Kuombea mvua wakati ni huu viongozi wa dini sauti zenu zisikike

ujinga mtupu
 
Soma maneno ya Kagame,huwezi kutatua matatizo ya Afrika kwa maombi na Dua,Mungu hawezi kukupa kitanda,atakupa miti!ni kazi yako kutengeneza kitanda kwa kutumia bongo aliyokupa,
 

Attachments

  • 20221002_201547.jpg
    76.5 KB · Views: 3
Sijawahi ona zile kampeni za upandaji miti kama alizokuwa anahamasisha Mzee R. Mengi.
Bwana Mungu wa Mbinguni amlaze mahala pema penye kaubaridi na kakivuli ka miti huko Peponi,sote tuseme Amen.
 
Thubutuuu. Maombi ya mvua mapema hivi, subiri wakarbie tarehe za mvua walivyotabiri TMA ndio utawaona. Unafikiri na wao hawana akili ee
 
Kiongozi aliepo si chaguo la mleta mvua,

Mungu alileta kiongoz aliekua na maono akaleta na mvua ili kuirahisisha kazi,

wauaji wakafanya yao, mvua ikakata, jua likashika kasi, raia hawajui waseme nini

Maombi yanayoambatana na vitubio ni muhim sana kwa taifa la tz
 
WALIOHARIBU MAZINGIRA
WALIOKATA MITI
WALIORUHUSU KULIMA KWENYE VYANZO VYA MAJI
AMBAO NI CCM NA SERIKALI YAKE NDIO WANAPASWA WAKAE CHINI WAOMBEE MVUA MSIWACHOSHE VIONGOZI WETU WA DINI HAWAHUSIKI NA UHARIBIFU HUO
 
Amka jinyoshe hapo hapo kitandani, kumeshakucha tayari. Simama upambane na siku mpya maishani mwako.
 
Gharama za kuchimba mabwawa ta kuvuna maji inaanzia kiasi gani, kwa makadirio ya shamba la ekari 10
 
Gharama za kuchimba mabwawa ta kuvuna maji inaanzia kiasi gani, kwa makadirio ya shamba la ekari 10

Bwawa kubwa la eneo la heka kumi, au bwawa ndani ya shamba la heka kumi?
 
Tunaangamia pia kwa kukosa maarifa.
Kuna uangamizaji mkubwa sana wa miti/misitu. Miti inakatwa hovyo kwa kilimo cha hovyo kabisa na ardhi ikichoka kidogo wanakimbilia ardhi mpya kwa kukata miti.
Hii nimeshuhudia huko manyara.
Watu walazimishwe kulima eneo dogo kwa mbinu za kisasa, mavuno mengi. Kwa njia hii misitu itaokolewa na mvua zitanyesha.
Unaharibuje mazingura halafu unataka upate kwa kuomba!
Kingine tujenge mabwa kuhifadhi maji ya umwagiliaji.
Mvua zinanyesha nyingi na maji yanakwenda baharini kugeuka ya chumvi. Wiki moja tu baada ya mvua kunyesha tunahangaika kutafuta maji.
Tuombe lakini pia tutumie akili alizotupa Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…