Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Huu mtindo wa wafanyabiashara wa migahawa, bar na vyoo vya umma kuchukua sabuni ya maji halafu kuiongezea maji ili iwe nyingi ni upumbavu wa hali juu. Wabongo kuna ujanja mwingine tungeachana nao tu maana tunakuwa duni kuliko hata ngedere, kama ni ubahili wa kubana matumizi basi pia ni ubahili wa kipumbavu.
Sabuni huwa zinatengenezwa kwa kanuni/formula maalumu ili ziweze kuondoa uchafu na kuua vijidudu, kuongeza maji ila chupa moja itoe chupa tatu ni kupoteza kabisa maana ya formula iliyotumika na hiyo inakuwa sio sabuni tena bali ushahidi wa sabuni tu.