Kuongezeka kwa ubaguzi wa kiuchumi, kieneo na ukabila nchini Tanzania

Kuongezeka kwa ubaguzi wa kiuchumi, kieneo na ukabila nchini Tanzania

Kitendo cha Nyerere kutoendeleza Butiama hakimuonyeshi Mwalimu kuwa ni mzalendo sana! Ni mapungufu yake, kama mapungufu mengine waliyonayo watu wengine...
Muwamba ngoma hata mada hupindishia kwake.
 
Tatizo ni huu unafiki wa kushindwa hata kusema tatizo unaloliona na nani anapendelewa. Sema ni nani ili tujadili na kukemea tatizo. Unaogopa hata kusema unachofahamu kwa majina bandia!! Cowardice!...
Mkuu umeongea ukweli mtupu
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu
Si kwamba hajui kinachoongelewa, tatizo wengine wanataka kudadavuliwa kila kitu na kuwa spoon fed.
Anaita ati ni cowardice, mie naita tact.
Explain the situation and intelligent persons figure it out.
 
Kamwe nashindwa kupita kimyakimya kwenye mada kama hii inayosononesha moyo.

Wakati huo huo, karibu kila mtu anaimba "Tano Tena", kama utani vile!

Sijui nchii imepatwa na janga gani.

Ni kama wote tumepigwa ganzi tusitambue ni nini hasa kinatokea.

Mimi sijui ni nani atakayekuja kututapisha sumu hii tuliyoonjeshwa sasa, ili taifa letu liendelee kuwa taifa lenye mshikamano kama aliouacha Mwalimu Nyerere.

Eeenh, sasa Mwalimu hata anasimangwa. Wale watoto nao wamekuwa kama mazuzu vile, wanatafuta ulaji, wanapoukosa wanaambiwa sababu ni kuwa baba yao hakufanya kitu nyumbani kwao!
Maneno mazito mkuu!
Surely tunapita katika tanuru tusilolijua.
 
Kamwe nashindwa kupita kimyakimya kwenye mada kama hii inayosononesha moyo.

Wakati huo huo, karibu kila mtu anaimba "Tano Tena", kama utani vile!

Sijui nchii imepatwa na janga gani.

Ni kama wote tumepigwa ganzi tusitambue ni nini hasa kinatokea.

Mimi sijui ni nani atakayekuja kututapisha sumu hii tuliyoonjeshwa sasa, ili taifa letu liendelee kuwa taifa lenye mshikamano kama aliouacha Mwalimu Nyerere.

Eeenh, sasa Mwalimu hata anasimangwa. Wale watoto nao wamekuwa kama mazuzu vile, wanatafuta ulaji, wanapoukosa wanaambiwa sababu ni kuwa baba yao hakufanya kitu nyumbani kwao!
Nakubaliana mkuu.
Ile dhamira njema inayoitwa resolve, lazima iendane na fairness na goodwill.
Mwalimu alijaribu sana kubalance haya mambo.
 
Nakubaliana mkuu.
Ile dhamira njema inayoitwa resolve, lazima iendane na fairness na goodwill.
Mwalimu alijaribu sana kubalance haya mambo.
"Resolve" ya kutokiuka taratibu zilizowekwa kupata hiyo "fairness" ikiachwa ifanye kazi bila ya kuingiliwa na mtu mmoja mwenye madaraka yote, hapo patakuwa na utulivu wa hali ya juu.
 
Kanda ya ziwa sasa hivi naona neema imewajia mpaka kwenye teuzi
 
Tulikuwepo wakati wa upendeleo wa wazi wakati CD akipendelea kwao na baadaye kukemewa na Mwalimu.
Huwezi pindisha historia.

Na Mwalimu in exasperation aliwahi kusema.”Nimekuwa na Mwaziri wakuu wengi, pamoja na Waziri Mkuu wa Mwanga..”
It was a rebuke!

Haya tunayoyaona sasa yana ulinganishi.
kaka hebu tueleze miradi ya maendeleo iliyopelekwa jimbo la mwanga kwa upendeleo ni ipi? unasema wewe ulikuwepo wakati cleopa msuya anawahujumu watanzania sasa hebu tupe walau mifano miwili mitatu ili kuthibitisha madai yako.

binafsi simpendi cleopa msuya kwasababu ya siasa zake chafu, yeye na kundi lake, ktk kumpiga vita chediel mgonja. msuya alikuwa hawezi kupambana na mgonja ktk majukwaa na sanduku la kura akaamua kumfanyia figisu na hujuma. lakini pamoja na hayo siwezi kumsingizia cd msuya kwamba alipendelea jimbo la mwanga, au aliwahujumu watanzania.

msuya alikuwa anapigwa vita kwenye chama na serikalini kwasababu alikuwa mchapakazi na aliaminiwa na Mwalimu Nyerere na Mzee Ali Hassan Mwinyi. pia cd msuya ni msemakweli na mwenye misimamo. sasa wakati mwingine misimamo yake ilikuwa inakinzana na wafia chama. msuya kwa background yake ni civil servant hivyo hakuwa na tabia za kupiga siasa, yeye ni mtu wa facts zaidi.

huyu cd msuya mnayempiga vita na kumzushia ndiye ambaye Mzee Kikwete aliyemuita "baba wa mageuzi ya uchumi Tz." Mzee Mwinyi anasifiwa kwa kuikwamua Tz ktk mporomoko wa kiuchumi. waziri wa fedha na mipango wa Raisi Mwinyi alikuwa CD Msuya. Baba wa Taifa anakumbukwa kwa kujenga viwanda nchi nzima. sasa waziri wa kwanza aliyepewa jukumu la kutekeleza blue print ya viwanda Tz baada ya kuvunjika kwa EAC alikuwa ni CD Msuya.

utendaji na ufanisi wa cd msuya kama mbunge wa kuchaguliwa jimboni, unafanana na utendaji na ufanisi wa mzee jackson makweta aliyepata kuwa mbunge wa njombe. wote walikuwa na tabia ya kuhamasisha wananchi kujitolea ktk shughuli za maendeleo badala ya kubweteka, kubembeleza, na kusubiri huruma ya serikali. kwa mfano, kama wananchi wake walihitaji zahanati cd msuya aliwahimiza wajitolee kujenga mpaka hatua ya kupaua, na baada ya hapo ndio waombe msaada wa mbunge au serikali. utaratibu huu cd msuya na jackson makweta waliyaanza zamani sana.

cc Gerald .M Magembe, Masamila
 
Tunaishi nyakati unazizijua vema.

Na mada umeilewa vema ila una unafiki wa ku act kuwa a wounded guy.

Kisaikolojia umasikini wako unaamua kujihalalishia ubaguzi wako.

Refer kwa Mwalimu, nakupeleka SUNGURATEX Butiama, ingwaje kule wanalima pamba.

Hata barabara kwenda Butiama zilijengwa baada ya yeye kufariki.

Buhemba pale kuna dhahabu, lakini Mwalimu hakuweka umimi mbele.

Tunayoyaona yanashangaza.
Uzi kama huu umeuanzisha kwa sababu kubwa kuliko hizi bhla! bhla! kama ni hizi tu hukuwa bna sababu ya kuanzisha uzi JF.
 
Eti wahaya hawaalikani? Naona umelewa rubisi si bure.

Infact hao uliosema wamejaa CRDB na TRA wapo na walikuwepo na watazidi kuwepo
Hayo ndo majibu tunayoyataka. Tujadili badala ya kushitakiana. Kuna tabia watu wanafundishwa tangu wadogo ukitaka kuziondoa ukubwani lazima nguvu itumike.
 
Kila mtu alivyo ameundwa na jamii yake. Unaweza kumlaimu lakini na wewe jiulize una mchango gani kwa tabia ya huyo mtu
Mume alikuwa alikuwa natabia ya kudharau na kuponda kila alichofanya mke. Hatimaye mke taratibu alijenga tabia fulani dhidi ya matendo ya mme. Tabia ilikomaa mwisho ikawa majanga.
Hivo tunashangilia kila kitu tujue tunaumba kitu pia baade tunamnyooshea mtu kidole.
 
Uzi kama huu umeuanzisha kwa sababu kubwa kuliko hizi bhla! bhla! kama ni hizi tu hukuwa bna sababu ya kuanzisha uzi JF.
Anzisha wewe basi uzi wenye madini tuuone.
Blank head!
 
huu ni UONGO. hebu tueleze wilaya ya mwanga ina kitu gani cha ajabu ambacho kimepelekwa na msuya na mbunge mwingine hawezi kukipeleka. msuya ndiye aliyepewa jukumu la kujenga viwanda baada ya jumuiya ya afrika mashariki kuvunjika. je, mwanga kuna kiwanda chochote kile? kuna gofu la kiwanda kilichojengwa enzi za mwalimu na msuya? barabara za milimani zinazowashangaza wengi zilijengwa na wafumwa wakati wa mkoloni.

Hii habari ya kusema wapare walipendelewa ni uongo uongo uongo. wapare wa kusini wana barabara ya mkomazi mpaka same wanalia mpaka kesho kwamba haijajengwa kiwango cha lami. na hiyo ndiyo barabara kongwe nchini lakini kila raisi anaipiga danadana kuijenga, halafu kuna mtu leo nimemsoma anasema daniel yona alipendelea same na wapare.

kilichowainua wapare ni uamuzi wa wafumwa kuchangamkia elimu kwa kila mtoto ambao ulitekelezwa kwa majaribio wakati wa mkoloni. uamuzi huo ndio uliopelekea wapare wathamini elimu hata ya mtoto wa kike. wakati tunapata uhuru Waislamu wa Upare walikuwa na shule zaidi ya 20, wakati Waislamu nchi nzima wanaambiwa hawapendi kusoma.

Wapare walishawahi kuwa na gazeti lao habari za Upare. kingine kilichowainua ni tabia ya wapare kutoka maeneo walikozaliwa kwenda mijini kutafuta maisha na kutokusahau kwao. wapare waliotoka nje zamani ndio waliopeleka wazo la kupasua barabara za milimani wakati wa utawala wa wafumwa/ machifu.
Majivuno ya kikabila unatuletea, haya basi mmesoma sana nyie
 
Ubaguzi nchini una historia ya muda mrefu sana na kila uchao ubaguzi unazidi sasa makabila hivi makabila na jamii mbalimbali nchini at leat zinaanza kujielewa na kufanya kama wao walivyofanyiwa kipindi cha nyuma yaani malipizo,malipizo ambayo kimsingi ndo yanazidi kutuumiza na yanafayika kwa ubaya zaidi.....sasa miaka kadhaa baadae tutavuna tulichopanda kabisa , mana hadi sasa tunaona hasara za ubaguzi ulionza toka kipindi cha Uhuru,wapuuzi wachache waliokuwa viongozi enzi hizo walichukua faida ya umuhimu wao nchini na uzandiki ukaanzia hapo sasa wanadamu unakuta wanakusubiria kwenye pembe sahihi ili wakubomoe vizuri na ndo hapo kila anayepata nafasi anajaribu kufanya kile kilichafanywa miaka ya nyuma na pengine kuongeza ambapo kiuhalisia ni ujinga na upuuzi unaoturudisha nyuma kwa kufanya mambo ya jalalani.....
 
Una umri gani wewe? Upendeleo ulikuwepo miaka yote. Nahisi kuna watu upendeleo umewatega mgongo ndo maana wanalia lia! Walipopendelewa wakasema ni haki yao. tulieni nchi inyooke.
Ogopa Mungu kusema uongo nchi ilipendelewa wapi? Kama nchi ingependelewa na waliopita basi leo Mkoa wa Mara ungekuwa nchi kamili kwa sababu una kila kitu cha kuifanya kuwa nchi kuliko Burundi na Rwanda,Zanzibar yangekuwa makao makuu ya nchi ya Tanzania,Mtwara kungekuwa na miundo mbinu inayojitosheleza kuliko mikoa mingine na Bagamoyo ingekuwa Bandari kuu kuliko Dar es Salaam na shughuli za kiserikali zingeamia huko.
 
Ubaguzi nchini una historia ya muda mrefu sana na kila uchao ubaguzi unazidi sasa makabila hivi makabila na jamii mbalimbali nchini at leat zinaanza kujielewa na kufanya kama wao walivyofanyiwa kipindi cha nyuma yaani malipizo,malipizo ambayo kimsingi ndo yanazidi kutuumiza na yanafayika kwa ubaya zaidi.....sasa miaka kadhaa baadae tutavuna tulichopanda kabisa , mana hadi sasa tunaona hasara za ubaguzi ulionza toka kipindi cha Uhuru,wapuuzi wachache waliokuwa viongozi enzi hizo walichukua faida ya umuhimu wao nchini na uzandiki ukaanzia hapo sasa wanadamu unakuta wanakusubiria kwenye pembe sahihi ili wakubomoe vizuri na ndo hapo kila anayepata nafasi anajaribu kufanya kile kilichafanywa miaka ya nyuma na pengine kuongeza ambapo kiuhalisia ni ujinga na upuuzi unaoturudisha nyuma kwa kufanya mambo ya jalalani.....
Ulisoma Historia ya wapi wewe? Mikoa kama Kilimanjaro,Kagera,Mbeya na Arusha walinufaika sana kutokana na vipaumbele vya wakoloni kwenye mikoa hiyo,walianzisha shule nyingi huko,hospitali na huduma mbalimbali za jamii kiasi kwamba hata baada ya uhuru sehemu hizo kulikuwa na ustaarabu wa kutosha kuweza kuwanyanyua kimaisha,lakini ustaarabu huu tunaoulazimisha sasa kuna siku utakuja kuliponza taifa.
 
Huyo alikuwa mwalimu. Kila mtu na muono wake. Viongozi hawafanani. Hatuwezi kurudia mapungufu yaliyofanywa na viongozi wakuu waliopita. Nasema never ever.
Tunaishi nyakati unazizijua vema.

Na mada umeilewa vema ila una unafiki wa ku act kuwa a wounded guy.

Kisaikolojia umasikini wako unaamua kujihalalishia ubaguzi wako.

Refer kwa Mwalimu, nakupeleka SUNGURATEX Butiama, ingwaje kule wanalima pamba.

Hata barabara kwenda Butiama zilijengwa baada ya yeye kufariki.

Buhemba pale kuna dhahabu, lakini Mwalimu hakuweka umimi mbele.

Tunayoyaona yanashangaza.
 
Ogopa Mungu kusema uongo nchi ilipendelewa wapi? Kama nchi ingependelewa na waliopita basi leo Mkoa wa Mara ungekuwa nchi kamili kwa sababu una kila kitu cha kuifanya kuwa nchi kuliko Burundi na Rwanda,Zanzibar yangekuwa makao makuu ya nchi ya Tanzania,Mtwara kungekuwa na miundo mbinu inayojitosheleza kuliko mikoa mingine na Bagamoyo ingekuwa Bandari kuu kuliko Dar es Salaam na shughuli za kiserikali zingeamia huko.
Hukumuelewa!
 
Back
Top Bottom