Kuondoa Tozo kwenye Mabenki huku mkiacha kweye Miamala ya Simu, ni unyonyaji

Kuondoa Tozo kwenye Mabenki huku mkiacha kweye Miamala ya Simu, ni unyonyaji

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Nimeona Waziri wa Fedha akisema tozo kwenye mabank wameziondoa na tozo walizoziondoa ni kama zifuatazo.

(i) Tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu pande zote.

(ii) Tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja.

(iii) Tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine.

Bado najiuliza za kwenye sim kwanini wameziacha ilihali huko ndo kuna watumiaji wa hali ya chini? Nani awasemehe watu wa hali chini? Mbona mnawatenga hivo?

20220920_103259.jpg
 
Tozo iondolewe kote kote ni unyonyaji mbona vyanzo vya kupata pesa vipo vingi tu. Mfano kwenye magari kuna pesa nyingi Sana kuliko hata hizo tozo.
 
Tozo za bank zimeondolewa lini, leo tu nimepokea meseji ya makato kwenye account yangu, nimeuliza bank wanasema hawajapokea waraka wowote wa kusitisha kukata tozo, nchi ngumu hii jamani
 
Tozo ya Kutoa pesa Bank sijaona ikiongelewa popote kwenye hizo zilizoondolewa! Kwa maana nyingine hakuna namna pesa yako lazima ikatwe tozo tu kama utaamua kuitumia Cash in hand lbd uwe unalipa kieletronikale!!!

Ndg Mwl kale kamshahara kakiingia ukienda ATM nadhani bado tozo itakuhusu tu, lbd kama maelezo ya mleta mada kuna sehemu karuka!

Tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi!
 
Ok mbona sijaelewa.kuhamisha benk moj tozo hakuna.na kuhamisha bank moja kwend benk nyingine nayo hakuna
Which is which.
Nashauri.wawe pia wanaweka na makato yatakuaje ili kusud mtu anapofanya ajue.kujihamishia kutoka ac kwend line bei gan
 
Hoja yangu Kuhusu tozo itabakia pale pale kwamba tozo za banks zilipogiwa kelele kwa sababu watumiaji wakubwa ni majizi na matajiri wa mjini ila kwenye simu wanaotumia ni watu wa chini Ndio maana wamewaachia mzigo..

Majitu ya Vijijini amkeni,mnanyonywa kwa aji ya kutajitisha watu wa Mijini na nyie ndio wengi lakini hamthaminiwi..
 
Tozo za bank zimeondolewa lini, leo tu nimepokea meseji ya makato kwenye account yangu, nimeuliza bank wanasema hawajapokea waraka wowote wa kusitisha kukata tozo, nchi ngumu hii jamani
Kuanzia Oct 1
 
Tozo ya Kutoa pesa Bank sijaona ikiongelewa popote kwenye hizo zilizoondolewa! Kwa maana nyingine hakuna namna pesa yako lazima ikatwe tozo tu kama utaamua kuitumia Cash in hand lbd uwe unalipa kieletronikale!!!

Ndg Mwl kale kamshahara kakiingia ukienda ATM nadhani bado tozo itakuhusu tu, lbd kama maelezo ya mleta mada kuna sehemu karuka!

Tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi!
Nashangaa
 
Nakumbuka Makamba naye alitangaza kuifuta ile tozo ya 100/Lita ya mafuta halafu "Mama" akaibuka na kudai isiondolewe tayari hiyo pesa ipo kwenye budget.

Tusubiri atoke msibani.
 
Kwenye magari kuna pesa gani nyingi mkuu?tusaidie kutufungua macho
Ipo hivi kuna principal mpya ya kodi nimeibuni inaitwa CHEAP TO IMPORT EXPENSIVE TO MAINTAIN.

Hii principal inafanya na tabia za watu.Kwenye expensive to maintain ndipo serikali inapopata mapato yake.IPo hivi.

Serikali iruhusu magari, pikipiki,bajaji yote yaingie free bila ushuru kutokana na tabia za watz kila mtu atataka kumiliki chombo cha moto iwe ni private au ya biashara kwa sababu wengi awafahamu hesabu.

Kodi ya serikali inapatikanaje

1. Kwenye usajili wa chombo cha moto badala ya laki 5 iwe milioni moja.
2. Mafuta
3. Bima za magari hapa zipande kidogo
4. Ushuru wa parking hapa kuanzia stand za mabus na barabara za mjini
5. Fine za traffic
6. Fire
7. Spare parts hizi ushuru upande kidogo
8. Ushuru wa barabara uwepo
9. Ushuru wa Usajili wa mamlaka husika mfano latra, dawasco, tbs, misitu,nk
10. Ongezea kodi zingine.

Hoja ya ant dumping. Hii ishu haina mashiko kwa ulimwengu wa SAsa sababu ya mambo ya recycling. KWA maana hata SAsa gari chakavu zote zinaenda screpa kisha zinarejeshwa nje ya nchi kama material za kuzalisha gari zingine.

Hoja ya foleni kwamba ohoo gari zitajazana mjini na kuleta msongamano,nani kakwambia magari yote yatabakia Dar.Kama hofu ya Dar, dar kuwepo na special number ijulikane hili gari matumizi yake si nje ya Dar, mikoani huko still foleni sio tatizo, na pia foleni inatatulika kwa kuongeza miundombinu. So pesa nyingi itapatikana kwenye uendeshaji wa gari.
 
Hoja yangu Kuhusu tozo itabakia pale pale kwamba tozo za banks zilipogiwa kelele kwa sababu watumiaji wakubwa ni majizi na matajiri wa mjini ila kwenye simu wanaotumia ni watu wa chini Ndio maana wamewaachia mzigo..

Majitu ya Vijijini amkeni,mnanyonywa kwa aji ya kutajitisha watu wa Mijini na nyie ndio wengi lakini hamthaminiwi..
Pumbavu wewe acha kutuita majitu ya vijijini, acha dharau kwa kukaa mjini. Toa hoja kwa kuheshimu ambao hatujakukosea.
 
Hoja yangu Kuhusu tozo itabakia pale pale kwamba tozo za banks zilipogiwa kelele kwa sababu watumiaji wakubwa ni majizi na matajiri wa mjini ila kwenye simu wanaotumia ni watu wa chini Ndio maana wamewaachia mzigo..

Majitu ya Vijijini amkeni,mnanyonywa kwa aji ya kutajitisha watu wa Mijini na nyie ndio wengi lakini hamthaminiwi..
Ila wewe uchawa wako una kudhalilisha sana!

Si ni wewe ulikuwa unakata viuno humu kushabikia tozo?
 
"Wananchi wameikubali Tozo" Raisi Samia

"Tozo ni pendekezo la wananchi" Mwigulu
 
Back
Top Bottom