uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 1,657
- 2,406
Kuna mambo mengine tukubali,kuna sehemu zilikuwa nyumaTusiposema sasa mawe yatasema.
Sasa hivi nchi inapitia ubaguzi wa wazi kieneo, ukabila na upendeleo wa wazi kwa sehemu fulani fulani nchini Tanzania.
Haya ni mambo ambayo Tanzania hatukuyazoea wala kushuhudia toka enzi za kupata uhuru.
Mwalimu alijishusha mno na hata hakupendelea kwao kwa jinsi tunavyoshuhudia sasa, mimi Butiama nimefika.
Ubaguzi wa aina yoyote una mwisho si mzuri kwa mustakabali wa Taifa.
Chama kimelala.
Bunge ndio kabisa.
Lakini wahenga wanasema tutavuna tunachopanda.
lazima hatua za kimakusudi zichukuliwe ili nao wajione wapo tanzania/zilisahaulika.
Ninachoamini ni kuwa hakuna barabara yenye lami inawekewa lami juu ya lami kisa ipo ukanda wa kiongozi fulani.
wala sehemu zenye miundombinu ya maji au umeme kuongezewa maboresho wakati kwingine hakuna miundombinu hiyo.
Tujifunze kuvumiliana tunapoona sehemu nyingine zinapigishwa hatua angalau kuelekea tulipo sisi tusijisikie vibaya.
Tanzania ni yetu sote tujitahidi kugawana kilichopo kwa usawa.