Kuongezeka kwa Wimbi la wanawake kuzalia nyumbani (kuzaa kabla ya kuolewa)

Nadhani kuna kitu hukukidurusu yaani athari za usasa na ukosefu wa malezi ya kizamani kuhusiana na maadili ya maisha kwa ujumla au unyago. SIku hizi vijana wengi wanajiishia kama miti bila mafunzo ya namna ya kuishi kama tulivyoishi wazazi wenu. Usasa unawafundisha kujuajua wakati kuna mengi hamuyajui. Mie nitoe uzoefu wangu.Nilipeleka dada yenu chuo. Badala ya kukimbiza vitabu akakimbiza wanaume hadi wakamchoka na akaanza kuhisi anazeeka. Alipopata kibarua akaingia mkenge wa kuahidiwa kuolewa akabeba mimba. Mwanamke aliyefundwa hawezi kukubali ujinga wa kubeba mzigo kabla ya mwenye kutaka kumuoa kuchukua jumla. Mwingine alimtegeshea waliyekuwa wakiishi kinyumba bila kuoana wakaishia kutimuana na mwanamme akaoa mwanamke mwengine. Mwingine anataka kila kitu kitoke mtandaoni hasa mapishi. Badala ya muda alitimliwa. Kuna visa vingi wanangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…