Kuongezeka kwa bei za Dhahabu na Mahindi duniani; Mawaziri Biteko na Bashe na Gavana BoT mmejipangaje?


This is like Betting, I wish I could have put my stake to such n such a team
 
Hivi Tanzania tunaongoza kwa kununua nini??
Tunaongoza kwenye uozo mkubwa ambao umerudi kwa mlango wa nyuma. Zile kampuni za mafuta za Msoga Corporation nazo zitavuna faida kubwa. Awamu ya nne imerudi kazini, tutakoma. Upinzani umelaininshwa na Kiswahili cha Zanzibar nao sasa wamebaki kama mazuzu ya CCM. Unaona sasa walewale wamerudi ili kurudisha mikakati ya kuikamuwa nchi mpaka ikome. Mikopo sasa njenje, lakini kulipa ni Tanganyika!
 

kuna wakati mkuu tuache kuwa walalamishi, tujitahidi tuwe tunatoa michango yetu kulingana na mada zilizopo jukwaani, hapa wanaulizwa mawaziri wamejipangaje kulingana na "kupanda kwa bei za dhahabu na mazao"

Binafsi naona wengi wetu tumekuwa walalamishi wa kunyooshea viongozi vidole huku na sisi tukiwa na tabia zilezile huku mitaani, wapo watanzania wanalalamikia viongozi kila kukicha lakini wenyewe wameajiliwa sekta binafsi na huko nao ni wezi pia, wengine huku mitaani tunao kazi yao kudhulumu wenzao, wengine wachawi, wengine wezi nk...

Hawa viongozi tunaowalalamikia kila siku ndio hawa hawa wakija kwenye familia zetu kwenye misiba na harusi tunawashukuru kwa michango yao mikubwa, wakija kwenye familia wakisomesha ndugu kwa hizo hizo hela za wizi tunawafurahia na kuwapongeza....

Binafsi naamini matatizo ya Tanzania ni matatizo ya Africa yoote, shida hizi kila mahala ukienda Africa utazikuta kifupi ndio tabia ya mtu mweusi, Tunalalamikia awamu ya nne kana kwamba awamu zote hazikuwahi kuwa na wizi au upigaji, nchi hii awamu zote za uongozi kuanzia JKN mpaka hii ya leo zote watu ni wapigaji tu kupindukia maana ndio tabia ya mtu mweusi hata mimi na wewe ni wale wale tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…