Kuongezeka kwa Wimbi la wanawake kuzalia nyumbani (kuzaa kabla ya kuolewa)

Kuongezeka kwa Wimbi la wanawake kuzalia nyumbani (kuzaa kabla ya kuolewa)

Kuna ongezeko kubwa la mabinti kuzalia home kwa wazazi kabla ya kuolewa.
Nimefanya utafiti ,majibu yangu yamejuwa na ukweli, Lakini sababu kubwa ni kutokana na
1. wanawake wengi kukata tamaa, 2.umri mkubwa,
3.lakini pia nimekutana na majibu ya wanawake waliamua kushika mimba baada ya kuhakikishiwa kuolewa,Lakini Mara baada ya kuzaa mwanaume amechange gia na kupiga U-turn
4. Wachache sana walionyesha ndoa sio muhimu kwao,Lakini asilimia kubwa ya kundi hilo walikuwa wameshaumizwa

Wanaume walipoulizwa katika madodoso yao sababu hasa za kuwapa ujauzito wanawake na kuwaacha wengi walijaza majibu haya
1. Majibu ya ovyo ya wanawake yaliwakimbiza wengi - 40% waijibu katika madodoso jibu hill
2. Dharau na kiburi kwa wanawake wengi walisababisha wanaume wengi kusitisha mahusiano ili hali tayari hayo mahusiano yalishaleta madhara kama mimba au mtoto.
3. Wanawake kuwa na mahusiano na wanaume/ wanaume wengine ilidabababisha pia mahusiano kusitishwa na wanaume -45% swali hili lilijibiwa
4. Wivu na tamaa , wanawake kuingia tamaa ya kutaka vitu vikubwa kama vile mavazi, n.k wanaume waliamua wajitoe kwenye mahusiano mapema
5. Wanaume wengi kutokuwa waaminifu katika mahusiano hasa kutokana na kuwepo kwa wanawake wengi wazuri ,imwsababisha wanaume wengi kukimbilia huko
Nadhani kuna kitu hukukidurusu yaani athari za usasa na ukosefu wa malezi ya kizamani kuhusiana na maadili ya maisha kwa ujumla au unyago. SIku hizi vijana wengi wanajiishia kama miti bila mafunzo ya namna ya kuishi kama tulivyoishi wazazi wenu. Usasa unawafundisha kujuajua wakati kuna mengi hamuyajui. Mie nitoe uzoefu wangu.Nilipeleka dada yenu chuo. Badala ya kukimbiza vitabu akakimbiza wanaume hadi wakamchoka na akaanza kuhisi anazeeka. Alipopata kibarua akaingia mkenge wa kuahidiwa kuolewa akabeba mimba. Mwanamke aliyefundwa hawezi kukubali ujinga wa kubeba mzigo kabla ya mwenye kutaka kumuoa kuchukua jumla. Mwingine alimtegeshea waliyekuwa wakiishi kinyumba bila kuoana wakaishia kutimuana na mwanamme akaoa mwanamke mwengine. Mwingine anataka kila kitu kitoke mtandaoni hasa mapishi. Badala ya muda alitimliwa. Kuna visa vingi wanangu.
 
Back
Top Bottom