Kuongea kwa kuchanganya lugha kiswahili na Kiingereza, ni usomi au ujanja?

Ni sawa na sio sawa. Kwa harak haraka mkuu Artificial Intelligence kuiita akili mnemba inataka mazoea. Sababu hata nikiambiwa tunga sentensi mbili kwa kutumia neno mnemba, sijui vizuri maana ya mneba.

Inawezekana mtu alikosa msamiati, au hana uwezo wa kulielezea suala hilo kwa kiswahili. kingie ni sanaa ya mtu katika kutumia lugha.

hata katika kiswahili tupu kila mtu ana machaguzi ya kipekee ya misamiati. Mfano NIPO KWENYE daladala. Mwingine NIKO KATIKA daladala, mwingine anatumia NIKO KWENYE, au NIPO.

Mfano mashine unataka kusema iko STAND BY, useme iko tayari kwa kuanza kazi, maneno yanakuwa mengi. Kama ni katika maongezi na watu wanaweza kuelewana sioni tabu sana. Pia inakusaidia kujua mtu unaeongea nae kama ni tapeli, mjinga na kadhalika.

Mfano mtu anakwambia yeye ni daktari halafu anasema jamaa nikamfanyia blood transmission akatoka salama, na wewe labda ni mtu wa fani hiyo unajua alitakiwa aseme blood transmission. So kama ni mtu mpya unaanza kujua unawasiliana na mtu wa aina gani, unawasha dta ya umakini.

Ilakuna wale pia wa kutafuta jambo fulani la kisifa sifa eneo husika, unawavumilia mkuu, maisha ni sayansi na sanaa na upande wa sanaa kila mtu anabuni njia zake afikie lengo.

Mfano unaongelea mpira unaweza kujikuta unawaambia watu tactical na technique, pass na pace ambayo kwa kiswahili unaweza kujikuta tactical na technique umeyaweka sehemu muha , na pace ukafanya tuhisi ni pass.
 
Mimi ni msafwa. Kisafwa changu huwa kina maneno mengi ya kiswahili. Ninaamini kuchanganya lugha ni hulka inayojileta tu kwa ajuaye lugha zaidi ya moja.
 
leo dada uwepo wako mama ni kama upepo hauonekani ila unafeel ubaridi,wewe una like tu unapita hivi mama siku hizi umeachagua kuwa mkimya hivi 🤩 nani amemkasirisha dada yangu🙃
 
hiyo inaitwa code mixing au code switching ungepita form5 usingeuliza ngoja nikupe sababu ya hiyo kitu
1. ufahari wa mtu kuongea hivyo yaani sifa ajulikane amesoma au anajua
2. uhaba wa misamiati mf kswhl tunaupungufu wa misamiati
3. wengine tabia yao tu
4. kusisitizia jambo flani au mkazo mfano akipga kswhl akaweka English anaonekan kweli amemaanisha
5. Wengine wana umahiri wa lugha zaidi ya Moja kwahy siyo shida zao kuswitch
 
Ni uelewa
 
Lugha ni chombo cha mawasiliano, na lugha inakua, inaiba maneno kutoka lugha mbalimbali.Ushishangae sentensi - I gurantee you...itakuwa inamaana ya kwishwahili - kugarantii
 
Yaani usome Kwa lugha ya Kiswahili miaka 7. Uje usome Kwa English miaka takribani 4,6 au 9 halafu kwenye kuongea uongee pure Swahili au pure English. Ukiweza unastahili tuzo!
 
Ni uharibifu wa hizo lugha mbili..Ulimbukeni wa lugha ya kigeni ili jamii ijue kuwa shule ipo kichwani sio bogazi..lakini, wakati mwingine huyo mtu anaweza akawa hzo lugha zinampiga chenga yaani hazijui vizuri ndomaana anazichanganya kwa pamoja kuunganisha sentensi..au lugha moja anaifaham vizuri nyingine anapapasa.
 
Kawaida tu. Kuna wakati mtu anakosa neno la kiswahili linalofit vizuri kwenye hiyo scenario ☺️☺️☺️ nimefanya yaleyale. Ila kufanya hivyo kwa watu ambao unajua kabisa hawatakuelewa pia ni ukosefu wa akili
 
Dhima kuu ya mawasiliano ni kupashana habari.

Kama ujumbe unafika wala hakuna shida yoyote hata mngesema muwe mnawasiliana kwa ishara tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…