Kuongezeka kwa ubaguzi wa kiuchumi, kieneo na ukabila nchini Tanzania

Kuongezeka kwa ubaguzi wa kiuchumi, kieneo na ukabila nchini Tanzania

Tunakoelekea bora tugawane majimbo kila jimbo lijiendeshe lenyewe maana kwa mfumo huu tulonao ni kama unyonyaji kwa baadhi ya mikoa
Fikiria mara mbili, iko mikoa tukigawana majimbo itasumbuka sana, mikoa ya kaskazini taabu ni kubwa zaidi, mikoa yenye neema kwa miaka mingi ijayo ni kanda ya ziwa.

Wana Ardhi yenye rutuba, wana maji ya kutosha, sasa hivi wana dhahabu nyingi ya akiba kuliko dhahabu tulio kwisha kuichimba tangu nchi hii iumbwe iko kwao Pole Pole Wilaya ya Sikonge. . Na Almasi ni hivyo hivyo .

Wako wengi ki uchumi maana yake ni soko, na ni watu wa bidii. Hawana kitu Watakosa labda elimu. Na ni naona jitihada ya shule ime ongezeka sana na sio wajinga madarasani.

Tutafute kingeni hiki hakina faida kwetu.
 
Hali mbaya sana mpaka kwenye mifupa, juzi nilikuwa Mwanga kwa dingi Christmas , baadae nikaendelea kwa bii mkubwa Lyamungo, kelele zinafana sana, na kote hali mbaya kuliko walivyozoea.
Vipi utaratibu wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa chato wakati Arusha au mwanza au geita hamna ni sawa?
 
Vipi utaratibu wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa chato wakati Arusha au mwanza au geita hamna ni sawa?
Ndiyo maana nilisema huko nyuma kaubaguzi ka kieneo kiuchumi kanatunyemelea.
Nakumbuka Waziri Mkuu Cleopa Msuya alijaribu kitu kama hiki kwa jimbo lake la Mwanga.
Mwalimu alimkemea.
 
Inawezekana nisikubaliane na yote ya JPM, lakini..bila uthubutu wa viongozi kama JPM kuna mikoa na wilaya humu Tanzania zitakuwa masikini milele!
Sasa huyo JPM huo uthubutu wake anaufanya wapi kama sio kwao?! Mikoa kama Lindi, Mtwara, Rukwa, Singida, Pwani na mingine mingi tu ni mikoa yenye umaskini wa kutisha!!

Je, huo uthubutu mbona hatuuoni akiufanya na huko? Nini msingi wa hoja yako kama sio kujaribu kutetea mambo ya hovyo yanayopaswa kukemewa! Tukisema kila kiongozi apendelee kwao tutakuwa na taifa la aina gani?!

Tanzania lina mikoa 25, hata kama urais ingekuwa unaenda kwa mzunguko, ina maana ulitarajia mkoa utakaokuwa wa mwisho kupata nafasi ya urais ukae angalau miaka 100 kabla haijafikiwa na share ya upendeleo kwa kupata rais wa kwao?! Hivi hata hiyo Chato itafika wapi tukisema marais watakaofuata waipe mgongo na kila kitu waelekeze kwao?
 
Ndiyo maana nilisema huko nyuma kaubaguzi ka kieneo kiuchumi kanatunyemelea.
Nakumbuka Waziri Mkuu Cleopa Msuya alijaribu kitu kama hiki kwa jimbo lake la Mwanga.
Mwalimu alimkemea.
Tayari ubaguzi ushaota mizizi ni vigumu kuukwepa maana Rais ajaye atatanguliza shukrani kwao kama afanyavyo huyu yohana. Hili ni tatizo litakalopelekea unequal distribution of natioanl wealth.

Kodi zoooote za Nchi nzima zitakuwa dedicated kwa kaeneo kadogo tena unproductive, wha a shame we are going to feace? Tanzania ishapoteza sifa yake ya kutambulika duniani kuwa mahali penye amani na utulivu kwa tamaa za watu wachache tu. Very insane!
 
Ndiyo maana nilisema huko nyuma kaubaguzi ka kieneo kiuchumi kanatunyemelea.
Nakumbuka Waziri Mkuu Cleopa Msuya alijaribu kitu kama hiki kwa jimbo lake la Mwanga.
Mwalimu alimkemea.
huu ni UONGO. hebu tueleze wilaya ya mwanga ina kitu gani cha ajabu ambacho kimepelekwa na msuya na mbunge mwingine hawezi kukipeleka. msuya ndiye aliyepewa jukumu la kujenga viwanda baada ya jumuiya ya afrika mashariki kuvunjika. je, mwanga kuna kiwanda chochote kile? kuna gofu la kiwanda kilichojengwa enzi za mwalimu na msuya? barabara za milimani zinazowashangaza wengi zilijengwa na wafumwa wakati wa mkoloni.

Hii habari ya kusema wapare walipendelewa ni uongo uongo uongo. wapare wa kusini wana barabara ya mkomazi mpaka same wanalia mpaka kesho kwamba haijajengwa kiwango cha lami. na hiyo ndiyo barabara kongwe nchini lakini kila raisi anaipiga danadana kuijenga, halafu kuna mtu leo nimemsoma anasema daniel yona alipendelea same na wapare.

kilichowainua wapare ni uamuzi wa wafumwa kuchangamkia elimu kwa kila mtoto ambao ulitekelezwa kwa majaribio wakati wa mkoloni. uamuzi huo ndio uliopelekea wapare wathamini elimu hata ya mtoto wa kike. wakati tunapata uhuru Waislamu wa Upare walikuwa na shule zaidi ya 20, wakati Waislamu nchi nzima wanaambiwa hawapendi kusoma.

Wapare walishawahi kuwa na gazeti lao habari za Upare. kingine kilichowainua ni tabia ya wapare kutoka maeneo walikozaliwa kwenda mijini kutafuta maisha na kutokusahau kwao. wapare waliotoka nje zamani ndio waliopeleka wazo la kupasua barabara za milimani wakati wa utawala wa wafumwa/ machifu.
 
huu ni UONGO. hebu tueleze wilaya ya mwanga ina kitu gani cha ajabu ambacho kimepelekwa na msuya na mbunge mwingine hawezi kukipeleka. msuya ndiye aliyepewa jukumu la kujenga viwanda baada ya jumuiya ya afrika mashariki kuvunjika...
Nyundo juu ya msumari.
 
huu ni UONGO. hebu tueleze wilaya ya mwanga ina kitu gani cha ajabu ambacho kimepelekwa na msuya na mbunge mwingine hawezi kukipeleka. msuya ndiye aliyepewa jukumu la kujenga viwanda baada ya jumuiya ya afrika mashariki kuvunjika....
Nyie watoto wa juzi hamjui kuwa ile main road toka Moshi hadi zkorogwe ilianza kuwa diverted ili ipite katikati ya mji wa Mwanga.
Kazi ilianza na ilistopishwa na Serikali ya Mwalimu.

Wakati jimbo jipya la Mwanga ( likitengwatoka Same) linaanzishwa mambo mengi sana yalipangwa na CD lakini yalikataliwa.
Source: mimi mweyewe
 
Una umri gani wewe? Upendeleo ulikuwepo miaka yote. Nahisi kuna watu upendeleo umewatega mgongo ndo maana wanalia lia! Walipopendelewa wakasema ni haki yao. tulieni nchi inyooke.
Sasa itanyooka? Au ndiyo inapinda zaidi? Unajua tofauti ya haki na upendeleo? Ukipewa maendeleo wewe ni haki yako! Ila unapopewa zaidi ya stahiki yako ni upendeleo,na upendeleo ni zao la ubaguzi,na ubaguzi ni baba wa chuki,na chuki huzaa hasira,na hasira huzaa ghadhabu iletayo machafuko!!na---
 
Alafu kuna watu wanataka kumuongezea muda 😬😬😬 Anyway kila mtu apambane na hali yake
Typical of TRUMPIANS ... a generative syndrome with this aetiology:
Screenshot_20210208-210858_Chrome.jpg
 
Siku zote kipande chako cha mkate kikipakwa siagi huwezi kuelewa maumivu ya wenzako. Leo Rais akitoka Kigoma, usishangae kuna watakaosema Kigoma inapendelewa. Mkoa ambao mpaka juzi kati ulikuwa hauna hata KM 50 za lami!..
Masanja!! Ok!
 
Hivi humu si ndio kuna mada lukuki za watu kujidai eti mkoa wetu wa KILIMANJARO unaongoza kwa lami nyingi mpaka vijijini, umeme mpaka kwenye migombani. Na mikoa mingine ikidhihakiwa kwamba ni hohehae.

Sasa tunaanza kulia lia nini wkt Serikali inapambania kuweka usawa wa maendeleo kwa mikoa na maeneo mengne yaliyosahaulika ktk nchi hii?

Tuvumiliane tu, mbio za vijiti ni kupokezana.
 
Usipate majotro bro!
Mi na Maso ni waumini wa Mwalimu.
Na tuna mkataba wa kutuana tafu.
Nyie waumini wa nani?
Jiwe.

Hayo uliyoandika hapo juu tulishayajadili vya kutosha na kueleweka. Hakuna sababu tena ya kuyarudia rudia.
 
Fikiria mara mbili, iko mikoa tukigawana majimbo itasumbuka sana, mikoa ya kaskazini taabu ni kubwa zaidi, mikoa yenye neema kwa miaka mingi ijayo ni kanda ya ziwa...

Maendeleo siyo kilimo cha hand to mouth ngosha,wala siyo tu dhahabu na almasi zilizo mchangani,kuna nchi zina mafuta na dhahabu na vurugu na vita juu,yote sababu ya ukorofi wa watawala wao,kuna nchi hazina dhahabu wala mkaa wa mawe ila zina maendeleo na amani tele
 
Tusiposema sasa mawe yatasema.

Sasa hivi nchi inapitia ubaguzi wa wazi kieneo , ukabila na upendeleo wa wazi kwa sehemu fulani fulani nchini Tanzania...
Kuna tabia za kichawi ambazo zinakuja tunapotawaliwa na wachawi wafuga mintunga tabia hii inaitwa tukose wote. Tutaelewana tu subirini
 
Inawezekana nisikubaliane na yote ya JPM, lakini..bila uthubutu wa viongozi kama JPM kuna mikoa na wilaya humu Tanzania zitakuwa masikini milele!
Kwa hiyo unategemea na kuamini "...mikoa na wilaya humu Tanzania" nazo zitawapata akina JPM wao ili nazo ziondokane na "umaskini milele", kama inavyoondokana na umaskini Chato?
Huu ndio utaratibu utakaoondoa umaskini Tanzania?
 
Sasa itanyooka? Au ndiyo inapinda zaidi? Unajua tofauti ya haki na upendeleo? Ukipewa maendeleo wewe ni haki yako! Ila unapopewa zaidi ya stahiki yako ni upendeleo,na upendeleo ni zao la ubaguzi,na ubaguzi ni baba wa chuki,na chuki huzaa hasira,na hasira huzaa ghadhabu iletayo machafuko!!na---
Mkuu si wengi wanaiona mantiki hiyo. Watu wengine wanoana sasa mtu wa kwetu amepata madaraka, ndo muda wa kula.
Nepotism! Peleka miundombinu na kila kitu kwenu.

Kwa mfano, hivi zkassim Majaliwa, akiwa na sifa zote, hata sasa anazo, achaguliwe baada ya awamu hii na amepata urais.
Kitu cha kwanza kujenga kiwanja cha kimataifa kule kwao Ruangwa, Lindi.

Cha pili kupeleka wanyama na kuanzisha mbuga na hoteli za kitalii.

Kujenga mabenki huko na vile vile Ikulu kule Rwangwa.

Of course mtu kwao becomes standard norm.
 
Back
Top Bottom