“Kuondoa hatari” katika mchakato wa maendeleo ndilo jambo ambalo dunia inapaswa kufanya

“Kuondoa hatari” katika mchakato wa maendeleo ndilo jambo ambalo dunia inapaswa kufanya

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
WIRELESS20230714094200035AXG2B06J79.jpg


Mkutano wa 14 wa Baraza la Uchumi la Majira ya Joto uliofanyika hivi karibuni mjini Tianjin, China, umerejea katika mtindo wa nje ya mtandao baada ya kusitishwa kwa miaka mitatu kutokana na janga la COVID-19, na hivyo kuzusha matarajio mazuri kutoka pande mbalimbali.

Tofauti na Mkutano wa Majira ya Baridi wa Baraza la Uchumi unaojulikana kama “mwelekeo wa hali ya hewa ya uchumi wa dunia,” mkutano wa Baraza hilo wa Majira ya Joto unalenga zaidi katika ‘viongozi wapya.’ Kimsingi, washiriki wa mkutano huo ni pamoja na kampuni zinazoibuka duniani, na hivyo kuupa jina la ‘maua yanayochipuka ya uvumbuzi wa teknolojia’ katika majira ya joto.

Uvumbuzi na ujumuishi ni kati ya mambo maalum ya kipekee katika mkutano huo. Licha ya wasiwasi na sintofahamu kuhusu mtazamo wa uchumi wa dunia, na pia mvutano wa siasa za kijiografia unaoondoa msingi wa ushirikiano, upepo mpya unaoletwa na Baraza la Davos la Majira ya Joto utasaidia kuondoa wasiwasi huo na kutoa mwelekeo sahihi wa maendeleo ya dunia.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya Mkutano huo ni “Ujasiriamali:Nguvu ya Msukumo wa Uchumi wa Dunia,” na inaendeleza moyo wa kutafuta uvumbuzi huku ikisisitiza umuhimu wa kuchochea moyo wa uvumbuzi na uhai wa makampuni kama maajenti wakuu wa uvumbuzi katika majira ya mageuzi. Chini ya ushawishi wa mambo mbalimbali yasiyo na uhakika, kama vile mivutano ya siasa za kijiografia, nchi fulani zinatetea ‘kutengana,’ na utayari na uwezo wa kampuni zinazovuka mpaka, hususan kampuni za teknolojia ya juu, kufanya uvumbuzi, umekabiliwa na vizuizi, na hivyo kuathiri kwa kiasi fulani hali ya uchumi wa dunia nzima. Kutokana na hilo, moyo wa ujasiriamali na nguvu ya uvumbuzi vinahitajika zaidi sasa kuliko ilivyokuwa awali.

Baada ya China kutangaza kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Davos, kampuni kutoka nchi mbalimbali duniani zilijiandikisha kushiriki, na jumla ya watu 1,500 kutoka nyanja mbalimba ikiwemo wanasiasa, wafanyabiashara na wasomi kutoka nchi na sehemu 100 duniani walishiriki mkutano huo.

Kauli ya “kuondoa hatari” imepata umaarufu sana katika nchi za Magharibi, na hivyo kujenga mawazo yasiyostahili. Kadri mtu anavyokabiliwa na vurugu za siasa ya kijiografia, ndivyo anazidi kutaka ‘kuondoa hatari,’ hata hivyo, jinsi mtu anavyokuwa na nia ya kuondoa hatari, ndivyo anaweka kipaumbele kushindana na kukabiliana kuhusu maendeleo, hatimaye, kuongeza zaidi hatari.

Ukweli ni kwamba, bila maendeleo, usalama unaweza kuhakikishwa kwa njia gani? Ni kupitia ushirikiano na maendeleo, kwa kutatua migogoro katika maendeleo, na kuimarisha usalama kupitia maendeleo, ndipo dunia inaweza, tena kwa uhakika, ‘kuondoa hatari.’ Katika mchakato huu, kushikilia moyo wa ujasiriamali wa uvumbuzi, ushirikiano, uwajibikaji na kufanya kazi kwa pamoja, ni msingi muhimu wa kusuluhisha hatari hizo.

Tangu mwanzo wa mwaka huu, China imekuwa mwenyeji wa mikutano kadhaa muhimu, ikiwemo Jukwaa la Maendeleo la China, Mkutano wa Boao wa Asia, na Mkutano wa Baraza la Uchumi la Majira ya Joto uliofanyika Tianjin. Mikutano hii imepata umaarufu, na si tu kwamba imeonyesha dunia fursa kubwa katika soko la China na fursa za maendeleo, bali pia imeashiria kuwa kadri mvutano wa kisiasa duniani unavyokua, ndivyo chachu ya kutafuta ushirikiano inavyoongezeka. Dunia inavutiwa na dhana bora ya maendeleo na usalama ya China, hivyo, bila kujali kwa kiasi gani baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi na wanasiasa kuisema vibaya China, kampuni ambazo zinashiriki kiuhakika katika shughuli za kiuchumi bado zinaichagua China, na ushirikiano na China umekuwa uchaguzi muhimu sana kwa nchi nyingi za Magharibi.

Kwa kadri mivutano inavyoendelea duniani, ndivyo ilivyo muhimu zaidi kutumia kikamilifu moyo wa ujasiriamali, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, na kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga siku nzuri za baadaye.
 
Back
Top Bottom