Aloyce Dedu
New Member
- May 19, 2024
- 2
- 1
UTANGULIZI
Data au Taarifa ni kiini cha maendeleo katika taifa. Taifa lililoendelea na linaloendelea hutegemea data (taarifa), namna nchi inavyokusanya taarifa,kuzihifadhi,kuzichakata na kupata matokeo ya data hizo ndiyo imekua tofauti kubwa kati ya Mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea.
Tumeshuhudia nchini Tanzania kumekuwa na maendeleo makubwa ya mifumo ya tehama kwa kipindi cha hivi karibuni, ingawaje kumekuwa na changamoto kadhaa katika mifumo hii Lakini jambo jema ni kuwa tunaendelea vizuri kwakuwa changamoto ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko.
HALI YA SASA KATIKA MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHEMA
Ingawaje ukusanyaji wa data sahihi umekua ni changamoto nchini Tanzania lakini
kwa sasa kumekua na matumizi mazuri ya tehama na yanaleta faraja kwa maendeleo ya taifa mfano hospitali za rufaa zimekua zikitumia mifumo ya tehema kama vile (GotHoms,AfyaCare na n.k), upande wa elimu kumekua na mifumo ya (ess n.k) pia maombi ya ajira yamerahisishwa kwa uwepo wa ajira portal n.k, kwa ujumla kumekuwa na matumizi ya mifumo ya tehama katika halmshauri na sekta mbali mbali za kiserikali na binafsi.
CHANGAMOTO YA HALI YA SASA KATIKA MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHEMA
1. Baadhi ya mifumo ya tehama haipo 'active' mfano mifumo mingi ya halmshauri machapisho yake ni ya muda mrefu hivyo inawanyima wananchi taarifa sahihi kwa wakati husika.
2. Ukosefu wa mifumo na maafisa wa tehema kwa ngazi za kata,kwani uwepo wao ungesaidia kutunza kumbu kumbu za miradi na shughuli nyinginezo za kata hivyo kurahisisha uwepo wa taarifa sahihi.
3. Ukosefu wa maafisa tehama mashuleni hali hii imesababisha taarifa nyingi za wanafunzi kutohifadhiwa kwani kumbukumbu pekee zilizopo ni za kitaaluma lakini tabia,afya n.k kumbukumbu hizi hupotea.
4. Uhaba wa watumishi kusimamia mifumo ya tehama hali iliyopelekea uwepo wa taarifa siziso sahihi mfano ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali imeonesha namna mifumo ya tehama ilivyofanya mihamara isiyohakikiwa.
5. Uelewa wa wananchi katika kutumia mifumo ya tehama pia uelewa mdogo wa wananchi wa jinsi ya kutumia mifumo hii ya tehama imekua changamoto kubwa zaidi na kupelekea kulalamikia mifumo pasipo kujua inafanyaje kazi hivyo inawanyima taarifa.
NINI KIFANYIKE KUBORESHA HALI ILIYIPO KUFIKIA TANZANIA TUITAKAYO KATIKA KUONGEZA WIGO WA MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHAMA.
1. Mifumo iliyopo iongezewe uwezo na iwe 'active' hasa mifumo ya halmshauri na baadhi ya taasisi ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wananchi.
2. Uwepo wa mifumo ya kata pamoja na maafisa tehama wa kata ambao watashirikiana na watendaji wa kata pamoja na watumishi wengine dani ya kata ili kutunza kumbukumbu za miradi na shughuli nyinginezo ndani ya kata husika, hii itarahisisha uwepo wa taarifa bila kupotea.
3. Kuwepo na maafisa tehama mashuleni hii itasaidia kuwepo wa kumbukumbu za wanafunzi sio tu kitaaluma lakini kiafya,kitabia, n.k kumbukumbu hizi zitarahisiha teuzi na uchaguzi wa viongozi wanaofahamika sio tu kitaaluma bali kiafya na kitabia, hii imetokana na uwepo wa viongozi na watumishi wengi wasio na maadili mema na sababu kubwa ni baadhi ya data zao hazifahamiki hasa kwa ngazi ya elimu ya msingi na sekondari.
4. Uwepo wa maafisa wa tehama wenye sifa watachochea usimamizi mzuri wa mifumo ya tehama na hivyo kudhibiti upotevu wa taarifa muhimu.
5. Wananchi wapatiwe elimu kupitia maafisa tehama wa kata hii itarahisisha na kuchochea uelewa kwa wananchi kwa ajili ya mikakati ya mbele ya serikali kuamia kwenye mtandao(digital government).
HITIMISHO
Uwepo wa data sahihi kwa ngazi ya chini ndiyo msingi wa maamuzi sahihi kwa viongozi, ambao huleta maendeleo chanya kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
ZINGATIA
Neno data= taarifa.

Upvote
6