Kuondoka kwa Harmonize WCB tutegemee Mwisho wa Ali Kiba?

Kuondoka kwa Harmonize WCB tutegemee Mwisho wa Ali Kiba?

Wanajua kabsa mbwa kupanda juu n shuhuli pevu
Mkataba wake na WCB ulikuwa wa miaka 15 na masharti kibao. Tuombe Mungu avuke kizingiti hicho. Ndio maana mameneja wa WCB wanacheeeeeeeka
 
nyimbo za mwana, chekecha, kadogo zote zili hit na ametoa kipindi ambacho kila mmoja anajua ashakufa kimuziki

hoja yangu ni kuwa kama Diamond yuko juu, hawezi kamwe kushindana na Kiba

Kiba katulia na hana papara anaweza kukaa hata miaka minne na akatoa wimbo na ukafanya vizuri.Diamond hajawahi pitia hii test ya kukaa more than three years kisha aje atoe wimbo

Kuwa nani ana viewers wengi ni Diamond, nani anajaza kumbi diamond'

Kiba yuko moderate na washabiki wake ni royal hawasukumwi kwa upepo wa msimu, ukiangalia shows za kadogo Live utaona nilichoandika

so Kiba he is there to stay!!! hata kama kwa mezi nane hatasikika, akitoa atasikika na hafi

hii ni reality
viewers walikua wangapi??
 
Kiba ameshapotea zamani tu,amebaki kupiga picha na sinia za pilau
 
Ni siku chache zijazo, tutaanza kuzisikiliza nyimbo za Harmonize bila kibwagizo cha ‘Wasafi Records’ na ‘Eyo Laiza’. Mwanamuziki huyo, ambaye jina lake halisi ni Rajab Abdul Kahali ameandika barua ya kujitoa katika lebo ya Wasafi Records.
Msanii huyo ambaye nyimbo zake za ‘Kwangalu’ na ‘Show Me’ zimeleta gumzo nchini, bila shaka ataleta upinzani mkubwa kwa wasanii wa lebo hiyo akiwamo Diamond mwenyewe.
Kwa sababu Harmonize ameishi WCB, anajua nguvu yao, anajua udhaifu wao, anajua sehemu ya kupita na kufanya vitu vya tofauti.
Licha ya watu wengi kudhani kuwa WCB itatetereka, hali haiwezi kuwa hivyo kwa sababu Diamond na wenzake wataamka na kufanya vitu vya tofauti zaidi wakijua sasa wapo katika mapambano halisi.
Hilo haliwezi kukwepeka kwa sasa kwamba Diamond atajipanga zaidi kwa sababu katika akili yake anajua kuwa Harmonize anakwenda kuwa mpinzani wa kweli tofauti na Ali Kiba, ambaye upinzani wake umetengenezwa zaidi na mashabiki.
Ushindani huo unaweza ukampoteza kwa muda Ali Kiba, ambaye mashabiki wamekuwa wakilazimisha ili aonekane kuwa mpinzani wa Diamond.
Utajiuliza kwanini mashabiki wanalazimisha? Hoja hapa ni kuwa unamlinganishaje msanii ambaye kwa mwaka anatoa nyimbo zaidi ya 10 na mwingine ambaye anatoa wimbo mmoja.
Ni rahisi kutetea kuwa idadi haijalishi, lakini ni ukweli kuwa Diamond anafanya muziki kibiashara tofauti na Ali Kiba, ambaye kwa kiasi kikubwa anafanya kama ‘kujifurahisha zaidi’. Bila shaka mashabiki wa Ali Kiba na wale wanaomchukia Diamond, kwa muda fulani watashangilia chochote kinachofanywa na Harmonize na kila wimbo wa msanii huyo utapendwa na kundi hilo la mashabiki bila kujali kiwango chake.
Kwa namna fulani jambo hilo linaweza kufanya ushindani wa Diamond na Harmonize kuwa mkali kwa muda fulani na hasa itategemeana na jinsi Harmonize atakavyoondoka WCB kama ni kwa shari au kwa amani.
Kwa vyovyole vile, upinzani wa Diamond na Harmonize unaweza kufunika nyota ya Ali Kiba kama akishindwa kucheza karata zake vizuri.

Copy n Paste from
mwananchi Official IG
Nyimbo 10 vs wimbo 1...QUALITY VS QUANTITY over.
 
200% true.
Alikiba aliishi kwa hisani ya wasiopenda maendeleo ya Diamond, nao sasa watahamishia majeshi kwa Harmonize
Ikumbukwe aliwepo kabla ya diamond ndo mtuambie sasa kipindi hicho alishabikiwa na wasiompenda nani?
 
Ali hawezi shindana na Mond, wala harmonize walioshindana nae wote hapo awali hawapo wamepotea

why?

Kiba hatoi back to back!..anaweza akakaa miaka miwili akatoa hit song kisha akapotea!!...kujua anafanya nini ana uwezo gani ni ngumu, huyu wataisha akina Mond na wote mnaowajua yeye atabaki!'

Kama mtaishi maisha marefu, Kiba atatoa nyimbo mpaka uzeeni..iko damuni, na hana mzuka wa kushindana na mtu

Kwa hiyo uko sahihi, Kiba yuko level zingine, miziki mingine, vision tofauti na hao

Hata miaka sita anaweza kukaa kimya, siku akitoa anafuta zingine kwa muda na anakuwa kama "yuko kila siku kwenye game"
Kah Ahsantee umekata kiu yangu.
 
Back
Top Bottom