Kuongezeka kwa ubaguzi wa kiuchumi, kieneo na ukabila nchini Tanzania

Kuongezeka kwa ubaguzi wa kiuchumi, kieneo na ukabila nchini Tanzania

Hivi humu si ndio kuna mada lukuki za watu kujidai eti mkoa wetu wa KILIMANJARO unaongoza kwa lami nyingi mpaka vijijini, umeme mpaka kwenye migombani. Na mikoa mingine ikidhihakiwa kwamba ni hohehae...
Wachagga wanajivunia bidii ya mikono yao zaidi ya kazi za serikali,ndiyo maana wanajivunia nyumba bora,elimu bora,uchumi wa mtu mmoja mmoja na biashara zao zaidi ya viwanja vya ndege na makusanyo ya tra,hawajivunii ukoloni japo ukoloni ndiyo uliowawezesha kielimu kuliko hata serikali ya nchi yao,hivyo tu
 
Jiwe.

Hayo uliyoandika hapo juu tulishayajadili vya kutosha na kueleweka. Hakuna sababu tena ya kuyarudia rudia.
Mkuu pamoja na kutofautiana kimawazo, sithubutu kumwita Rais Magufuli Jiwe.
Its disrespectful.
Na ndio maana naweza criticise ideas ambazo naona si sawa.
 
Mkuu pamoja na kutofautiana kimawazo, sithubutu kumwita Rais Magufuli Jiwe.
Its disrespectful.
Na ndio maana naweza criticise ideas ambazo naona si sawa.
Wewe sio mgeni ndani ya jukwaa hili.
Hilo jina sio kigezo tena cha kuwa "disrespectful", imekwishakuwa 'nickname', kama zilivyo zingine zote.

Lakini naelewa maana yako ya kuja hivyo, maana nakumbuka mwanzo wa kujibishana kati yetu ilianzia huko huko unakotokea, kwa hiyo hiyo hainishangazi "Jidu La Mabambasi"; jina linalo'rhyme' vyema.
 
Kujadili haya ni ubatili na upuuzi mtupu!!
Tunapaswa kuijadili katiba mpya ili kuondoa madaraka makubwa alopewa MTU mmoja kiasi anaamua apendavyo na anatisha watu ajiskiavyo. Upuuzi wakumweka MTU juu yasheria na katiba wanasheria wajao watajiuliza hawa wanaojiita "wakili msomi" tulonao leo walisomea ujinga ama nini!. Haiwezekani wanasheria wasomi wanashindwa kuipigania Katiba bora kwa ustawi wa nchi wanachojua ni kujiita mawakili wasomi kwakutetea tuu vibaka na wabakaji... shame on them!!!
 
Nyundo juu ya msumari.

Hakuna nyundo wala msumali hapo!!! Iko kwenye DNA ya Viongozi Wengi wa Tanzania kupendelea kwao na kujilimbikizia mali. Sumaye alipokuwa waziri mkuu alihakikisha kuwa kwao wanapata Mkoa[ MANYARA]; mtoto wa mkulima nae akazalisha mkoa kwao[ KATAVI]. Kuhusu kujilimbikizia mali , viongozi wote wamejilimbikizia mali zilizowekezwa huko:

Usambara, Dar es salaam, Mtibwa, Katavi, Dodoma, Msoga,Chato, Zanzibar na DUBAI!!! Hivyo kila aliyepata nafasi ya kuongoza kasoro Kambarage peke yake hao wengine wote walikuwa wakwapuaji!!! Ukisikia mtu analalamika ujue aliwahi kukaa mezani kula na sasa hayupo mezani kwani ni zamu ya wengine kula!!!

Ntashangaa sana kama Jiwe atamaliza muhula wake bila Chato kuwa mkoa!!!
 
Yaani mtu kashindwa kuajiri, kupandisha madaraja mishahara, kulipa wastaafu kwa miaka mitano, kaharibu uchumi, biashara, siasa, mahusiano ya kimataifa huyu ndio aongezewe muda serious? Mgonjwa wa bipolar disorder kabisa.
 
Una umri gani wewe? Upendeleo ulikuwepo miaka yote. Nahisi kuna watu upendeleo umewatega mgongo ndo maana wanalia lia! Walipopendelewa wakasema ni haki yao. tulieni nchi inyooke.
Kwa maana hiyo unakiri kuwepo kwa unaguzi huo kama njia ya kulipiza kisasi?
 
Tunakoelekea bora tugawane majimbo kila jimbo lijiendeshe lenyewe maana kwa mfumo huu tulonao ni kama unyonyaji kwa baadhi ya mikoa.
Juzi niliangalia Jimbo Fulani Lina mgodi wa aina yake wananchi wake wanabebwa Kwa Nagari kwenda kishuhudia utiaji sahihi .Jimbo halina mradi WA maana hata mmoja na hata campaign Mzee hakuona maana ya kwenda huko Bali kiwabeba kama wenyewe Hawana kwao
 
Tunakoelekea bora tugawane majimbo kila jimbo lijiendeshe lenyewe maana kwa mfumo huu tulonao ni kama unyonyaji kwa baadhi ya mikoa.
Kwa miaka mingi CHADEMA na watu wenye akili na kusisitizwa na Lissu, walijaribu kupendekeza mfumo wa Majimbo lakini wajinga wa CCM wamekuwa wakipinga na kukejeli kwa nguvu ya wingi wao lakini ukweli wa nchi kubwa kama Tanzania Utawala wa Majimbo ndo unafaa kuliko uongozi wa mtu mmoja kutoka Chato peke yake.

Katika Mfumo huu, kila Jimbo linakuwa na Serikali yake ikiongozwa na Viongozi wake wanaopatikana kutokana na wakazi wake kwa kutumia rasirimali zinazopatikana Jimboni. Mfano: Kama Geita lingekuwa Jimbo Uwanja Ndege wa Chato usingejegwa kwa sababu siyo mahitaji muhimu ya wakazi wa Jimbo vilevile gharama za ujenzi ni kubwa kuzidi uwezo wao lakini kama wakazi wangekuwa wanahitaji Uwanja huo, ingebidi Jimbo liombe msaada Serikali Kuu ambayo ina mapato yake na ina uwezo wa kukopa.

Uwanja ule umejengwa na Watanzania wote kwa manufaa ya wakazi wa Chato!
 
Tusiposema sasa mawe yatasema.

Sasa hivi nchi inapitia ubaguzi wa wazi kieneo , ukabila na upendeleo wa wazi kwa sehemu fulani fulani nchini Tanzania...
Ni kweli, waziri wa fedha wakati ule hakupendelea miradi ya maendeleo kama barabara , shule, umeme, na viwanda kwao, na kwa mashirika yalio chini ya fedha au viwanda hakupendelea wa kwao
 
Nyie watoto wa juzi hamjui kuwa ile main road toka Moshi hadi zkorogwe ilianza kuwa diverted ili ipite katikati ya mji wa Mwanga.
Kazi ilianza na ilistopishwa na Serikali ya Mwalimu.
Wakati jimbo jipya la Mwanga ( likitengwatoka Same) linaanzishwa mambo mengi sana yalipangwa na CD lakini yalikataliwa.
Source: mimi mweyewe

barabara ya korogwe same mwanga moshi inapita ktk jimbo la mwanga ambalo msuya alikuwa mbunge. sasa hebu tueleze huo upendeleo uko wapi wakati tayari barabara inapita jimboni kwake? mimi ninavyoelewa upendeleo ni kiongozi kupeleka huduma fulani eneo lake na kuwanyima wananchi wa maeneo mengine huduma hiyo. kwa mfano kiongozi toka wilaya A alazimishe huduma ipelekwe ktk eneo lake wakati serikali ilikuwa imepanga huduma hiyo iende eneo B.

tukirudi kwa cleopa msuya kuna wakati watu walikuwa wanadai kwamba amechukua ramani ya ujenzi wa jiji la dodoma na kwenda kujenga kwao mwanga. sasa kuna watu wa ccm walitembelea jimbo la mwanga na kukuta hali tofauti na maneno ya mitaani yaliyokuwa yakisemwa kuhusu wapare, wana mwanga, na cleopa msuya. mambo mengi kuhusu msuya siyo ya kweli, bali yametokana na vita ya uongozi ndani ya ccm na serikalini.

mwisho, naomba uache kuchonganisha jamii wa wapare na watanzania wenzao. maendeleo ya upareni yametokana na juhudi za wananchi wenyewe kutokana na utamaduni wa kujitolea kazi wa MSARAGAMBO. kupitia msaragambo wapare wameweza kujenga mashule, kuchimba mifereji ya kilimo cha umwagiliaji, kuchimba barabara za milimani, n.k
 
Nyundo juu ya msumari.
huyu jamaa ni mtu wa hovyo kabisa. anataka kutuletea chuki tusiyoistahili. utakuta ndio wale wanaoamini kwamba chediel mgonja ndiye aliyepeleka elimu upareni. wangefanya uchunguzi wangegundua kwamba kisomo cha watu wazima kilianza upareni mwaka 1949 kwa mpango wa majaribio wa serikali ya muingereza. wapare walishafikia malengo ya mpango wa upe miongo kadhaa kabla ya tanzania kuamua kutekeleza mpango wa upe mwaka 1977. mwingine kule jukwaa la historia alidai wapare walifundishwa dini ya Kiislamu mwaka 1945 na jamaa mmoja toka Uchagani. Mimi nikamuuliza mbona kabla ya hapo tayari kulikuwa na Wafumwa ambao ni Waislamu?
 
huyu jamaa ni mtu wa hovyo kabisa. anataka kutuletea chuki tusiyoistahili. utakuta ndio wale wanaoamini kwamba chediel mgonja ndiye aliyepeleka elimu upareni. wangefanya uchunguzi wangegundua kwamba kisomo cha watu wazima kilianza upareni mwaka 1949 kwa mpango wa majaribio wa serikali ya muingereza. wapare walishafikia malengo ya mpango wa upe miongo kadhaa kabla ya tanzania kuamua kutekeleza mpango wa upe mwaka 1977. mwingine kule jukwaa la historia alidai wapare walifundishwa dini ya Kiislamu mwaka 1945 na jamaa mmoja toka Uchagani. Mimi nikamuuliza mbona kabla ya hapo tayari kulikuwa na Wafumwa ambao ni Waislamu?
Wengine wanadandia tuu, stories za mitaani wanataka kuzilazimisha ziwe kweli.

Karibu kila Ukoo wa kipare una Waislamu , na dini ya uislamu nafikiri imeingia zamani sana, sina hakika kwa hili, lakini kabla ya Ukristu kuingia Upareni.

Na kila Mpare mwenye zaidi ya miaka 60 atakwambia elimu alipata kwa taabu na shule hazikuwa karibu karibu sana kama leo.
 
Wachaga bwana...kwa hiyo wanalalamika wanasemaje mkuu??? Jamani wonders shall never end..wao waliendelea zamani wanalalamika nini Sasa..mpaka huku kwetu buzirayombo wapo..Kama Ni matunda ya kazi nzuri za baba Jesca bado wanafaidi tu..mwanza ndio usiseme ndio wanarun the show...na Kahama...Sasa wanalalamika nini hao akina bwashee... Kikubwa serikali ya baba Jesca Ni serikali ya watu wote..haina ubaguzi wa kikabila,kidini au rangi..haya mengine ni maneno ya mashabiki tu..
Na kikubwa watanzania wenzangu tupendane..na tuvumiliane kwa misingi ya tofauti zetu...nchi hii Ni yetu sote
SEREKALI YA MAGUFULI INAO UBAGUZI WA KISIASA ( UBAGUZI KTK MISINGI YA ITIKADI ZA KISIASA)
 
Tusiposema sasa mawe yatasema.

Sasa hivi nchi inapitia ubaguzi wa wazi kieneo , ukabila na upendeleo wa wazi kwa sehemu fulani fulani nchini Tanzania...
Kweli, na mimi Butiama nimefika nikitokea Kilimanjaro! Kwa nini sasa hivi maendeleo yanasambazwa Tanzania nzima? Mfano; kwa nini maji yanatolewa ziwa Victoria kwenda Tabora?

Hii itawafanya watu wa Tabora waendelee kama Kilimanjaro! Ni ukabila mtupu, tunataka maendeleo ya baki yalivyo achwa na Mwalimu Nyerere -na pia ni marufuku sehemu anapotoka raisi kupeleka maendeleo! Tuendane na Butiama, kama si hivyo, ni ukabila.
 
Tusiposema sasa mawe yatasema.

Sasa hivi nchi inapitia ubaguzi wa wazi kieneo , ukabila na upendeleo wa wazi kwa sehemu fulani fulani nchini Tanzania...
Jiwe hovyooo kabisa. Chato ni ikulu ya 3 baada ya Magogoni na Chamwino.
 
Ki
Tunaishi nyakati unazizijua vema.
Na mada umeilewa vema ila una unafiki wa ku act kuwa a wounded guy...
Kitendo cha Nyerere kutoendeleza Butiama hakimuonyeshi Mwalimu kuwa ni mzalendo sana! Ni mapungufu yake, kama mapungufu mengine waliyonayo watu wengine.

Na hayo mapungufu kurudiwa na kiongozi mwingine ni carelessness na unfortunate!
 
barabara ya korogwe same mwanga moshi inapita ktk jimbo la mwanga ambalo msuya alikuwa mbunge. sasa hebu tueleze huo upendeleo uko wapi wakati tayari barabara inapita jimboni kwake? mimi ninavyoelewa upendeleo ni kiongozi kupeleka huduma fulani eneo lake na kuwanyima wananchi wa maeneo mengine huduma hiyo. kwa mfano kiongozi toka wilaya A alazimishe huduma ipelekwe ktk eneo lake wakati serikali ilikuwa imepanga huduma hiyo iende eneo B...
Tulikuwepo wakati wa upendeleo wa wazi wakati CD akipendelea kwao na baadaye kukemewa na Mwalimu.
Huwezi pindisha historia.

Na Mwalimu in exasperation aliwahi kusema.”Nimekuwa na Mwaziri wakuu wengi, pamoja na Waziri Mkuu wa Mwanga..”
It was a rebuke!

Haya tunayoyaona sasa yana ulinganishi.
 
Back
Top Bottom