Kuongea mwenyewe ni tatizo au ni kawaida?

Kuongea mwenyewe ni tatizo au ni kawaida?

Ukiona dalili hizi fika kituo cha afya ya akili haraka!

Denis Mpagaze
__________________

Unajua siku hizi unaweza kukutana na mtu kavaa suti usijue hadi akianza kuongea ndo unasema alaaa, kumbe tuko na mwehu halafu hamsemi😄😄!!

Kwahiyo ukiona haya yanakutokea kimbia chapu hospitali ukatibiwe kabla hujaharibu sana!

1. Kuwa na mawazo sana lakini hujui unawaza nini hasa! Halafu mawazo yanashindana kichwani.

2. Kuwa na furaha iliyopitiliza. Muda wote unatabasamu! Kitu kidogo unacheeeeka mpaka unakaa chini! Ukiulizwa unacheka nini huna jibu!

3. Kuwa mpoleee na mkimya kupitiliza. Hata ukiwa na watu uko kimyaaa kama bubu. Unageuza geuza macho tu kama kinyonga maskini ya Mungu. Kapate tiba!

4. Unalala sanaa! Unaingia kitandani saa mbili usiku, hata kula unaona uvivu, unaamka kesho yake saa sita mchana na bado una usingizi😄

5. Kuwa msahaulifu kupitiliza. Yaani ukiweka kitu sehemu hukumbuki. Yaani kila ukitaka kuondoka hukumbuki uliweka wapi funguo! Unatafuta mpaka una sala!

6. Kutokuwa na utulivu katika kutenda. Unaanza kupika mara unaacha, unaenda kufua unaacha, unaenda kulala, unaamka unaangalia TV, programu haijaisha umeshika simu!

7. Umejaa hofu ya kila kitu. Hujiamini. Huna kosa lakini unajiona mwenye hatia! Unamuoga kila mtu.

8. Unatamani mtu akuchokoze umnase kibao ili ufurahi. Asipokuchokoza unaumiaaa! Nenda hospitali.

9. Unatabia ya kufanya kitu ambacho hujatarajia kukifanya na baadaye unajilaumu na kuapa hutorudia. Halafu unarudia tena!

10. Unapewa muda wa kusalimia, unahutubia, muda, unapewa kuhubiri, unahubiri hadi watu wanasinzia, ukipewa nafasi unaongea hadi kushindwa kufanya majukumu mengine.

11. Unapenda kesi kweli. Jambo dogo unampeleka mtu polisi! Unaomba mtu akuguse ukamfunge!

12. Hupendi kufuata sheria hata siku moja. Unaendesha gari kwa speed kubwa pasiporuhusu speed kubwa.

13. Kukasirika sana kwa jambo dogo sana, na hivyo kuanzisha ugomvi.
 
Back
Top Bottom