria wenye madhara (allergens) kupenya na kusababisha athari za ngozi. Chapisho la Harvard linaeleza pia sabuni za kuogea za kuua bakteria (antibacterial) zinaua bakteria wanaotakiwa kwenye ngozi.

Hii huathiri uwiano wa viumbe hao kwenye ngozi, na huweza kupelekea uwepo wa viumbe wasio rafiki ambapo hawasikii dawa.Mfumo kinga wa ngozi unahitaji kichocheo kutoka kwa bakteria, uchafu na vitu vingine vya kwenye mazingira ili kuweza kujitengemezea kinga.

Hii ni moja ya sababu ya wataalamu wa ngozi kushauri watoto wasiogeshwe kila siku kwani kufanya hivyo kunaweza kuipunguzia ngozi uwezo wa kujitengenezea kinga yake.

Aidha, sababu nyingine ya kukufanya usioge kila siku inaweza kuwa maji unayotumia.

Maji ambayo hutumiwa kusafisha mwili yanaweza kuwa na chumvi, kemikali mbalimbali au madini (heavy metals, chlorine, fluoride) na dawa za kuuwa wadudu.

Vyote hivi vinaweza kuwa na madhara kwenye ngozi. Hata hivyo, licha ya kuwa hakuna kiwango kinachokubalika kwa wote kuhusu suala la kuoga, wataalamu wanashauri kuwa kuoga mara kadhaa kwa wiki kunafaa kwa watu wengi.

Lakini unaweza kuoga mara kwa mara ikiwa umetokwa jasho, uchafu kama vile vumbi, moshi, au sababu nyingine ya kukufanya uoge. Kama sababu ya kukufanya uoge kila siku ilikuwa ni ya kiafya, basi unaweza kupunguza idadi hiyo.
🙏
 
Back
Top Bottom