Gily Gru
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 8,632
- 23,673
Mimi ni mchaga kutokea Mkuu Rombo, ila pia ni mkazi wa Dar es Salaam japo sipendi kuitwa mwanaume wa Dar.
Kuna jambo moja linanikera sana kwa kweli kila nikienda nyumbani Kilimanjaro nikikutana na wakazi wengi amabao ni ndugu au wachaga tu huwa wana tabia ya kuomba hela sana. Ukikutana na mtu asipokuomba hela basi atakuomba kapombe. Kuna siku nakumbuka kuna ndugu yangu kuona niko kwenye bodabda kaisimamisha nasema labda ananisalimia kumbe akaniambia “nipe pesa ndi umefika za motomoto kabla hazijaisha”. Siku ukiwa umeenda huna pesa unakuwa kama mwivi kazi ni kujificha migombani huko au chini ya mikahawa ili wasikuone.
Wana mbinu nyingi za kuomba pombe au pesa, ila hawaombi sukari au chakula cha watoto nyumbani. Basi nikakutana na mtu akanambia “Nikukombe kiadu” maana yake “nikulambe kiatu” akimanisha anaomba hela. Nikamnjibu “nilambe na chako pia”, yule mama alinichukia sana akawa anasema mbovu eti nilivyokuwa mdogo alinifuta mavi sasa nimekuwa nimekuwa jioni.
Kuona maneno maneno anaacha huko siku nikampa elfu mbili yule mama akashika mikono yangu akaniambia maneno matamu upate nyingi nyingi. Moja ya maneno ambayo nishawahi sikia mtu akisema akimwambia mzee mwenzake baada ya kuwanunulia pombe “Teta na Mungu amninge mwana shu besa” maana yake Ongea na Mungu ampe mtoto huyu pesa”.
Mimi binafsi sikatai kutoa nikiwa na hela kwa sababu kutoa ni moyo na si utajiri ila kwa kweli hela unayotafuta kwa shida alafu unaenda kumpa mtu anaponda kwenye pombe inakatisha tamaa sana. Kwa wale mnaoomba hela alafu mnaenda kuziponda hii ni kero sana achene hizo habari. .