Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Amani iwe nanyi,
Habari kuu kwa sasa duniani ni kupanda kwa bidhaa adimu kutokana na vita vinavyoendelea vya Russia v Ukraine.
Bidhaa adimu kama mafuta na Gesi zinazidi kupanda kwa kiwango cha kutisha na Mataifa yenye mafuta na Gesi Afrika yameanza kukamatia fursa kuongeza mapato yake kwa mfano Algeria, Angola, Equatorial Guinea, Nigeria na Misri
Bidhaa nyingine zinazopanda bei kwa kiwango cha kutisha kwenye soko la dunia sasa ni Dhahabu na Mahindi.
Tanzania hatujaingia kwenye soko la dunia kwa bidhaa za Mafuta na Gesi ila kwenye bidhaa za Dhahabu na Mahindi tupo kwenye soko la dunia maana dhahabu na mahindi kutoka Tanzania yanauzwa kwenye soko la dunia.
Baada ya taarifa hizi za kuzidi kuongezeka kwa bei ya dhahabu na Mahindi ambazo zinaweza kutuingizia mapato makubwa kipindi hiki napenda kuwauliza Waziri wa Madini Dotto Biteko, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na Gavana wa Benki Kuu Prof Luoga wamejipangaje katika kuhakikisha Tanzania tunafaidika sana na hali hii?