Kuongeza Mwili: Muongozo wa Mazoezi na lishe (Gym workout & Diet)

Ngoja kwanza Anord schwarzenegger amefariki??
 
Doctor alikua sahihi, ukitaka kupunguza kitambi haimaanishi ufanye mazoezi ya tumbo hapana. Inabidi ufanya mazoezi ya aerobics na kuzingatia diet. Eventually, mwili kwa ujumla utapungua, ikiwepo kitambi.
Wanawake wengi hawataki kupunguza mwili unakuta anataka atowe tumbo tu.na wengi wa hivi hawawezagi mazoezi je mkanda unaweza punguza tumbo ili siku nikipata kitambi nijifungie zangu mkanda
 
Umeongea ukweli kabisa
Nidhamu ya kula nalo ni neno kabisa.
Wanasema :

Eat Less. More Exercise

Hiyo ni principal ya kupungua hata uwe kibonge vipi. Usipopungua Basi kuna mkono wa mtu.

Mtu anafanya mazoezi anaenda kula kilo tatu ya wali hahaha.

Mimi nafanya mazoezi ya kukimbia asubuhi na jioni kwenye uwanja karibu na ninapoishi. Nimekata kilo 18 kwa kukimbia tu bila zoezi lolote kwa Kipindi Cha miezi 6.
 
Mkuu, kwanza kabisa nianze kwa kukupongeza kwa kuleta uzi mzuri na wenye lengo la kujenga. Kwa ujumla umegusia mambo ya msingi ingawa kuna machache ambayo ningependa kuyaongelea.

Kwanza: kwenye Mazoezi ya free weights kuna goals tatu i.e Strength, Hypertrophy na Endurance.

1. Strength/nguvu: Ili uweze kujenga nguvu, inabidi uweke plate nzito ambazo utaweza kunyanyua mara 3-5 tu (i.e rep range of 3-5)
2. Hypertrophy/kujenga misuli: Ili kuweza kumaximize kujenga misuli inabidi uweke uzito ambao utaweza kunyanyua mara 8-12 i.e rep range of 8-12).
3. Endurance/uvumilivu: ili kujenga au kuwa na misuli stamilivu inabidi uwe unatumia uzito utakaoweza kuunyanyua mara 15 na kuendelea (i.e 15+ rep range).

Pili: Umesema mazoezi muhimu ni mawili TU, ya mikono na kifua.

Mwili wa binadamu una musce groups kadhaa mfano kifua, mabega, mikono, mgongo, miguu (quads, hamstring, glutes), tumbo n.k. Watu wengi wanapoanza gym hua wanafanya mazoezi ya misuli inayoonekana wakijitazama kwenye kioo mfano kifua na mikono. Matokeo yake wanakua juu wakubwa ila chini wadogo, wazungu wanaita chicken legs. Hakikisha unafanya mazoezi ya miguu, mgongo, mabega sambamba na kifua na mikono. Ili kuwa na muonekano uliobalance ni lazima ufanye mazoezi ya mwili mzima.

Tatu: kwa mtu anayeanza gym, kwa wiki anatakiwa afanye mazoezi angalau mara 3. Katika hizi siku unafanya mazeoezi ya mwili mzima (all muscle groups).

Nne: Kunyanyua kilo nzito kwa reps chache hakufanyi mtu akomae/akauke/adumae. Sana sana inaomungezea nguvu

Mambo ambayo ningependa kuyatilia mkazo:

1. ili kujenga misuli ni lazima ufanye mazoezi kustimulate muscle growth, then ule protini ili iende kujenga misuli na mwisho upumzike/ulale angalau 8hrs.

2. Ili kuondokana na wembamba hakikisha unakula SANA chakula. Lengo ni ili mwili uwe kwenye caloric surplus. kula vyakula vyote iwe junk kama pizza burger, ugali wali etc. Kwa sababu wewe ni mwembamba, unahitaji calories nyingi.

Update
3
. Kama una kitambi na unataka kukipunguza bila ya kupunguza makalio au hips, bahati mbaya hilo haiwezekani. Na pia hakuna mazoezi yoyote maalumu ambayo ukiyafanya yanapunguza ONLY kitambi. Kupunguza kitambi, fanya mazoezi ya mwili mzima i.e aerobics, ila chamsingi zaidi ni msosi. Fanya diet, hakikisha mwili upo kwenye "Caloric deficit" utapungua mwili mzima including kitambi.

4. Kwa wale wenye wasiwasi wa kupoteza makalio/glutes endapo wakipunguza mwili/kitambi, kuna mazoezi ya kujenga Glutes mfano squats, lunges, horse kick back, Hip thrusts n.k.

 
Aisee nimejiandikisha gym jana maana mazoezi ya ghetto hayanipi mwitikio nakosa kampani. Watu wote hawafanyi mazoezi hafu kuna watoto wa kike hapa hivo nilikuwa navizia usiku wa manane. Sasa tangu leo nitaamka asubuhi mapema naingia gym kama dakika 40 kisha najiandaa na ratiba ya masomo.

Leo nimepiga kidogo tu mikono imelegea. Mimi ni mtu niliyekuwa very negative na mazoezi, nimeenda ili niongeze uzito kiafya. Bajeti ya chakula nimetenga kuanzia leo nitaongeza chakula. Miaka kama minne sasa nakula mlo mmoja kwa siku, nimeacha. Nilipopiga leo nikahisi njaa jambo lisilo la kawaida.

Sema kuna influence kama hii
 
Kumbe wewe mwana jogging mwenzangu[emoji23]
Jogging nzuri kimsingi changamoto za maisha zinfanya tusiwe huru ila nikiwa kwenye form mlolongo wangu unakuwa kama hivi

1)Free Weight Workout: Najaza misuli kwanza na nguvu (Body Power).
2)Body Weight Workout: Kwaajiri ya kuumiliki mwili (Body Strength).
3)Jogging & Jumping Rope: Kwajiri ya kujenga punzi.
4)Yoga: Kwaajiri ya kunyoosha, kuimarisha na kufanya misuli, mifupa na mwili kuwa imara (flexible).

Ukifanya Package nzima hii you will be unstoppable.
 
Safi kabisa mkuu
 
Unafanya haya mazoezi ndani ya siku moja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…