Kuongezeka kwa bei ya mafuta nchini kunatokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia na siyo kosa la serikali ya Rais Samia

Unapoondoa kodi lazima uwe na mbadala wa mapato ya kodi hiyo kwa haraka ili nchi iendelee kujiendesha

Kuondoa kodi siyo kitu rahisi kama unavyofikiria, huo siyo ushauri rafiki na haiwezekan
Iviii zile kodi za miamala za simu zilizokuwa imposed ni kodi ipi ilifutwa ilii izo za miamala ya simu iwe mmbadalaa
 
Bei ya mafuta ni 2700-3000


Hiyo 3400 labda wanakouza kwa madumu huko vijijini au migodini ambako wanajiamulia bei
Kigoma bei halali ni 3093, na ndio Bei ya juu nchi nzima

Unapaswa kusema ni kati ya 2700-3100

Hizi bei zimetolewa na ewura Wala huna haja ya kukaza mishipa
 
Hizo ni brah brah tunataka bei ishuke hayo mengine hayatuhusu 🐒
 
chapati moja 500,kitumbua na andazi 300,chai 400, unga kilo1300 kweli vita ya urusi kiboko
 
Kwani hawa Marais wanaopambana na changamoto ya mafuta kupanda bei ni kosa lao?🐒🐒🐒
 
Kigoma bei halali ni 3093, na ndio Bei ya juu nchi nzima

Unapaswa kusema ni kati ya 2700-3100

Hizi bei zimetolewa na ewura Wala huna haja ya kukaza mishipa
Sasa bei ya 3400 uliitoa wapi?
 
Bei ya mafuta ni 2700-3000


Hiyo 3400 labda wanakouza kwa madumu huko vijijini au migodini ambako wanajiamulia bei
Unaongea kama juha. Kwahiyo siku hizi kuna bei za migodini na za mikoani? Ujinga wa nchii hii mpk kuwe na mbadala wa sifiasifia
 
Unaongea kama juha. Kwahiyo siku hizi kuna bei za migodini na za mikoani? Ujinga wa nchii hii mpk kuwe na mbadala wa sifiasifia
Bei elekezi ni kwa ajili vituo vilivyosajiliwa kuuza mafuta. Yanayouzwa kwenye madumu yanauzwa kinyume na utaratibu
 
Wakati wa mlipuko wa covid 19 bei ya mafuta kwenye soko la dunia iliteremka hadi kufikia dola 20 kwa pipa kwani watu wengi walikuwa lockdown na uzalishaji viwandani ulikuwa umesimama kwa kiasi kikubwa. Lakini hapa kwetu bei ya mafuta iliendelea kupanda. Ilifika hadi watu wa Mbeya kununua mafuta hayo toka Zambia kwani kule bei iliteremka sana licha ya mafuta yao kupitia DSM.

Serikali yetu ina aina ya tozo zaidi ya kumi kwenye bidhaa hii ya mafuta kama ilivyokuwa kwenye bidhaa za kilimo hususani kahawa. Na kila mwaka wa bajeti, serikali huwa inaongeza aina ya tozo kwenye bidhaa hii ya mafuta.

Vita ya Russia vs Ukraine imepelekea nchi za Amerika na za ulaya kususa (sanction) kununua mafuta toka Russia ili kumbana mruso kiuchumi ashindwe vita. Russia ni mzalishaji mkubwa duniani. Theluthi moja ya mafuta yote duniani hutoka Russia. Ususaji huu umepelekea nchi ya Saudi Arabia (top producer) na zile za OPEC kuendelea kupandisha bei za mafuta yao ili kujinufaisha na mzozo huu. Leo pipa linauzwa kwa dola 150. Na bado litaendelea kupanda. Si ajabu ndani ya wiki mbili zijazo likafika dola 300. Hatujui vita hiyo itachukua muda gani kwisha na hali kurejea tulikotoka. Lakini mafuta toka Russia yameendelea kupungua bei hadi sasa kufikia dola 30 kwa pipa.

Hivyo kama hatutajipanga vizuri kila kitu kitavurugika. Mfumuko mkubwa wa bei utatokea. Uchumi wa nchi utasinyaa sana. Thamani ya pesa yetu itateremka sana. Makusanyo ya kodi yataporomoka kwani uchumi utakuwa umesinyaa. Maamuzi aliyofanya Makamba ya kuagiza mafuta haya ya bei ya dola 150 kwa pipa la crude oil (refined oil ni zaidi ya dola 230) kwa mkupuo wa kututosheleza miezi 3 hadi Juni 2022? si sahihi hata kidogo. Kwani kama bei ya soko la dunia itateremka hadi kufikia dola 80 kwa pipa mwezi May 2022, itakuwa imekula kwetu. Na kuna dalili kubwa wa mzozo huu wa Russia vs Ukraine kuisha hivi karibuni.

Mapendekezo makini ya kukabiliana na tatizo hili ni kama ifuatavyo:
1. Kupunguza kwa kiwango kikubwa cha idadi ya tozo za serikali katika bidhaa hii hadi zibakie aina ya tozo sisizozidi tatu kama tulivyofanya kwa kahawa ili kulinda uchumi wa nchi yetu.

2. Kubana sana matumizi ya serikali yasiyo ya lazima hususani washa, semina na safari za ndani ya nchi na nje ya nchi.

3. Kuiga mfano uliooneshwa na nchi za India na China, wa kununua mafuta haya kutoka Russia ambayo yameteremka bei hadi kufikia dola 30 kwa pipa baada ya sanctions.
 
Rais lege lege hawezi kusanya kodi kutoka vyanzo vigumu. Badala yake hukusanya kodi Kupitia vyanzo laini kama hivi vya mafuta.

RIP JPM
 
Rais lege lege hawezi kusanya kodi kutoka vyanzo vigumu. Badala yake hukusanya kodi Kupitia vyanzo laini kama hivi vya mafuta.

RIP JPM
umeongea point kubwa sana
some people are not paying their fair share ,na serikali kwa makusudi inawalinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…