Mkuu, kwanza kabisa nianze kwa kukupongeza kwa kuleta uzi mzuri na wenye lengo la kujenga. Kwa ujumla umegusia mambo ya msingi ingawa kuna machache ambayo ningependa kuyaongelea.
Kwanza: kwenye Mazoezi ya free weights kuna goals tatu i.e Strength, Hypertrophy na Endurance.
1. Strength/nguvu: Ili uweze kujenga nguvu, inabidi uweke plate nzito ambazo utaweza kunyanyua mara 3-5 tu (i.e rep range of 3-5)
2. Hypertrophy/kujenga misuli: Ili kuweza kumaximize kujenga misuli inabidi uweke uzito ambao utaweza kunyanyua mara 8-12 i.e rep range of 8-12).
3. Endurance/uvumilivu: ili kujenga au kuwa na misuli stamilivu inabidi uwe unatumia uzito utakaoweza kuunyanyua mara 15 na kuendelea (i.e 15+ rep range).
Pili: Umesema mazoezi muhimu ni mawili TU, ya mikono na kifua.
Mwili wa binadamu una musce groups kadhaa mfano kifua, mabega, mikono, mgongo, miguu (quads, hamstring, glutes), tumbo n.k. Watu wengi wanapoanza gym hua wanafanya mazoezi ya misuli inayoonekana wakijitazama kwenye kioo mfano kifua na mikono. Matokeo yake wanakua juu wakubwa ila chini wadogo, wazungu wanaita chicken legs. Hakikisha unafanya mazoezi ya miguu, mgongo, mabega sambamba na kifua na mikono. Ili kuwa na muonekano uliobalance ni lazima ufanye mazoezi ya mwili mzima.
Tatu: kwa mtu anayeanza gym, kwa wiki anatakiwa afanye mazoezi angalau mara 3. Katika hizi siku unafanya mazeoezi ya mwili mzima (all muscle groups).
Nne: Kunyanyua kilo nzito kwa reps chache hakufanyi mtu akomae/akauke/adumae. Sana sana inaomungezea nguvu
Mambo ambayo ningependa kuyatilia mkazo:
1. ili kujenga misuli ni lazima ufanye mazoezi kustimulate muscle growth, then ule protini ili iende kujenga misuli na mwisho upumzike/ulale angalau 8hrs.
2. Ili kuondokana na wembamba hakikisha unakula SANA chakula. Lengo ni ili mwili uwe kwenye caloric surplus. kula vyakula vyote iwe junk kama pizza burger, ugali wali etc. Kwa sababu wewe ni mwembamba, unahitaji calories nyingi.