Kuondoa Tozo kwenye Mabenki huku mkiacha kweye Miamala ya Simu, ni unyonyaji

Kuondoa Tozo kwenye Mabenki huku mkiacha kweye Miamala ya Simu, ni unyonyaji

Tozo ya Kutoa pesa Bank sijaona ikiongelewa popote kwenye hizo zilizoondolewa! Kwa maana nyingine hakuna namna pesa yako lazima ikatwe tozo tu kama utaamua kuitumia Cash in hand lbd uwe unalipa kieletronikale!!!

Ndg Mwl kale kamshahara kakiingia ukienda ATM nadhani bado tozo itakuhusu tu, lbd kama maelezo ya mleta mada kuna sehemu karuka!

Tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi!
Tulipe kodi kwa maendeleo ya Mwigulu.
 
Nilitaka kulipia control number ya mgonjwa wangu Muhimbili hapa kwa simu, nikaona Makato (tozo) ilikuwa 7,000,,,

Nimaamua kuingia kwa wakala kuilipia, nimelipia gharama ya bili tu nimeomoa elfu 7 ya tozo.

Hebu fikiria, elfu 7 si ni nauli ya kunileta Muhimbili kumwona mgonjwa siku mbili ambayo ningekatwa kwenye tozo?

Me nashauri badala ya kuendelea kupigizana makelele na serikali, watu ni kupunguza kufanya miamala ya tozo kwa kadiri ya tunavyoweza, kama kulipia hizi control number kwenye simu, makato ni makubwa nenda kalipie kwa wakala ni bure.

Kumtumia mtu hela, usiweke kwenye simu yako, nenda kwa wakala unayemuamini atume direct uokoe makato kwako,,, me situmii mtu hela tena siku hizi, narusha kwa wakala direct.

Bank utapita mshahara tu, vile vihela vyangu vya biashara nilivyokuwa naviweka bank, nitaziweka tu nyumbani isiwe shida
 
Back
Top Bottom