Kuongeza ufanisi wa pc kwa bajeti, Je ninunue SSD GB 128 kwajili ya windows kisha niigeuze hdd ya 1 tb kwajili ya storage au ni lazima iwe 1TB SSD ?

Soko la Nand lime crash, wame produce Nyingi kuliko Mahitaji, kampuni Zote Sk Hynx, Micron na Samsung zimepata matrilioni ya Hasara, ssd sasa hivi zinauzwa kama Karanga.

Even Highend Ssd zenye speed 3.5GBps kupanda kama Samsung 970 Evo plus, 980 unazipata around $50. Crucial p3 plus (5GBps), Western Digital black na Blue mpaka 5.1GBps zote hizi ni $50 ama chini ya hapo.

Zile brand ndogo ndogo zenye speed chini ya 3.5GBps na endurance ndogo zimeshuka hadi around $30.

Hadi Intel ambaye ssd zake ni bei ndefu bei humo humo unapata 2TB kwa $60-70.
 
Anyway labda mwalimu wangu hakunifundisha vizuri


1. SSD itakupa speed kwenye booting tu kuwaka haraka kwa sababu ya kasi ya speed ya SSD kwenye kusoma OS Files.

2. Kuna vitu kwenye PC vitategemeana yule mwalimu alitumia maneno kama


RAM ni eneo au uwanja ambapo kazi zote zinapofanyikia temporary

HDD Hii ikiwa umefanyiwa formatting vizuri kwa kutumia system files za NTFS au now days HPFS na ukafanya Pertition then haina nafasi kwenye kuifanya PC iwe slow

Processor Yenye clock speeds, Performance-cores and Efficient-cores nzuri

SO cheza na RAM tu hapo wengine wataelewana
 
Mkuu, unaweza kusaidia kurecommend specifications za ssd nzuri, kama ikiwezekana pia na brand, manake sokoni zimekuwa nyingi tofauti tofauti zinachanganya kama hauna utaalam nazo.
 
Mkuu, unaweza kusaidia kurecommend specifications za ssd nzuri, kama ikiwezekana pia na brand, manake sokoni zimekuwa nyingi tofauti tofauti zinachanganya kama hauna utaalam nazo.
Siku hizi Mainly zipo aina mbili,

Sata ssd na Pcie (Nvme ssd aka m2)

Sata ssd ni kama hdd za kawaida umbo lake hizi zinaingia machine yoyote ya sata, mpaka Computer za miaka 10 ama 20 iliopita zinakubali, kutokana na Connector ya Sata (6gbps) hizi huwa speed yake inakuwa around 500MB/S

Kama una computer ya kizamani huna ujanja ssd ni hii tu.

Kama una computer ya kisasa inayoingia m2 ssd hapa ndio inabidi uwe makini kidogo

1. Size
Kikawaida size za m2 ssd kwenye laptop ni 2280 ila kuna vifaa kama laptop nyembamba ama Tablets ama handheld kama Steam deck wanatumia vi m2 ssd vidogo vya 2230.



2. Gen ya Pcie.
Juu tumeona sata ssd hazina speed sababu ya Connector, kwenye pcie ssd pia generation ya pcie inaamua ssd yako iwe na speed kiasi gani
-pcie gen 3 ina lane 4 kwenye m2 na kila lane ni kama 1GBps hivyo in theory utapata kama 4GBps speed ndio maana ssd zake nyingi zinakuwa 3.5GBps.
-pcie gen 4 kila lane ni GBps kwa lane 4 inakuja kama 8GBps ndio maana ssd nyingi zake ni 5-7GBps.


Ila nisikutishe sana most of time kwenye Nvme watu wananunua m2 2280 pcie gen 3 hizo za 3.5GBps.

Kama huna uhakika ukipost model nitakusaidia aina ya ssd inayotumia.
 
Habari ya uzima wana jamii forum
Naomba msaada juu ya mchanganuo wa kufungua library classic ya HD/4K ipoje na imekaajee soko lake kwasasa ...

1.maitaji kiujumla
2.faida na hasra(changamoto)
3.ushauri na maoni yanapokelewa

Plz n plz naomba msaada wenu
 
No need
Kuna malicious za kutosha tu. Kama unaitumia akwenye internet futa tem files zote but ukiona ngumu basi fanya backup na format mashine itarudia speed yake. Kwa ram 8gb ni kubwa inatosha sana tu, 1tb pia iko sawa huna haja uingie gjarama kununua ssd hdd
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…