Kuongezeka kwa ubaguzi wa kiuchumi, kieneo na ukabila nchini Tanzania

Kuongezeka kwa ubaguzi wa kiuchumi, kieneo na ukabila nchini Tanzania

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Tusiposema sasa mawe yatasema.

Sasa hivi nchi inapitia ubaguzi wa wazi kieneo, ukabila na upendeleo wa wazi kwa sehemu fulani fulani nchini Tanzania.

Haya ni mambo ambayo Tanzania hatukuyazoea wala kushuhudia toka enzi za kupata uhuru.

Mwalimu alijishusha mno na hata hakupendelea kwao kwa jinsi tunavyoshuhudia sasa, mimi Butiama nimefika.

Ubaguzi wa aina yoyote una mwisho si mzuri kwa mustakabali wa Taifa.

Chama kimelala.
Bunge ndio kabisa.
Lakini wahenga wanasema tutavuna tunachopanda.
 
Kamwe nashindwa kupita kimyakimya kwenye mada kama hii inayosononesha moyo.

Wakati huo huo, karibu kila mtu anaimba "Tano Tena", kama utani vile!

Sijui nchii imepatwa na janga gani.

Ni kama wote tumepigwa ganzi tusitambue ni nini hasa kinatokea.

Mimi sijui ni nani atakayekuja kututapisha sumu hii tuliyoonjeshwa sasa, ili taifa letu liendelee kuwa taifa lenye mshikamano kama aliouacha Mwalimu Nyerere.

Eeenh, sasa Mwalimu hata anasimangwa. Wale watoto nao wamekuwa kama mazuzu vile, wanatafuta ulaji, wanapoukosa wanaambiwa sababu ni kuwa baba yao hakufanya kitu nyumbani kwao!
 
Tatizo ni huu unafiki wa kushindwa hata kusema tatizo unaloliona na nani anapendelewa. Sema ni nani ili tujadili na kukemea tatizo. Unaogopa hata kusema unachofahamu kwa majina bandia! Cowardice!

Miaka iliyopita sisi tuliposema wachaga wanakusanyana TRA, na CRDB tulipewa jibu la urahisi kwamba wamesoma sana! walikenua meno kwa furaha na kuamini kweli wamesoma.

Leo hii bado wamesoma? Kulikuwa na miaka Wanyakyusa walijaa NIC ya Mwaikambo na NBC ya Nsekela wakasingizia wingi na kusoma. Sijuyi leo wamepungua na hawasomi!

Watu wa Iringa nao sasa hivi wanajionesha na kuhalalisha sababu ya kusoma sana wakati tunajua wanaalikana na hata kuunda vikundi vya kutambulishana. Ujinga umewaanza baadaye watalia midomo wazi maana ubaya makabila machache yanapenda kuishi mikoa ya iringa na Njombe. Wahaya wamesemwa sana lakini hatujawahi kuwaona wakialikana kwenye ofisi au taasisi ya serikali.

Tuseme wazi acha kujidai mwana fasihi wakati unachoeleza unataka kijadiliwe.
 
Tatizo ni huu unafiki wa kushindwa hata kusema tatizo unaloliona na nani anapendelewa. Sema ni nani ili tujadili na kukemea tatizo. Unaogopa hata kusema unachofahamu kwa majina bandia!! Cowardice!...
Eti wahaya hawaalikani? Naona umelewa rubisi si bure.

Infact hao uliosema wamejaa CRDB na TRA wapo na walikuwepo na watazidi kuwepo
 
Siku zote kipande chako cha mkate kikipakwa siagi huwezi kuelewa maumivu ya wenzako. Leo Rais akitoka Kigoma, usishangae kuna watakaosema Kigoma inapendelewa. Mkoa ambao mpaka juzi kati ulikuwa hauna hata KM 50 za lami!

Chato na wilaya nyinginezo pembezoni zilikuwa zimeshahalalishiwa umasikini.

Inawezekana nisikubaliane na yote ya JPM, lakini..bila uthubutu wa viongozi kama JPM kuna mikoa na wilaya humu Tanzania zitakuwa masikini milele!
 
Tatizo ni huu unafiki wa kushindwa hata kusema tatizo unaloliona na nani anapendelewa. Sema ni nani ili tujadili na kukemea tatizo. Unaogopa hata kusema unachofahamu kwa majina bandia!! Cowardice!..
Tunaishi nyakati unazizijua vema.

Na mada umeilewa vema ila una unafiki wa ku act kuwa a wounded guy.

Kisaikolojia umasikini wako unaamua kujihalalishia ubaguzi wako.

Refer kwa Mwalimu, nakupeleka SUNGURATEX Butiama, ingwaje kule wanalima pamba.

Hata barabara kwenda Butiama zilijengwa baada ya yeye kufariki.

Buhemba pale kuna dhahabu, lakini Mwalimu hakuweka umimi mbele.

Tunayoyaona yanashangaza.
 
Back
Top Bottom