Kuongezeka kwa bei ya mafuta nchini kunatokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia na siyo kosa la serikali ya Rais Samia

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2012
Posts
3,139
Reaction score
2,488
KUONGEZEKA KWA BEI YA MAFUTA YA PETROL NA DIESEL KUMESABABISHWA NA ONGEZEKO LA BEI KTK SOKO LA DUNIA NA SIYO KOSA LA RAIS SAMIA.

Hapo jana serikali imetangaza bei mpya ya mafuta ya bei ya petroli na diesel ambapo kwa hapa Tanzania bei inatarajiwa kuanzia leo kuwa kati ya sh 2700-3000

Kuna watu wengi hutumia mwanya wa ongezeko la bei ya mafuta kuwa ni uzembe wa Rais Samia na wengine wamekwenda mbali kwa kusema kuwa angekuwepo Magufuli (R.I.P) BEI ISINGEPANDA; Huu ni upotoshaji na uchonganishi usiokuwa na tija kwa Taifa letu. Rais Magufuli amefanya kazi kubwa sana ktk nchi yetu lakini siyo sahihi kusema angekuwepo yeye bei ya mafuta isingekuwa kubwa ilihali kiuhalisia bei ya mafuta haijapanda ktk soko la ndani baki ktk soko la dunia ambapo kwa namna yoyote athari za bei lazima uzipate kwa kuwa sisi siyo wazalishaji wa mafuta hayo

Linapokuja suala la mabadiliko ya bei ya mafuta ktk soko la dunia bei hiyo hubadilika ktk nchi zote na tunaoumia hasa ni nchi ambazo hazizalishi mafuta ikiwemo Tanzania.

Bahati nzuri ktk ukanda wa Afrika Mashariki licha ya bei ya mafuta kupanda ktk soko la dunia lakini bei yetu ni nafuu kuliko nchi zingine za afrika mashariki kama Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Kwa wale wanaoamini kuwa Magufuli angekuwepo bei ya mafuta isingepanda naomba niwakumbushe kidogo.

Kipind Magufuli anaapishwa 2015, TZ bei ya petroli ilikuwa 1900-2000/litre ambapo bei ya mafuta duniani ilikiwa ni $40 kwa pipa.

Mpaka anafariki 2021, aliacha mafuta yakiuzwa 2400-2500/-. Leo hii pipa la mafuta katiķa soko la dunia ni hadi $140 na Tanzania yakiuzwa kati ya 2700-3000 kwa lita.

Ikumbukwe kuwa bei imeongezeka karibu mara mbili ya bei ya mwaka 2020 na karibu mara tatu ya bei ya mwaka 2015 lakini serikali imejitahidi kudhibiti mfumuko wa bei ya mafuta.

Uwezo wa serikali yetu ni kudhibiti mfumuko wa soko la ndani liendane na soko la dunia lakini si rahisi kudhibiti bei tofauti na ile inayouzwa ktk soko la dunia

Aidha tunaweza kulaumu tu kama bei ya mafuta nchini ikiwa kubwa kuliko nchi zingine au kuliko ktk soko la dunia.

Njia pekee ya kuweza kukabiliana na makali ya bei ni kwa serikali kutoa fedha ya ruzuku kwa wafanyabiashara ili kuuza bei rafiki (mfumo huu ni wa gharama ambao unategemeana na bajeti na uwezo wa serikali kifedha)

Tumeshuhudia nchini Kenya kwamba siyo tu bei imepanda lakini wenzetu wana uhaba wa mafuta kiasi cha kufanya kuwe na foleni ktk vtuo vya mafuta.

Hapa chini nimeweka bei za mafuta ktk nchi mbalimbali mpaka kufikia jana ambayo kimsingi bado inaonesha kuwa bei ya Tanzania ni nafuu kulinganisha na nchi zingine Afrika Mashariki.

Mimi binafsi ninaamini serikali haipendi wananchi wake wateseke hivyo wanaendelea kuchukua hatua zilizo ndani ya uwezo wetu ili kuona namna bora ya kuhakikisha ongezeko hii la bei halituathiri kwa kiasi kikubwa.

Tuendelee kushikamana na serikali ktk kipindi hiki kigumu lakini tusisahau kushauri namna bora zaidi badala ya kupotosha au kuchonganisha.

Kwa mtizamano wangu ni wakati sasa serikali kuwekeza zaidi ktk gas badala ya mafuta ya petrol na diesel ili tupunguze kasi ya utegemezi wa nishati.

20220406_111556.png

Hapa chini ni bei ya mafuta ktk nchi mbalimbali hadi kufikia jana kabla ya bei mpya za leo ikionesha kuwa licha ya bei ya mafuta kupanda lakini bei yetu ni nafuu kuliko nchi zingine zingine Afrika Mashariki.
Screenshot_20220406-083804_WhatsApp.jpg

20220406_131603.jpg
 
Bandiko zuri Ila Kuna sehemu hujaweka taarifa sahihi
Magufuli hadi anaafariki bei ilikua ni sh. 1981 na sio 2400 to 2500
Hiyo Bei 2400 to 2500 ilikua Ni mwaka Jana November na december
Screenshot_20220406-122221_1.jpg
 
Gesi gani..? Hii ambayo nayo haieleweki! Tunagesi nchini lakini bei sasa ndo waje walete kwenye magari si mtapaki magari huko..😂
 
KUONGEZEKA KWA BEI YA MAFUTA YA PETROL NA DIESEL KUMESABABISHWA NA ONGEZEKO LA BEI KTK SOKO LA DUNIA NA SIYO KOSA LA RAIS SAMIA.

Hapo jana serikali imetangaza bei mpya ya mafuta ya bei ya petroli na diesel ambapo kwa hapa Tanzania bei inatarajiwa kuanzia leo kuwa kati ya sh 2700-3000

Kuna watu wengi hutumia mwanya wa ongezeko la bei ya mafuta kuwa ni uzembe wa Rais Samia na wengine wamekwenda mbali kwa kusema kuwa angekuwepo Magufuli (R.I.P) BEI ISINGEPANDA; Huu ni upotoshaji na uchonganishi usiokuwa na tija kwa Taifa letu. Rais Magufuli amefanya kazi kubwa sana ktk nchi yetu lakini siyo sahihi kusema angekuwepo yeye bei ya mafuta isingekuwa kubwa ilihali kiuhalisia bei ya mafuta haijapanda ktk soko la ndani baki ktk soko la dunia ambapo kwa namna yoyote athari za bei lazima uzipate kwa kuwa sisi siyo wazalishaji wa mafuta hayo

Linapokuja suala la mabadiliko ya bei ya mafuta ktk soko la dunia bei hiyo hubadilika ktk nchi zote na tunaoumia hasa ni nchi ambazo hazizalishi mafuta ikiwemo Tanzania.

Bahati nzuri ktk ukanda wa Afrika Mashariki licha ya bei ya mafuta kupanda ktk soko la dunia lakini bei yetu ni nafuu kuliko nchi zingine za afrika mashariki kama Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Kwa wale wanaoamini kuwa Magufuli angekuwepo bei ya mafuta isingepanda naomba niwakumbushe kidogo.

Kipind Magufuli anaapishwa 2015, TZ bei ya petroli ilikuwa 1900-2000/litre ambapo bei ya mafuta duniani ilikiwa ni $40 kwa pipa.

Mpaka anafariki 2021, aliacha mafuta yakiuzwa 2400-2500/-. Leo hii pipa la mafuta katiķa soko la dunia ni hadi $140 na Tanzania yakiuzwa kati ya 2700-3000 kwa lita.

Ikumbukwe kuwa bei imeongezeka karibu mara mbili ya bei ya mwaka 2020 na karibu mara tatu ya bei ya mwaka 2015 lakini serikali imejitahidi kudhibiti mfumuko wa bei ya mafuta.

Uwezo wa serikali yetu ni kudhibiti mfumuko wa soko la ndani liendane na soko la dunia lakini si rahisi kudhibiti bei tofauti na ile inayouzwa ktk soko la dunia

Aidha tunaweza kulaumu tu kama bei ya mafuta nchini ikiwa kubwa kuliko nchi zingine au kuliko ktk soko la dunia.

Njia pekee ya kuweza kukabiliana na makali ya bei ni kwa serikali kutoa fedha ya ruzuku kwa wafanyabiashara ili kuuza bei rafiki (mfumo huu ni wa gharama ambao unategemeana na bajeti na uwezo wa serikali kifedha)

Tumeshuhudia nchini Kenya kwamba siyo tu bei imepanda lakini wenzetu wana uhaba wa mafuta kiasi cha kufanya kuwe na foleni ktk vtuo vya mafuta.

Hapa chini nimeweka bei za mafuta ktk nchi mbalimbali mpaka kufikia jana ambayo kimsingi bado inaonesha kuwa bei ya Tanzania ni nafuu kulinganisha na nchi zingine Afrika Mashariki.

Mimi binafsi ninaamini serikali haipendi wananchi wake wateseke hivyo wanaendelea kuchukua hatua zilizo ndani ya uwezo wetu ili kuona namna bora ya kuhakikisha ongezeko hii la bei halituathiri kwa kiasi kikubwa.

Tuendelee kushikamana na serikali ktk kipindi hiki kigumu lakini tusisahau kushauri namna bora zaidi badala ya kupotosha au kuchonganisha.

Kwa mtizamano wangu ni wakati sasa serikali kuwekeza zaidi ktk gas badala ya mafuta ya petrol na diesel ili tupunguze kasi ya utegemezi wa nishati.

View attachment 2177633

View attachment 2177634
50% kwenye bei ya lita moja ya mafuta ni kodi za serikali baasi wangepunguza izo kodi ili wananchi tupate unafuu
Walisema ile 100 ndo inarudishwa cha ajabu wamepandisha hadiii 310
Majiraniiii zetu serikali imetoa pesa 13b ili kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta ili kuleta unafuu kwa mwananchi sisi serikali yetu ndo kwanzaaaa imeongeza bei
 
Unapoondoa kodi lazima uwe na mbadala wa mapato ya kodi hiyo kwa haraka ili nchi iendelee kujiendesha

Kuondoa kodi siyo kitu rahisi kama unavyofikiria, huo siyo ushauri rafiki na haiwezekan
 
Yani kwako 100 huioni kama ni pesa au hutaki tu kukubali ukweli kuwa huyu mama ameongeza maumivu kwa kuongeza 100 kwenye kila lita?
Nasisitiza hata ukiondoa hiyo 100 haitapunguza uwezekano wa kupanda kwa bei
 
Back
Top Bottom