Kuombwa Hela Kijijini

Kuombwa Hela Kijijini

Gily Gru

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
8,632
Reaction score
23,673
Mimi ni mchaga kutokea Mkuu Rombo, ila pia ni mkazi wa Dar es Salaam japo sipendi kuitwa mwanaume wa Dar.

Kuna jambo moja linanikera sana kwa kweli kila nikienda nyumbani Kilimanjaro nikikutana na wakazi wengi amabao ni ndugu au wachaga tu huwa wana tabia ya kuomba hela sana. Ukikutana na mtu asipokuomba hela basi atakuomba kapombe. Kuna siku nakumbuka kuna ndugu yangu kuona niko kwenye bodabda kaisimamisha nasema labda ananisalimia kumbe akaniambia “nipe pesa ndi umefika za motomoto kabla hazijaisha”. Siku ukiwa umeenda huna pesa unakuwa kama mwivi kazi ni kujificha migombani huko au chini ya mikahawa ili wasikuone.

Wana mbinu nyingi za kuomba pombe au pesa, ila hawaombi sukari au chakula cha watoto nyumbani. Basi nikakutana na mtu akanambia “Nikukombe kiadu” maana yake “nikulambe kiatu” akimanisha anaomba hela. Nikamnjibu “nilambe na chako pia”, yule mama alinichukia sana akawa anasema mbovu eti nilivyokuwa mdogo alinifuta mavi sasa nimekuwa nimekuwa jioni.

Kuona maneno maneno anaacha huko siku nikampa elfu mbili yule mama akashika mikono yangu akaniambia maneno matamu upate nyingi nyingi. Moja ya maneno ambayo nishawahi sikia mtu akisema akimwambia mzee mwenzake baada ya kuwanunulia pombe “Teta na Mungu amninge mwana shu besa” maana yake Ongea na Mungu ampe mtoto huyu pesa”.

Mimi binafsi sikatai kutoa nikiwa na hela kwa sababu kutoa ni moyo na si utajiri ila kwa kweli hela unayotafuta kwa shida alafu unaenda kumpa mtu anaponda kwenye pombe inakatisha tamaa sana. Kwa wale mnaoomba hela alafu mnaenda kuziponda hii ni kero sana achene hizo habari. .
 
Kuna watu nishaona ukiwapa hela wanapiga na magoti wanaimba nyimbo za kichaga na wanamtemea eti mate mazuri mikononu na usoni. Kuna jamaa alitemewa mate sana usoni kuwa anabarikiwa japo sijui kama hapo Baraka zinakuja au la. Haya mambo vijana wenzangu mnakutana nayo huko vijijini kwenu au nimeyaona mie tu????
 
"Gilbert ninga hata kabia kemu ndiakwa"...in chagas ascent

Wape hai hapo mkuu
 
"Gilbart niachie hela ya kabia kamoja"..Mambo yako naona yapo mwake..in chagas ascent

Hahaha mzee baba kama ulikuwepo aisee umenichekesha sana maana umenikumbusha mule mule
 
Gilbert ninga hata kabia kemu ndiakwa"...in chagas ascent

Wape hai hapo mkuu

Hahaha ukundi kawari ee enda oo kwa matesha ukobe ngama ngishe taa, akuninge kashori kamu

Hahahah we jamaa umenikumbusha nyumbani, mie niko Dar nitawasalimia nikienda aisee na gari ya Tilisho au Ester
 
Tatizo uwe nazo au usiwe nazo wao ni pesa tu jamanib utazani pesa zipo juu mwembe unatikisa tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Hahaha usipokuwa na pesa kijiji kizima kitajua huna pesa

Kuna jamaa aliniomba hela baada ya kushukuru na kuendelea na maisha yake, akaenda kuwaambia wenzake nao wakaja kuniomba hela. Kilichoniuma nilimsikia mmoja wao akizungmza "yule mpumbavu katupa hela leo" wakati sijawahi hata kuwakosea. Kuna mda wanaona tunaowapa hela sisi ni wajinga
 
Aisee endelea na moyo wa kutoa hivyo hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unazani unaitwaje! Ndiyo majina yao,sasa uwe hujaoa siku ukioa majukumu yameongezeka pesa hawapewi kama zamani utasikia mkewe huyo hasira zote kwa mke

Back
Top Bottom