KERO Kuongezeka kwa Watendaji wanaokaimu nafasi za uongozi katika Halmashauri, tatizo ni nini?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la watumishi wanaokaimu nafasi za wakuu wa idara na vitengo mbalimbali katika halmashauri. Hali hii inazua maswali kuhusu utaratibu wa uteuzi na upatikanaji wa watumishi wenye sifa za kushika nafasi hizo.

Je, ni kweli katika wizara na taasisi zetu hakuna watumishi wenye sifa zinazostahili kupandishwa vyeo na kushika nafasi hizo moja kwa moja? Au kuna mazingira yanayowezesha baadhi ya watu kukaimu kwa muda mrefu kwa lengo la kutafuta sifa au kufanikisha uteuzi wao baadaye?

Kwa mfano, katika Masasi TC, Mkuu wa Idara ya Afya anayekaimu nafasi ya TMO ni mtumishi ambaye bado ni kijana. Hii inazua swali kama hakuna madaktari wengine wenye sifa na uzoefu wanaoweza kushika nafasi hiyo moja kwa moja, huku huyo anayekaimu akiendelea kutekeleza majukumu yake hadi atakapostahili kupandishwa cheo kwa kuzingatia uwezo na utendaji wake.

Mfano mwingine ni Newala TC, ambako kuna Mweka Hazina anayekaimu nafasi ya TFAO. Inadaiwa kuwa hali ya kukaimu imekuwa ikimfanya mtendaji huyo kujikita zaidi katika kutafuta kuthibitishwa katika nafasi hiyo, jambo ambalo linaweza kuathiri utendaji wa idara na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya shughuli zilizopangwa.

Kwa mujibu wa malalamiko haya, baadhi ya idara zinakabiliwa na changamoto za kupata fedha za safari za kikazi, malipo ya Extra Duty na utekelezaji wa mipango kazi iliyopitishwa.

Tunaomba Wizara na mamlaka husika zifanye tathmini ya utaratibu wa kukaimisha nafasi za uongozi. Ikiwa kuna watumishi wenye sifa zinazohitajika, kwa nini wasiteuliwe moja kwa moja badala ya kuwapa wengine nafasi za kukaimu kwa muda mrefu?

Kinachotia shaka zaidi ni pale nafasi inapokuwa wazi kutokana na kustaafu, kuhama au sababu nyingine, halafu badala ya kumpa mtu anayestahili kutoka katika kituo hicho nafasi ya kukaimu kwa muda, mtumishi huhamishwa kutoka kituo kingine ili akakaime. Hali hii inazua maswali kuhusu vigezo vinavyotumika katika uteuzi huo.

Tunaomba suala hili lifanyiwe uchunguzi na kuwepo kwa uwazi katika mchakato wa uteuzi na utekelezaji wa majukumu ya uongozi. Nafasi za uongozi zinapaswa kutolewa kwa kuzingatia sifa, uwezo, uzoefu na utendaji, ili kuhakikisha ufanisi wa halmashauri na kuondoa mianya ya upendeleo au matumizi mabaya ya madaraka.
 
Kuna wanaokaimu kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja lakini hawathibitishwi, wanaendelea kukaimu,,,yanashangaza
 
Back
Top Bottom