nizakale
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,035
- 2,938
CD aliamuru hosipitali ya wilaya ya Mwanga kujengwa kijijini kwake Usangi. Usijitoe ufahamu.
huu ni UONGO. hebu tueleze wilaya ya mwanga ina kitu gani cha ajabu ambacho kimepelekwa na msuya na mbunge mwingine hawezi kukipeleka. msuya ndiye aliyepewa jukumu la kujenga viwanda baada ya jumuiya ya afrika mashariki kuvunjika. je, mwanga kuna kiwanda chochote kile? kuna gofu la kiwanda kilichojengwa enzi za mwalimu na msuya? barabara za milimani zinazowashangaza wengi zilijengwa na wafumwa wakati wa mkoloni.
Hii habari ya kusema wapare walipendelewa ni uongo uongo uongo. wapare wa kusini wana barabara ya mkomazi mpaka same wanalia mpaka kesho kwamba haijajengwa kiwango cha lami. na hiyo ndiyo barabara kongwe nchini lakini kila raisi anaipiga danadana kuijenga, halafu kuna mtu leo nimemsoma anasema daniel yona alipendelea same na wapare.
kilichowainua wapare ni uamuzi wa wafumwa kuchangamkia elimu kwa kila mtoto ambao ulitekelezwa kwa majaribio wakati wa mkoloni. uamuzi huo ndio uliopelekea wapare wathamini elimu hata ya mtoto wa kike. wakati tunapata uhuru Waislamu wa Upare walikuwa na shule zaidi ya 20, wakati Waislamu nchi nzima wanaambiwa hawapendi kusoma.
Wapare walishawahi kuwa na gazeti lao habari za Upare. kingine kilichowainua ni tabia ya wapare kutoka maeneo walikozaliwa kwenda mijini kutafuta maisha na kutokusahau kwao. wapare waliotoka nje zamani ndio waliopeleka wazo la kupasua barabara za milimani wakati wa utawala wa wafumwa/ machifu.