Kamwe nashindwa kupita kimyakimya kwenye mada kama hii inayosononesha moyo.
Wakati huo huo, karibu kila mtu anaimba "Tano Tena", kama utani vile!
Sijui nchii imepatwa na janga gani.
Ni kama wote tumepigwa ganzi tusitambue ni nini hasa kinatokea.
Mimi sijui ni nani atakayekuja kututapisha sumu hii tuliyoonjeshwa sasa, ili taifa letu liendelee kuwa taifa lenye mshikamano kama aliouacha Mwalimu Nyerere.
Eeenh, sasa Mwalimu hata anasimangwa. Wale watoto nao wamekuwa kama mazuzu vile, wanatafuta ulaji, wanapoukosa wanaambiwa sababu ni kuwa baba yao hakufanya kitu nyumbani kwao!