Kuna watu wana stigma katika hili. Huwa naongea mwenyewe, na niko kwenye mid 20s wala sio uzee sijui kuchoka maisha. Sababu muda mwingi siongei na watu endapo hatuendani vitu tunapendelea. Sipendi mpira, mieleka, matamasha, mazishi au sehemu yoyote yenye watu wengi naona kama kuna gaidi atalipua bomu hapo au mtakanyagana mfano kama ni uwanjani. Hata sehemu zangu za kutulia ni kwenye watu wachache sana.
Wasio na akili kabisa wala kuelewa mambo kidogo wanaishi kwa raha maana hawaumizi vichwa. Ila wenye akili kiasi inabidi wajadili, sasa kama huongei na mtu unaongelea ndani kwako ni hatari. Bora ujadili mwenyewe kwa sauti, ujiulize na kujijibu, ujihoji na kutengeneza debate mwenyewe. Tofauti na hapo kuna kitu unakifungia ndani na kitakupa matokeo kwenye magonjwa ya moyo.
Unahisi Isaac Newton alivyogundua gravity aliongea na nani? Alijiuliza mwenyewe alipoangukiwa na tufaa.
Au Archimedes mpaka anagundua Archimedes' Principle akiwa anaoga kwamba alikuwa na mtu wanaulizana. Hadi alikosa wa kuongea nae akakimbia uchi anashangilia amegundua kitu.
Watu wanaoongea peke yao naturally kwa kiasi na kwa mpangilio (sio wenye stress) huwa wana IQ kubwa kidogo.